JK kutumia Mkutano wa CCM kulihutubia Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kutumia Mkutano wa CCM kulihutubia Taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoto wa Mkulima, Oct 31, 2007.

 1. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  JK kutohutubia Taifa

  Habari Zinazoshabihiana
  • Njohole atakiwa Uswisi Jumatatu 31.08.2006 [Soma]
  • Matumaini ya wafanyakazi leo ni kwa Kikwete, Karume 01.05.2007 [Soma]
  • Mwananchi alia na Wabunge kukanyaga 'Bendera ya Taifa' 07.07.2006 [Soma]

  RAIS Jakaya Kikwete hatalihutubia Taifa mwisho wa mwezi huu kama utaratibu ulivyo, kwa vile anatarajia kutoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kuanza Jumamosi hii katika ukumbi wa Kizota, Dodoma.

  Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu, Dar es Salaam, ilisema katika hotuba hiyo ya ufunguzi, Rais anatarajiwa kutumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi wote kwa ujumla na kuelezea na kutoa ufafanuzi wa masuala muhimu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

  Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma leo, huku habari zikisema atatumia mkutano huo kujibu mapigo ya wapinzani.

  http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4386
   
 2. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu hapo inakuwaje? anahutubia taifa kwa kofia ya mkuu wa nchi au kwa kofia ya chama?
   
 3. S

  Si Kitiyi Member

  #3
  Oct 31, 2007
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni dharau, na inaonesha ni jinsi gani viongozi wetu wasivyojua kutofautisha majukumu na mamlaka ya chama na yale ya Serikali. Si mara ya kwanza kufanya hivyo, hata last time wakati kukiwa na mkutano wa Halmashauri Kuu kule Dodoma alifanya hivyo ingawa ilikuwa ni kwa style nyingine. Alisema anaongea na Taifa kupitia Mkutano wake na Wakazi/Wazee wa Dodoma, lakini akatumia muda mwingi sana kuongea mambo ya C.C.M.Hamkumbuki kipindi kile alipowaagiza wana C.C.M. kuwanyima kura wanaojinadi kupitia jina lake? Si hiyo ilikuwa wakati analihutubia Taifa? Sasa mambo ya C.C.M. wakati wa kulihutubia Taifa wapi na wapi? Dharau hiyo!!!!! Si wananchi wote ni wanachama wa C.C.M.
   
Loading...