The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,064
- 14,079
JK kutohudhuria mkutano wa EU
2007-12-06 10:30:19
Na Gaudensia Mngumi
Rais Jakaya Kikwete hatashiriki mkutano wa nchi za Afrika na Ulaya unaotarajiwa kuanza Jumamosi ijayo jijini Lisbon, Ureno.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais hatakwenda kwenye kikao hicho cha AU na EU kutokana na kutingwa na majukumu mengi ya kitaifa.
Wizara ilisema kuwa badala yake Rais amemteua Waziri wa wizara hiyo Bw. Bernard Membe kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo mkubwa na wenye umuhimu kwa Afrika ambapo pamoja na mambo mengine utazungumzia ajenda za ushirikiano wa kibiashara na namna ya kuisaidia Afrika kupambana na ongezeko la joto duniani.
Wajumbe watakaoambatana na Waziri Membe ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Bw. Ali Mzee Ali mwingine atakayekuwa kwenye msafara wa Tanzania ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Bi. Anna Abdallah.
Mkutano huo wa EU na AU utaanza Jumamosi hadi Jumapili wiki hii nchini Ureno na kwa upande mwingine Desemba 9 siku ambayo Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 46 ya Uhuru wa Tanganyika.
Mkutano huo ulikumbwa na changamoto nyingi ambapo Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown, ameususia kwa madai ya kupinga ushiriki wa Rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe.
Alisema hatakwenda Lisbon iwapo Rais Mugabe ataalikwa, lakini viongozi wa Afika walipinga vitisho hivyo na kusisitiza kuwa kama kiongozi huyo wa Zimbabwe hatashiriki nao pia wataususia.
SOURCE: Nipashe