JK kutengeneza Mabilionea 100 watanzania 1015, New York

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
JK kutengeneza Mabilionea 100 watanzania 1015, New York

Rais Jakaya Kikwete amesema huu ndiyo mpango wake hata kama atakuwa ametoka madarakani, mazunguzo haya yalifanyinka nchini marekani katika ziara yake ya mwaka huu Sep.2007,

akimkabizi muheshimiwa R.Mengi kazi hiyo ili kuweza kutafuta pesa za kuwasaidia wafanyabiasha hao ambao wata saidia wengi kwa kiasi kikubwa, kwa mimi niliona nimpango mzuri sana tuweze kuwa na watanzania mabilionea na kushika sehemu muhimu za uchumi wa nchi yetu ikiwa nipamoja na madini, utalii, elimu, na nyingine zilizoka Tanzania.

Muh. Mengi aliuliza pesa atapata wapi JK akamuwambia sijui nikazi nimekupa,

pesa hizo zitakuwa zina kopeshwa wafanyabiashara kwa vikundi na ni kiasi kukubwa na siyo pesa kidogo,

Rais aliongea kwa uchungu akisema uchumi wetu umeshikiliwa na wageni wakati sisi hatuna kitu,
katika safari yake hii haikuwa na wafanya biashara wakigeni kwasababu wao hawana shida na safari kama hizi

kwawale wanao jua hii habari zaidi basi watanisaidi kuongezea haya ndiyo ninayo kumbuka tu.

asanteni
 
hahahahahhaaahaa ahah ahahaha...bro naona hii ni zile section ya nyepesi
 
Mimi naona hii ni nzito kama kweli ana lengo hili nadhani ni lengo la busara sana. Lakini utekelezaji wake ni vipi?
 
I think last week alipokuwa nchini aliona Forbes list ya billionea then imemchanganya. You cant have that list with 100% corruption cabinet, poor monetery system.... Mr President wake up, your in deep sleep.... You just dreaming
 
Hi Jamani hivi mabilionea wanatengenezwaje?? Au yasije wakawa mabilionea kama wa Zimbabwe!! Inflation juu, thamani ya pesa chini then watu wanakuwa mabilionea. Dalili zisha anza kujitokeza TZ. Ha ha ha ha a a a !!!!!!
 
Swala hapa mabilionea kwa kipimo gani THS? au USD, Yen , Yuan etc. Kwa TSHS inawezekana kabisa
 
Mabilionea 100 ?? nadhani ni kutafuta orodha ya wengine 89 maana moja kwa moja 11 wanaweza kuwa wale wa kwenye orodha ya Dr. Slaa. Atafanikiwa tuu,kwani ni suala la kuwashawishi wale walio waliojichotea fedha za umma kwa mabilioni na kujiwekea ktk mabenki ya Ulaya na kwingineko kuzihamishi New York na adhima yake kuwa imetimia.Ila namshauri Mengi kuwa hisia za wananchi wengi ni kuwa yeye ni msafi,aangalie favor anazozipata zisije mchafua maana ukitumbukia kwenye pipa la lami! mpaka utakate.....mhh.
 
muungwan keshapoteza muelekeo,ameghafirika na mambo yabnavyoenda kombo,nawaomba wana wa watanzania mumuombee japo apate wabunge wachache 2010 kutoka chama chake,thena atawashughulikia kina karamagi
 
Hi Jamani hivi mabilionea wanatengenezwaje?? Au yasije wakawa mabilionea kama wa Zimbabwe!! Inflation juu, thamani ya pesa chini then watu wanakuwa mabilionea. Dalili zisha anza kujitokeza TZ. Ha ha ha ha a a a !!!!!!

Mr. Zero, Mambilionea wanatengenezeka ndugu yangu. Kinachotakiwa ni nia thabiti ya kuwatengeneza. Nchi nyingi za Asia zimeendelea sana kwa kufuata utaratibu wa kutengeneza matajiri wakubwa. Matajiri ambao waliweza kubuni na kusimamia biashara kubwa sana kwenye nchi zao na hata kutoka nje ya mipaka ya nchi zao. Mifano ipo kwenye Tiger Economy (Malaysia, Indonesia n.k). Sisi pia tunaweza. Tatizo ni uwezo wetu wa kuvumilia kuona wenzetu wakitesa tu basi.
 
Wana JF; Mh.Rais wetu yuko sahihi ktk hilo,tusipende kusahau mapema kiasi hiki jamani,nakumbuka sana misimamo yake alipokuwa anaelezea matumaini yake,muungwana ni mshabiki mkubwa sana wa yule mtalaalam wa Malaya ambaye alikuwa Primier wao (Mahathir).

Mageuzi ya Malaya yalichagizwa na mikakati mingi shirikishi ikiwemo hili analolilia Mheshimiwa Rais wetu.

Anaumizwa na umaskini wetu kwa dhati ,nadhani sasa wakati umefika Wana JF kulizungumza hili kwa udhati sana.

"The only thing we have to fear is fear itself." – FDR
 
Bwana Mdogo punguza ukali wa maneno maana sasa unaashiria hasira yako ni mbaya but nakubaliana sana mtizamo wa Tiger Countries. JK analiona hilo kwa upana sana ila tatizo ni Je tuko tayri kuona hao 100 wakiibuka na sisi tukawaunga mkono? Mzindakaya tu tayari keshaitwa Fisadi ila mnasahau marehemu Johnson wa Jamhuri ya Kenya anamiliki sehemu kubwa ya ardhi ya Kenya lakini Sumaye alipopewa pori kule Morogoro ikawa kashfa tele na zaidi mkathubutu kusahau kuwa msomi huyu wa kilimo toka Kenya ajira yake ya kwanza ilikuwa ni wilayani Kilombero morogoro.

Ktk hili Amiri Jeshi wetu- songa mbele usirudi nyuma.
 
Hizo ndungu yangu nadhani ni habari nyepesi nyepesi na kama sio basi mh. Rais (muuza sura) aache kutudanganya sisi watanzania kwani sio watoto wadogo.. ile mikopo ya tsh 15million (mkopo wa kikwete) umeishia wapi??????? nani kapata?????? je yeye anataka wafanya biashara wakopeshwe swali je vipi kuhusu wale wamachinga waliowabomorea vibanda vyao au hao sio wafanya biashara??????? JE lile swala la ajira milion moja limeishia wapi?????? MH. RAIS (MUUZA SURA) ACHA KUONGEA VIPI BILA YA KUTEKELEZA WEWE KAZI YAKO NI KUONGEA TUUUUUUUUUU, AHADI KIBAO LINI UTAZITEKELEZA???? AU MPK UINGIE KABURINI NDIO UTAZITEKELEZA. imefikia wakati watanzania tuamke na tuache kudanganywa hovyo. mimi nimeshachoka kabisaaaaaaaa..
 
Swala sio kuumizwa na umaskini wetu, swali ni what is he DOING about our poverty?

Hakuna anayetegemea miracle kutoka kwa JK, what we want from him tunataka Rubani thabiti mwenye vision, nchi huwezi kuiendesha kiushkaji hata siku moja jamani! Jk anacheza sana faulo kuwakumbatia watu wasiozidi hamsini at the exepense ya watu million 38 waliompigia kura! Its a shame and morally unconscionable! Watu wenyewe ndo wamechoka ile mbaya!

Iweje mpaka leo uhusiano wa mlalahoi na serikali yake ni kipindi chakupiga kura tuu? Inabidi viongozi wetu wakubali kwamba wakati umefika sasa wa kutusikiliza na sisi, kila mtu ana uwezo wa kuwa na fikira mbadala kwa maendeleo ya wote na sio Karamagi na wateule wachache.

Trust me, viongozi wetu wamesahau kwamba siku hizi INFORMATION IS POWER, tulikuwa tunanyimwa habari sasa na internet ndo kabisaaa tuko sambamba na ujinga wao. NO SOCIETY WHICH CAN BE STUPID FOREVER and TANZANIA WE ARE INCREASINGLY PROVING THAT TO OURSELVES AND THE WORLD!
 
Wana JF; Mh.Rais wetu yuko sahihi ktk hilo,tusipende kusahau mapema kiasi hiki jamani,nakumbuka sana misimamo yake alipokuwa anaelezea matumaini yake,muungwana ni mshabiki mkubwa sana wa yule mtalaalam wa Malaya ambaye alikuwa Primier wao (Mahathir).

Mageuzi ya Malaya yalichagizwa na mikakati mingi shirikishi ikiwemo hili analolilia Mheshimiwa Rais wetu.

Anaumizwa na umaskini wetu kwa dhati ,nadhani sasa wakati umefika Wana JF kulizungumza hili kwa udhati sana.

"The only thing we have to fear is fear itself." – FDR
ACHA porojo ! Anaumizwa na umasikini wetu kwa dhati? are joking? kama angekuwa anauchungu huo angewabeba wanaozalisha umasikini kwa mbeleko ya cheo chake? Kama kweli angekuwa na uchungu angechukua hatua za dhati dhidi ya viongozi wachafu. Elewa hata kutuhumiwa sana kuwa wewe ni mwizi kunakukosesha sifa ya uongozi sio lazima mpaka ushahidi,maana kwa wadhifa alionao kiongozi anaweza kupoteza ushahidi wote wa kimahakama lakini anaowaongoza wanajua kabisa yeye mwizi tuu.
Tukumbuke kuwa pengine mimi na wewe hatupo katika kundi la maskini,lakini ni wangapi wanataabika,kufa ,kukosa huduma za msingi kama binadamu katika nchi hii iliyojaliwa neema mbalimbali za asili? Hamjui kuwa imefika wakati Twiga,fisi na wanyama wengine wana uhakika na maisha yao Kule Ngorongoro na Serengeti kuliko baadhi ya Watanzania wenzetu vijijini? AIBU ya kiasi gani hii !! Halafu tunakuja na longolongo za eti viongozi wana uchungu na umasikini!
Lazima wale ambao hawana na hawajui pa kusemea,tuwasemee kwa sauti kubwa nao waje wafaidi neema ya nchi yao kabla ya vifo havijawachukua.Huo ndio uzalendo. HAITOSHI KUJIITA MTANZANIA HUKU NDUGUZO WANANYANYASIKA KTK NCHI YAO.
Kutetea UOZO ni AIBU,AIBU AIBU
 
Sijui ni USANII au ni kutokujua, lakini matendo ya watu katika serikali yake hayaendani na hayo maneno yake.

Wengine tumesumbuka kweli kutaka kuongea na Muungwana juu ya matatizo ambayo wawekezaji wazalendo wanapata Tanzania lakini
hata barua tu wanashindwa kujibu.

Labda amejifunza na kama amempa Mengi hiyo kazi basi litakuwa jambo la maana sana. Nina imani kubwa na Mengi kama mzalendo na pia mchango wake kwenye kutengeneza ajira Tanzania hauna mfano.

Huenda JK kuna mambo mengi sana hajui yanayotokea pale karibu na yeye. Kuna vijana wengi sana ambao wanataka kufanya biashara za maana lakini kwa mfumo wa sasa wa banks TZ sio rahisi kabisa labda kama ni mtoto au ndugu wa kigogo.
 
hizi ni porojo tuu wakuu na kama yuko serious na haya nafikiri hazimtoshi huyu mndengereko na matajiri hawatengenezwi na serikali la sivyo Salma na Ridhwani wangekuwa mabilionea kuliko kugombea NEC kule kwa wamakonde
 
Koba,

Anachosema rais kinawezekana. Kutengeneza mabilionea haina maana
kuchukua watu anaowataka yeye na kuwapa mabilioni ya kutumia.

Kinachotakiwa ni kuwa na utaratibu ambao unawasaidia na kuwajengea mazingira mazuri Entrepreneurs ili waweze kufanikiwa.

Hayo ndio mambo yanayofanyika huku Ulaya na Asia, ukiwa na mawazo ya maana, kuna vyombo vya kuyapima na wakiona yanafaa basi unapewa kila aina ya msaada.

Kwa TZ ni tofauti, hata uwe na wazo zuri kiasi gani kama hutaki kutoa rushwa au huna vigogo bank wa kukusaidia hutapata msaada unaoutaka.

Kama rais ameliona hili na anataka kusaidia ni jambo zuri, ila tu
matendo yake na serikali yake kwa miaka miwili iliyopita hayanifanyi niwe optimistic. Huenda ni usanii tu mwingine.
 
Wana JF; Mh.Rais wetu yuko sahihi ktk hilo,tusipende kusahau mapema kiasi hiki jamani,nakumbuka sana misimamo yake alipokuwa anaelezea matumaini yake,muungwana ni mshabiki mkubwa sana wa yule mtalaalam wa Malaya ambaye alikuwa Primier wao (Mahathir).

Mageuzi ya Malaya yalichagizwa na mikakati mingi shirikishi ikiwemo hili analolilia Mheshimiwa Rais wetu.

Anaumizwa na umaskini wetu kwa dhati ,nadhani sasa wakati umefika Wana JF kulizungumza hili kwa udhati sana.

"The only thing we have to fear is fear itself." – FDR

Kumbuka kwamba JK alipata kura asilimia 80 kwa sababu hizi hizi za usanii...maneno matamu matamu anayosikia wapinzani wanasema kukosoa serikali, ambayo yanavutia masikioni mwa wasikilizaji, naye anayesema ku-win support. Naona baadfhi yetu hapa wameyasikia na wameanza kulegea! Swali ni je, yote hayo aliyokwishasema huko nyuma, yanafanana na matendo ya serikali yake? Au na sisi tunakuwa kama wale wanaosema "rais ana nia nzuri lakini wasaidizi wake ndio wanamkwamisha!" Aliwapata wapi hao wasaidizi? Nani alimlazimisha kuwa nao? Hajagundua kwamba 'wanamkwamisha?' Au ndiyo makubaliano yao? Mbona anazidi kuwabeba?
 
...hana lolote msanii tuu,akimkomesha Balali na mikataba fake ndio nitaanza kumsikiliza kidogo
 
Wana JF; Mh.Rais wetu yuko sahihi ktk hilo,tusipende kusahau mapema kiasi hiki jamani,nakumbuka sana misimamo yake alipokuwa anaelezea matumaini yake,muungwana ni mshabiki mkubwa sana wa yule mtalaalam wa Malaya ambaye alikuwa Primier wao (Mahathir).

Mageuzi ya Malaya yalichagizwa na mikakati mingi shirikishi ikiwemo hili analolilia Mheshimiwa Rais wetu.

Anaumizwa na umaskini wetu kwa dhati ,nadhani sasa wakati umefika Wana JF kulizungumza hili kwa udhati sana.

"The only thing we have to fear is fear itself." – FDR

Swala si kuumizwa na umasikini wetu Watanzania kwa maneno ya kusema tu. Je action gani amechukua?? Hatuoni nia ya dhati ya kama kweli anaumizwa na umasikini wa watanzania. Angekuwa anaumizwa kweli kweli na huo umasikini tungeshaona jitihada za kuwasaidia. Mi nafikiri alikuwa anaumizwa na umasikini wa maswahiba wake akina karamagi, Balali na nk. ndo maana amewaruhusu wachote size yao wakitosheka waache wenyewe.Huoni hata kwenye ile team ya LIST OF SHAME yumo???tena ni first eleven. naye ni mchezaji wa kutumainiwa???
 
Back
Top Bottom