Elections 2010 JK kutangazwa Rasmi Kesho, Kuapishwa Jumamosi!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Matokeo ya Urais kwa Majimbo Tanzania, yanakamilika usiku huu ambapo mshindi JK atatangazwa rasmi kesho saa 10 jioni pale kwenye viwanja vya Karimjee na kuapishwa Rasmi Jumamosi Saa 4:00 asubuhi kwenye Uwanja wa Taifa.

Tegemea kuwaona kina Dovutwa, Mziray, Mtamegwa, Rungwe na Lipumba, wakiwa kwenye colourful dress tayari kumpongeza JK kwa genuine smilling faces.

Dr. Slaa anatakiwa sana awepo. Mlio karibu nae, mshaurini asisusie, kweli asisaini kuyakubali matokeo, lakini awepo mahali hapo kuwasilisha live protest yake kwa wahusika for the sake of umoja wa kitaifa.
 
mkuu Pasco naona kazi ya "kumpa kikwete" awamu ya pili mmeimaliza. Hongera zenu.

What's next?
Kwa nini mnataka sasa Dr Slaa awepo kesho?
 
mkuu Pasco naona kazi ya "kumpa kikwete" awamu ya pili mmeimaliza. Hongera zenu.

What's next?
Kwa nini mnataka sasa Dr Slaa awepo kesho?
Naomba niji quote..
Wanabodi,
Dr. Slaa anatakiwa sana awepo. Mlio karibu nae, mshaurini asisusie, kweli asisaini kuyakubali matokeo, lakini awepo mahali hapo kuwasilisha live protest yake kwa wahusika for the sake of umoja wa kitaifa.
 
asipokuwepo nitashangaa kweli na nitamwona hafai kuwa kiongozi!kwa hayo majimbo matatu aliyolalamika ameibiwa kura hata akipewa kura zote bado hashindi tu!
 
Kama uchakachuaji haukuwepo basi aende.....Kama ulikuwepo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa then asiende,simple as that.
Akiamua tofauti na options hizo hapo juu,basi wengi watazidi kudhani kuwa haya mambo ya siasa za bongo ni viini macho tu.
 
asipokuwepo nitashangaa kweli na nitamwona hafai kuwa kiongozi!kwa hayo majimbo matatu aliyolalamika ameibiwa kura hata akipewa kura zote bado hashindi tu!

kama mna hakika na kura zenu, kwa nini mnakataa kurudia kujumlisha (sio kuhesabu) kura kwa kutumia kura zilizopatikana kila kituo?
 
Hiyo live protest ataifanya vipi?

Umoja wa kitaifa wakati mafisadi wakianzisha utawala wa kidikteta Tanzania?

Pasco, uko serious?
Mwafrika, kama Seif ameweza kukubali, why not Dr. Slaa.

Sherehe ya kesho kutangaza matokeo, washindwa wanapewa fursa ya kuongea, ndipo mshindi anatoa hotuba ya shukrani, Dr anatakiwa aitumie chance hii kutoa dukuduku lake.
 
Seif kapewa ulaji.... anaamini kuwa atawasilisha matatizo ya wapemba vizuri right now (chukulia kuwa Shein ni mpemba).

Upande wa JMT, hali ni tofauti.
Walichokifanya ccm na mafisadi wa NEC ni zaidi ya maelezo. Dr Slaa kwenda huko ni ku-dignify upuuzi.

Kama ni kuongea, Dr Slaa anaweza kuitisha mkutano wa waandishi wa habari anytime na akasema chochote kile anachotaka kusema.

BTW- kulingana na sheria za nchi, baada ya NEC kutangaza matokeo kesho, ndiyo imetoka hivyo.

Hakuna appeal au chochote kitakachobadili matokeo.

Ndo maana nimebadili signature yangu from now on
 
this is news which is not news.

mkwere katuibia kura ili ashinde kwa kishindo; na wabunge wasitimie kukwamisha hoja bungeni.
 
asipokuwepo nitashangaa kweli na nitamwona hafai kuwa kiongozi!kwa hayo majimbo matatu aliyolalamika ameibiwa kura hata akipewa kura zote bado hashindi tu!

Kama mlijua hawezi kushinda kwa hayo majimbo matatu mbona mmeiba????
 
Mwafrika, kama Seif ameweza kukubali, why not Dr. Slaa.

Sherehe ya kesho kutangaza matokeo, washindwa wanapewa fursa ya kuongea, ndipo mshindi anatoa hotuba ya shukrani, Dr anatakiwa aitumie chance hii kutoa dukuduku lake.
Alfa lela ulela,ama pia ni sawa na hamnazo tu,i mean whatever you're suggesting doesn't make no sense at all....Hapo si pahala pake unless you're referring to "ze comedy"
Kama matatizo yaliyotokea ni madogo madogo basi aende,lakini kama haki imepindishwa na uchakachuaji umeathiri matokeo,then proposal yako samahani sana ni ya kitoto.
 
hakuna haja ya kwenda kama mtu kashinda ushindi wa kipuuzi

Dr Atakuwa anajishushia P yake kwenda katika ujinga kama HUU

Mrema,Dovutwa na LIPUMBA nd o waende
 
count year 1..............................year2..............................year3......................................year4....................year5..............ooops kazi ipo.yabidi tumuombe sana njia pekee ya kujiokoa kwa uzembe hatutoweza mola tumuombe saaaaaaaaaana...............................matatizo kotekote mambo yetu yaenda mrama.............bila nguvu zake yeye hakuna liendalo sawa.
 
Mwafrika, kama Seif ameweza kukubali, why not Dr. Slaa.

Sherehe ya kesho kutangaza matokeo, washindwa wanapewa fursa ya kuongea, ndipo mshindi anatoa hotuba ya shukrani, Dr anatakiwa aitumie chance hii kutoa dukuduku lake.
Pasco usitake kutufanya hatuna kumbukumbu anakumbuka Seif 1995 na 2000 aliwahi si kususa tu kununa kwa miaka minne yeye pamoja na wawakilishi wake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom