JK kushindwa kuteua wakuu wa wilaya kwa zaidi ya mwaka kunatokana na CCM kupungukiwa makada?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,784
12,226
Tangu ulipomalizika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wilaya nyingi hazina wakuu wa wilaya kwa sababu mbalimbali na hivyo kusababisha baadhi ya wakuu wa wilaya kukaimu zaidi ya wilaya moja.

Katika hali ya kawaida inashangaza sana kwani kuna makada wengi ambao wanamaliza soli bila kuwa na hakika ya mlo wa kesho!

Je kucheleweshwa uteuzi wa wakuu wa wilaya kunaweza kuwa kunasababishwa na JK kutokuwaamini makada wake wengi wa CCM au CCM imeishiwa watu wenye sifa za kuwa wakuu wa wilaya?
 
tangu ulipomalizika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wilaya nyingi hazina wakuu wa wilaya kwa sababu mbalimbali na hivyo kusababisha baadhi ya wakuu wa wilaya kukaimu zaidi ya wilaya moja.

Katika hali ya kawaida inashangaza sana kwani kuna makada wengi ambao wanamaliza soli bila kuwa na hakika ya mlo wa kesho!

Je kucheleweshwa uteuzi wa wakuu wa wilaya kunaweza kuwa kunasababishwa na jk kutokuwaamini makada wake wengi wa ccm au ccm imeishiwa watu wenye sifa za kuwa wakuu wa wilaya?
ccm haijaishiwa makada ila makada wa mtandao wameisha hivyo kikwete ana mashaka na makada nje ya mtandao uliomuweka madarakani. Hiyo ndiyo siri yake
 
Nampongeza sana Kikwete kama hatoteuwa Wakuu wa Wilaya maana hawana kazi yoyote zaidi ya kututia hasara tu kodi za wananchi.
 
Nampongeza sana Kikwete kama hatoteuwa Wakuu wa Wilaya maana hawana kazi yoyote zaidi ya kututia hasara tu kodi za wananchi.

Bila shaka hili ni pendekezo lako katika katiba mpya ijayo kuwa nafasi ya ukuu wa wilaya ifutwe na badala yake wenyeviti wa halmashauri za wilaya na mameya wa miji, manispaa na majiji wasimamie shughuli zote za maendeleo katika maeneo yao. Kazi za usalama zisimamiwe na ma-OCD na ma-RPC!
 
Siku za nyuma wanaharakati walishawahi kuhoji umihimu wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni nini? kwamba ma-DAS na RAS wanatosha. Nafikiri JK anatafakari hilo kwa undani, vyeo hivi ni sawa na matumizi ya vyoo, havina tija kwa wananchi zaidi ya kuwapa Ulaji, Katiba Mpya iviondoe vyeo hivyo viwe ni ajira au kupigiwa kura na wawe ma-govenor chini ya serikali na siyo chama, pumbavu.
 
Back
Top Bottom