JK Kuongoza Mashambulizi: Kumg'oa Ndesa, Kumgalagaza Mbowe na kugomboa Karatu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Kuongoza Mashambulizi: Kumg'oa Ndesa, Kumgalagaza Mbowe na kugomboa Karatu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 21, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Wanabodi

  Nilipata ka vakasheni kafupi, hivyo nikaamua kwenda kujipumzisha mikoa ya Moshi na Arusha
  juzi na jana.

  Baada ya mapumziko mafupi ya juzi yalitosha na jana nikaitumia kusafisha macho kwenye harakati za kisiasa mjini Moshi na Arusha.

  Habari kubwa niliyokumbana nayo ni kuwa CCM ina hali mbaya sana Jimbo la Moshi Mjini ambako Mzee Philemon Ndesamburo wa Chadema, bado anakubalika sana. Pia CCM iko kwenye hati hati za kulipoteza jimbo la Hai, ambapo Freeman Mbowe anakubalika sana, na kwa upande wa Arusha, Jimbo la Karatu ndilo jimbo pekee linayoinyima usingizi CCM ili kuligomboa jimbo hilo ambalo ndilo roho ya Dr.Slaa.

  Ili kujizatiti kwa mpambano huo, inasemekana CCM imemuomba Mwenyekiti wake na mgombea wa urais, kupiga kambi mikoa hiyo, kufanya kampeni ya nguvu ili kupata ushindi.
  Japo JK alishafanya kampeni yake huko, sasa atarejea tena wiki ijayo kwa kampeni ya funga kazi, kabla ya kurejea jijini Dar kukamilisha kampeni hizi siku ya Jumamosi 30 Octoba katika viwanja vya Jangwani.

  Kwa maoni yangu, JK atajiaibisha bure tuu kutaka kuking'oa kisiki cha mpingo kwa kutumia panga butu!. Kisiki cha mpingo hakikatika hata kwa shoka, bali huchimbwa kukizunguka mpaka kuufikia mzizi mkuu wa katikati ambao hukatwa kwa shoka kali, ndipo hung'ooka!.

  Mgombea wa CCM kwa Moshi mjini, Salakana, anmaendelea kwa kampeni ya nyumba kwa nyumba nyakati za asubuhi na jioni kwenye mikutano ya hadhara. Jana alikuwa mitaa ya Bondeni na kila alipopita alishangiliwa na kuahidiwa kura zote ni kwake, japo sina uhakika kama ahadi hizi ni kiini macho kwa kumuonea aibu akiwa mtaani kwao, au ndio kitakachofanyika Octoba 31.

  Kwa Upande wa Arusha, jana nimehudhuria kampeni za Mgombea wa Chadema, Godbless Lema pale Levolosi Desemba na kumalizia kampeni za Mgombea wa CCM, Dr. Batilda Burian Pale Kaloleni, kwa mikutano ya jana, ni CCM ilifunika, sijui kwa ile iliyotangulia maana sikuwepo!.

  Kwa nini CCM haina wasiwasi na jimbo la Vunjo?. Nadhani ni kwasababu Chadema, NCCR na TLP wanaparurana katika vita vya panzi, hivyo CCM imepozi pembeni kama Kunguru kusubiri kulitaka kiulani!.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  safi sana,acha akapoteze muda huko maana ataambulia patupu
   
 3. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  arusha mjini mkuu. Batilda anahemea mashine.
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ccm iko hoi mikoa yote tanzania bara na pemba. Asidanganyike kuwa moshi au arusha pekee. Taaaaabani kabisa ccm.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Endeleeni kujidanganya.............Kama unajua upepo wa kisiasa unavumaje ungelijua hakuna Mtanzania mwenye akili timamu anamsikiliza tena JK baada ya kushindwa vita dhidi ya ufisadi.........Yaani sasa hivi kukipigia debe CCM jamii yakuona kama mwenda wazimu vile au zimefyatuka na jamii itadadisi hivi wanufaikaje na huu ufisadi...........Dr. Batilda hapa Arusha hawezi kufua dafu kwa Lema...hilo lielewe na hao wachache wanaokwenda kwa Batilda wanafuata burudani tu lakini hawatampigia kura hilo liweke machoni kwako.........
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kikwete anadhaurika sana si na wanaCCM peke yako bali na watanzania wote wenye nia njema! Si turufu tena huyo ndo maana anaweka nguvu kubwa kutegemea familia yake zaidi
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lakini si kila uchaguzi CCM husema hivyo hivyo tu? -- "nguvu zote kukomboa majimbo ambayo bado yanakaliwa na upinzani -- lakini hujikuta wanashindwa." Jee safari hii wataweza pamoja na kuwepo kwa tsunami ya Dr Slaa?
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Pasco,

  Mkuu ni kweli Mama Dr Batilda anakuja juu sana kipindi hiki cha lala salama ingawa wapo watu wengi hawataki kukubaliana na hali ya mambo.Zipo habari makundi ndani ya CCM hasa Mhe Felex Mrema ameamua kurudi kundini baada ya kuahidiwa nafasi serekali ijayo.Mkuu mkutano wa Mama ulikuwa maeneo ya Stadium kama ulikuwepo nadhani uliona magari mawili [Malori]makubwa ya matangazo moja linamilikiwa na Tripple A na lingine CCM makao makuu.Vikundi vya sanaa na maigizo vilikuwa na watu wasiopunguwa arobaini pia wahudhuriaji wengi si wapiga kura wa kata ya Kaloleni nasema hivyo kwasababu nawajua wengi wametoka kata ya Kati ambayo ni ngome kuu ya CCM [NB kata ya Kati inawapiga kura 3,000 na kelele nyingi sana].

  Mama Batilda anatumia mbinu alizokuwa akitumia Lema kusomba watu wake kutoka kata mbali mbali kila anapofanya mkutano naona inaweza kumsaidia bila kufanya hivyo mkutano wake wa jana usingekuwa na nyomi ya kutosha.Lema alikuwa akitumia mbinu hii tangu mwanzo wa kampeni kila mkutano wake lazima Noah nne zilizosheheni watu zimemo kwenye msafara wake.
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hata apige kambi yeye na familia yake huko,hawezi kuivunja ngome imara ya CHADEMA!
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ngongo! sometimes unazungumza as if huko Arusha unaishi peke yako!
   
 11. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu za huko AR! hapo kwenye red kaka vipi? Kati ya chama kile kinachobeba watu na malori na huyu anayetumia Noah ni nani zaidi. RIP wale wa kule Zanzibar
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Nyambala,

  Najua kilichokukera ni hizo Noah kama utabisha muulize Pasco jana alipita Levolosi tukate mzizi wa fitina.Mkuu Nyambala hizo ni mbinu za kampeni ambazo zimemsaidia sana Lema hazikatazwi labda kama unamtazamo mwingine.Hivi umewahi kuwaona wale wacheza kamari karata tatu mbinu wanazotumia ni hizi hizi.
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Soma #12.
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Eeka Mangi,

  Mkuu CCM ni mabingwa wa kusomba watu hilo halina ubishi,tumeshawahi kulijadili hapa mara kibao lakini inashangaza kama si kustua mbinu hii ikitumiwa na wapinzani tunakuwa wagumu kukubali.Labda utakuwa hujui mazingira ya mji wa Arusha kuna kata kubwa kama Terati nadhani ukubwa wake ni sawa na Pemba inawapiga kura wachache sana sina uhakika sana hawazidi 2000 ukienda huko bila kampani ya watu wako unaweza kukosa watu wa kuwahutubia watu wa huko wako mbali mbali sana ni eneo ambalo halina msongamano wa watu kama Ungalimited.
   
 15. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Wiki iliyopita nilihudhuria baadhi ya mikutano ya hadhara kwenye Majimbo ya Hai, Moshi Vijijini na Vunjo. Nilihudhuria mikutano ya ccm na ya chadema. Kwa mfano Hai nilikwenda Kata ya Masama, Modio kwa Kimbita wa ccm, na baadaye Kware kwa Mbowe wa chadema, Moshi V, nilikwenda Kijiji cha Uri kata ya Kibosho Kati kwa Dr Chami wa ccm, na Kimochi kata ya Vunjo mashariki kwa Komu wa chadema. Katika jimbo la Vunjo, nilihudhuriri mkutano wa Mrema wa chadema Mamba Kotela, na wa Meela wa CCM Kilema pofo.
  My take:
  Watu wengi wanaohudhuria mikutano ya ccm ama wamekata tamaa kimaisha, au wanamahangaiko ya maisha hivyo kupata mahali pa kutulizia mawazo kwani kuna mbwembwe za vikundi vya waahamisishaji tena vya kukodiwa na hasa kama ni wanawake basi wana frustrations kwenye ndoa zao. Kwa wanaume hali kadhalika wao wanachukulia kama ajira hivyo kutangatanga kutoka mkutano huu kwenda mwingine.
  Kwa upande wa chadema, wengi wanaohudhuria ni watu wanaopenda kusikia, kupima na hata kuamua. Ni mara chache sana kumkuta mtu anahudhuria mikutano mingi kwani tayari anakuwa ameshapata ujumbe mzito unaotosha kufanya maamuzi tarehe 31. Kila mkutano na watu wapya hivyo kufanya sera ziwafikiewatu wengi zaidi na si wale wale kwa kila mkutano.
   
 16. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Noah inasheheni watu wangapi?
   
 17. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hata kama watafanikisha mradi wao wa kuiba kura na kuapishana upesi upesi kama alivyofanya Kibaki, wajue tu huyu bwana ataendelea kudharauliwa na Wananchi walio wengi na utawala wake utakuwa taabu tupu!!
   
 18. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mikoa kama kilimanjaro watu wameamka.Nadhani wangejikita hapa bagamoyo na morogoro.
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,662
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu mgonjwa bado anajidanganya kuwa yeye ni mtaji wa CCM? Poleni mnaondelea kusikiliza porojo na mipasho ya mgonjwa wa taifa.
   
 20. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Noah moja inachukua watu kumi comfortable mara nne arobaini,Ipo Toyota Landcruiser hardtop na saloon car tano ile ya mtoto wa Photo me T 537 ADJ haikosekani hata mara moja jana kidogo ilileta tafrani kwenye mkutano wa batilda.
   
Loading...