Jk kumuita daimond ikulu kumjulisha shoo ya us imekaaje??????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk kumuita daimond ikulu kumjulisha shoo ya us imekaaje???????

Discussion in 'Entertainment' started by eumb, Aug 24, 2012.

 1. eumb

  eumb Senior Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  JK Dimond.jpg Stori: Sifael Paula; www.globalpublisherstz.info

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz' na kumpa jukumu maalum, Ijumaa linairusha hewani.
  Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti' alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.
  "Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani.
  "Kwa mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari," alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hii thread imefikaje huku?
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  mmh! jamani anampeleka kwa gharama za chama ama za serikali? na kwaajili ya nini hasa?
   
 4. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  kigezo kilichotumika kupewa show diamondi.?
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Makubwa, sasa marekani anaenda kumtumbuiza nani? Rais, watanzania waishio kule au wamarekani?
   
 6. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mambo ya muhimu kwa Watanzania tunaambiwa fedha hakuna, hizi za safari isiyo na tija kwetu zimetoka wapi?
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi mkuu alishindwa waambia ata akina Ruge au Kusaga au hata akina Nchimbi mpaka alonge nae mwenyewe straight
   
 8. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kumbe sahvi kila mtu anaweza kuitwa tu ikulu na kwenda kama anavyokwenda matembezini mm nilidhani ni pahala 'sacred' au toka nche nkapa apageuze anuani ya biashara yake kila mtu anaweza kwenda cha kuzingatia ni ukiwa umefanya miadi yako na mkubwa.
   
 9. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Hah hah hah!
  Sasa anaenda kuutangaza utamaduni wa nchi gani. Au ni kuwaonyesha USA ni jinsi gani na cc TZ hatuko nyuma katika ku-copy mambo yao?
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kikwete kumbe meneja masoko wa Diamond!
  sijui mnawaita mapromota!
   
 11. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Taarifa zililopo ni kuwa anakwenda kutumbuiza 'Wanamagamba' waishio humo (Sijui kama wanafikia kumi)..
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,264
  Trophy Points: 280
  Yaani wote mnachangia thread hii bila hata ya kujiuliza source ya habari hizi wanasoma watu wenye sampuli gani ya Ubongo? Pamoja na udhaifu wote wa JK na nyinyi mnakubaliana na porojo hizi za kina Shigongo?
   
 13. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani nataka kuuliza kama hilo gazeti lililotumika kutoa taarifa linakubalika humu kwenye jukwaa la siasa kama chazo kinachoaminika cha habari?!!!
   
 14. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Acheni dogo ale shavu jamani.
   
 15. m

  malaka JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi JK hatungagi verse kweli?
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,268
  Likes Received: 19,412
  Trophy Points: 280
  kura zenu za mwaka 2005 na 2010 ndio zinafanya kazi izo mnafikiri zitaenda kimya kimya? Noo mtaona mengi na mmeshaona
   
 17. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waende sana Ikulu wakati CCM ingalipo madarakani, maana wakati waje wa kurejesha hadhi na heshima ya Ikulu kama ilivyokuwa kipindi cha mwalimu! Kipindi hicho ukiitwa ikulu unatetemeka! Sasa hivi mtu akiitwa ikulu anajua naenda kupewa mchongo tu na mambo yangu yananyooka!
   
 18. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Msiyaamini sana haya magazeti, ni ya udaku, mara nyingi habari huwa ni za kupika mwandishi ndo mhariri
   
 19. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waende sana Ikulu wakati CCM ingalipo madarakani, maana wakati waja wa kurejesha hadhi na heshima ya Ikulu kama ilivyokuwa kipindi cha mwalimu! Kipindi hicho ukiitwa ikulu unatetemeka! Sasa hivi mtu akiitwa ikulu anajua naenda kupewa mchongo tu na mambo yangu yananyooka!
   
 20. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  msanii mwenzake na ndio priority ya rais jk!mbona mpaka leo hajawaleta REAL MADRID?maana ilikua ilani ya ccm
   
Loading...