JK kukutana na Wazee wa Mkoa wa Dar J'nne kuwaeleza serikali yake haiendeshwi kwa kushinikizwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kukutana na Wazee wa Mkoa wa Dar J'nne kuwaeleza serikali yake haiendeshwi kwa kushinikizwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 22, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Baada ya Kikwete (kupitia Pinda) kutangaza hapo kesho kwamba hakuna waziri atakayejiuzulu kutokana na sakata linaloendelea, Mkuu huyo wa Kaya atakutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es Sakaam siku ya J'nne Ukumbi wa Diamond kuwashitaki Wabunge wachache wa CCM wasaliti walioshirikiana na wale wa upinzani kutaka kuiyumbisha serikali yake.
  Mada kuu itakuwa ni kwamba serikali yake haiendeshwi kwa kushinikizwa.

  Mwenyekiti wa Wazee ambaye anabeba tuhuma lukuki za ufisadi na ambaye hakuna chombo cha dola kinachodiriki kumgusa -- Iddi Simba ndiye atakayempokea rasmi rasmi JK ukumbini pale.

  Nataka kutapika!!!!!
   
 2. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Huyu Rais ana matatizo.
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nilijua tu
   
 4. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ina maana haendi tena kwenye mazishi ya B. Mutharika kesho?
   
 5. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  kwani nani kafa?
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Marksman,

  Sipendi kuamini Rais Kikwete anaweza kufanya mambo ya hovyo kiasi hicho.Tafadhali tumpatie Rais wetu heshima anayostahili na ikiwezekana tumsaidie amalize awamu yake salama mambo ya kumzushia kwamba atakutana na wazee wa Dar ni siasa za maji taka.


   
 7. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nenda wewe
   
 8. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hivi hakuna jinsi yoyote ya kumwadabisha huyu jamaa?
   
 9. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Hii ndio Point.
   
 10. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,467
  Likes Received: 3,732
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa kama atafanya hivyo nitaamini hamnazo
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  akifanya hivyo akieleza hivyo atakua ni rais mwehu katika sayari ya dunia!wazee si ndio mtaji wa ccm kwa sasa
   
 12. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mi nataka kujua kuwa hao Wazee wa Dar (Wana magamba wenzake) ndio washauri zake au wao ndio waliowaambia NEC wampitishe? Huyu Kikwete naona uzee unamjia vibaya hata kwenye manufaa ya Taifa yeye analeta ujinga na upumbavu wa maneno ya kejeli.:mad2:
   
 13. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ooh...oooh!!
  Kama kweli, huyu mtu hazimtoshi. Wanaoshinikiza kwani hawana sababu au wamekurupuka tu. Haya labda hao wazee ndio wawakilishi wetu.

  Vijana tuangalie namna ya kwenda. Hawa wazee wa ndio na ambao kwa kiasi kikubwa washapoteza tumaini hawatakiwi kutuamulia mambo yetu. Vijana ukiondoa matatizo mengine, tuna muda mrefu wa kuishi. Uozo unaondelea sasa ni mzigo kwetu siku za mbeleni na mengine tunayaona sasa.
  Tuseme yatosha.
  Hao wazee wanatutegemea sisi.
  Tuamue.
   
 14. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hahahah nchi inaendeshwesha kijinga hii khhhhhhhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 15. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama anaweza kufanya kitu kama hicho, na kama akifanya atakuwa wa kwanza ku-officiate mwanzo wa mwisho wa CCM.
   
 16. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mazishi ya President Bingu wa Mutharika ni kesho, na ilisemekana atakwenda
   
 17. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu kufanya hivyo (kuanza kupingana na wapunge wake, badala ya kuziba ufa kwa kutumia cement atakuwa anatomia nyundo hivyo kuzidi kubomoa..

  [​IMG]
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ngongo - heshima mbele. Huenda mtoa mada ana nia ya kumshawishi JK kutochukua hatua hiyo ya kijinga, yaani ya kukutana na wazee. Ni kama vile anajaribu kum-preempt asiende huko.

  Ni mtazamo tu.
   
 19. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Hakuna udhaifu mkubwa kwa kiongozi kama kuruhusu wapiga kelele kukuyumbisha, Kosa kubwa la JK ni kumteua PINDA ambaye hana misimamo ni weak sana yaani anaboa ningekuwa JK ningemfukuza na kumuomba astaaf hadi ubunge.
  Anaboa sana PINDA.
  Pinda ndio chanzo cha matatizo serikalini. Hivi hakuna wanajeshi bungeni wapewe hii nafasi!
   
 20. franktemu123

  franktemu123 JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 775
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 80
  Kama ni kweli Mkuu wa Kaya anakutana na Wazee wa Dar kuongelea ishu ya Mawaziri kutojiuzulu binafsi nitamuona mtu wa ajabu. Watanzania tuna uwezo wa kumuwajibisha yeye kama Mkuu wa Kaya 1. ni kupitia wabunge wetu kwa kuanzia ni kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu hivyo Rais atalazimika kuvunja baraza la mawaziri 2. Ni kwa wabunge huko mbeleni kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Mkuu wa Kaya 3. Ni kupitia chaguzi ndogo kutopigia kura wabunge/madiwani toka chama chake.... By ze way hii stori ina ukweli coz najua anaenda kuzika MALAWI au ndo atamtuma Makamu a.k.a MZEE WA MIKASI "KIBABU" amelegea kama mlenda sijui hata mikasi anapigaje? labda kama anapigwa yeye?
   
Loading...