Jk kukutana na waandishi live | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk kukutana na waandishi live

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mundali, Oct 28, 2010.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Habari nilizozipata kupitia Clouds Fm radio ni kwamba mgombea wa ccm, rais Jakaya Mrisho Kikwete atafanya mkutano na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Iwapo itatolewa fursa kwa waandishi waalikwa kuuliza maswali, naomba niwakilishwe pamoja na watanzania wote wenye mtazamo kama wa kwangu maswali yafuatayo: -
  1. Akiwa kampeni kwenye mikoa mbalimbali, mgombea wa kiti cha urais kupitia ccm amekuwa akitoa ahadi kemkem za miradi ya maendeleo yenye kutia matumaini kwa wananchi. Je, akiwa pamoja na timu yake ya kampeni amefanya tathmini ya gharama ya jumla kwa miradi yote aliyoahidi kuitekeleza ndani ya miaka mitano?
  2. Ni kiasi gani kwa pesa ya tanzania zinahitajika kukamilisha miradi hiyo yote aliyoahidi?
  3. Pesa za kugharamia miradi hiyo zitapatikana vipi?

  Mimi na baadhi ya watanzania wenzangu tumekuwa tukijiuliza maswali hayo bila kupata majibu stahili. Tunaomba ndugu zetu waandishi wa habari mtufikishie ujumbe wetu. Shukrani nyingi kwenu.
   
 2. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  :doh:kwani ni waandishi wa habari pekee wanaopiga kura? Mwenye akili timamu anaona kabisa kuwa huyu ajiitaye raisi anaogopa kufungulia maswali yatoke kila pahala maana anajua wananchi walivyo na hasira safari hii watamvua nguo. Eti maswali yatumwe kwa barua pepe, sms! Ili wakamtafutie majibu aje kusoma? Ama akariri usiku kucha?
  Ilitakiwa wananchi waachwe wamgawane vipande vipande!:A S angry:
   
Loading...