JK kuifumua CCM - AITISHA GHAFLA VIKAO VYA CC NA NEC DODOMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kuifumua CCM - AITISHA GHAFLA VIKAO VYA CC NA NEC DODOMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 9, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  • AITISHA GHAFLA VIKAO VYA CC NA NEC DODOMA


  na Danson Kaijage, Dodoma

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]​[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  BAADA ya kufanya mabadiliko kwenye Baraza lake la Mawaziri, Rais Jakaya Kikwete sasa anatarajia kuifumua sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumatano imebaini.
  Vyanzo vya habari kutoka ndani ya CCM, vilisema kuwa Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, ameamua kuitisha vikao vya chama ghafla pamoja na mambo mengine, kufanya mabadiliko kwenye sekretarieti yake.


  Duru za kisiasa kutoka ndani ya chama hicho tawala, zilisema kuwa mabadiliko hayo yanatokana na mmoja kati ya wajumbe wa sekretarieti, Januari Makamba, kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu.

  “Kama utakumbuka mara ya mwisho Rais Kikwete aliamua kuwaondoa mawaziri wote kwenye sekretarieti ya chama ili wajumbe hao waweze kufanya kazi muda wote. Alimwondoa Waziri Bernard Membe, Nape akalazimika kuachia u-DC. Kwa vile Makamba amekuwa waziri ni wazi kwamba ataachia nafasi hiyo na Rais ataijaza kwa kumteua mjumbe mwingine,” kilisema chanzo chetu cha habari.


  Wajumbe wengine wa sekretarieti hiyo ni pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Mhasibu Mkuu, Mwigulu Nchemba, Martin Shigela, Amina Makilage, Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenister Mhagama, John Chiligati, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Asha Juma na Katibu Mkuu, Willson Mkama.


  Katika kujaza nafasi hiyo, Rais Kikwete anaweza kuwagusa wajumbe wengine kama ataona kuna ulazima wa kufanya hivyo.


  Ukiachia mabadiliko hayo, vikao hivyo vya CCM ambavyo vinaanza Mei 11 hadi 14, vinajadili mambo mbalimbali, ikiwemo hali ya kisiasa ndani ya chama hicho hasa kipindi hiki ambapo kinakabiliwa na kukimbiwa na wimbi la wanachama wake.


  “Kuna mambo mazito ya kujadili. Kasi ya CHADEMA na ushindi wake Arumeru imeibua hofu, wimbi la wanahama wa CCM kuhamia CHADEMA, mpasuko ndani ya chama, suala la uchaguzi wa chama na mjadala wa Katiba ni baadhi ya mambo yatakayoibua mjadala mzito,” alisema mtoa habari wetu.


  Mtoa habari wetu alisema kuwa kikao hicho pia kinaweza kuwaweka kiti moto wabunge wa CCM walioungana na wenzao wa upinzani kutia saini za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


  Kwa mujibu wa ratiba ya vikao hivyo kuanzia jana hadi Mei 11 kutakuwa na vikao vya maandalizi, Kamati ya Maadili kukutana Mei 12 asubuhi na Kamati Kuu (CC) chini ya Rais Kikwete itakutana siku hiyohiyo jioni.


  Mei 12 kutakuwa na semina maalumu kwa wajumbe wote wa CC na NEC na Mei 14 itakuwa siku ya NEC.


  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Nape alisema kuwa vikao hivyo ni maalumu kwa ajili ya wajumbe kujadili mjadala wa Katiba mpya.


  Alipoulizwa kama kuna hatua zozote ambazo zitachukuliwa na kwa baadhi ya wabunge waliosaini fomu ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Nape alisema hoja hiyo haipo na haiwezi kuwepo kwani wabunge hao walitoa haki yao Kikatiba kuwawakilisha wananchi wao.


  “Kwanza ikumbukwe kuwa Rais akiwa Tanga aliwapongeza wabunge kwa kuonyesha msimamo wao leo itakuwaje Rais tena awageuke na kuanza kuwawajibisha? Hilo halipo kabisa!” alisema.


  Katika hatua nyingine, Nape alisema mawaziri wote waliotuhumiwa wawajibishwe kwa uzito wa makosa yao kama watabainika kuhusika.


  “Hakuna mtu aliye juu ya sheria, kama mawaziri wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu wako ndani ya Baraza la Mawaziri au wale walioachwa ni lazima kila mmoja achukuliwe hatua kadiri ya kosa lake, kama leo hii Rais mstaafu Benjamin Mkapa kafikishwa mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi itakuwa Baraza la Mawaziri?” alihoji Nape

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. R

  RMA JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania wanachotaka kwa sasa ni kuona HATUA KALI zinachukuliwa dhidi ya mafisadi! Tofauti na hapo hata kama yakifanywa mabadiliko gani ccm haina chake tena 2015.
   
 3. L

  Lion's Claws Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walisema ni upepo tu muda kidogo utapita. Lazima mafisadi wang'oke hadi hao wanaowakumbatia.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hakuna jipya chini ya CCM. Kanzu mpya shehe wa zamani!
   
 5. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Anaifumua kwani aliwahi kuisuka lini?

  JK bwana ananiacha hoi sana. mtu unaweza kufumua kitu ambacho hakijasukwa? yeye aseme anaiua moja kwa moja manake atakapoawatoa mavuvu zela Nape lazima waje waombe kombat huku pipoz power street.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Wanatapatapa na matamko ya CDM..ya kutaka kujitenga iwapo hawatapata mgombea wa urais kama wale vijana wa pwani walivyosema kuwa rais hatatoka kaskazini!wanataka kujitenga kuunda nchi ya Meru!kazi ipo hapo ngoja tuone
   
 7. g

  gotolove Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kurasa fulani wameandika matatizo ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Inafaa Kamati Kuu imshauri rais amwondoe yule Profesa wa UDOM anayekiharibu chuo. Mimi naona wanafunzi wanaomaliza vyuo ni watu hatari sana kuliko wazee wa vijijini. Tukitenda mema vyuoni CCM itakuwa inajihakikishia uwingi wa wapiga kura katika chaguzi zijazo. Kinyume cha hapo ni madhara makubwa. CCM shinikiza kuondolewa kwa profesa wa Kiswahili anayetajwatajwa pale UDOM HARAKA. TUSIWE SIKIO LA KUFA HALISIKII........
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,082
  Trophy Points: 280
  Ahangaikee weee!! mwisho tunataka mfumuko wa bei ushuke, reli zetu zifufuliwe, vipato vya watumishi yaboreshwe.......hali

  za maisha ya watanzania iwe bora.

  Siyo blah! blah!
   
 9. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ashaona CCM inamfia anatafuta pa kutupia lawama hana jipya.

  Mbona sijasikia kama wata review AHADI ZAKE ZA UCHAGUZI kwani katimiza ipi mpaka sasa
   
 10. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  Lusinde kuwa naibu katibu mkuu wa chama
   
 11. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  NAPE KAA CHONJO, unaweza ukajikuta unahamia CDM au Ukaanza tena mchakato wa ki-CCJ lakini safari hii kwa uwazi
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  lishapeleka vikao butiama, tukaambiwa wanavua gamba, tukasubiri uamuzi mzito, tukaambiwa mafisadi siku zao zinahesabika nk

  I DONT EXPECT ANYTHING....

  NA KWA HALI INAVYOENDA, NI HADI KIONGOZI MMOJA MKUBWA AFE AU AWE KICHAA NDIO MAMBO YATABADILIKA
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  seen,well done
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mabadiliko ya kimfumo ndio yanayohitajika
   
 16. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,775
  Likes Received: 8,040
  Trophy Points: 280
  JK hana ubavu wa kuifumua CCM. Juzi tu hapa alitaka kumuondoa Mkulo na wezi wenzie ilibidi akaombe ridhaa CC ya chama, leo hii mwombaji akawe mpaji, mmh! Puruzai za barazani hizi, hakuna jipya.

  Na kama mmesahau, kumbukeni kile kikao cha kuvuana magamba last year. Baada ya Lowassa kumwaga data, nani aliyenywea zaidi ya JK?
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kumbe re branding ya kasesela kujivua gamba haina tija,hali inakuawa worse!muda wa ccm umeisha tunaomba muelewe hivyo
   
 18. Jack G

  Jack G Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari JF,
  Kama anayohisi mwandishi ndio maudhui ya vikao; then makosa yamefanyika tangu siku nyingi na yana mzizi mrefu. Hit and run techniques may not work at the moment, naamini watanzania wa leo tunataka vitendo zaidi ya maneno. For decades , CCM leaders took this country for granted, it's time to learn a lesson.
   
 19. H

  Hingi Jr Senior Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CDM watasubili sana kwani CCM imejipanga na ina mizizi minene ambayo haing'ooki kwa mbwembwe za CDM ambazo hazina mafanikio kwa Taifa.CCM OYEEE! nasema CDM wanapenda na wanatamani CCM isambaratike lakini hiyo ni ndoto ya alinacha.CCM ina wenyewe na wenyewe ni wanachama na watanzania wanaojua na wanaoitakia mema Tanzania.Kidumu Chama Tawala Cha CCM.
   
 20. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hii ya January Makamba Kutoka kwenye vikao vya chama naona ni bonge ya pigo kwa upande mmoja,kwa upande fulani bonge ya strategy!!
   
Loading...