JK kufanya mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kufanya mabadiliko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 22, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 22.11.2008 0010 EAT

  • JK kufanya mabadiliko

  *Vigogo wengi wahaha,wakosa usingizi
  *Ni walioshindwa kwenda na kasi mpya

  Na Mwandishi Wetu
  Majira

  RAIS Jakaya Kikwete huenda akafanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa wilaya mbalimbali nchini hivi karibuni ili kuhakikisha anapata wachapakazi makini hasa katika kipindi hiki utawala wake ukielekea kutimiza miaka mitatu, vyanzo vya kuaminika Serikalini vimelithibitishia Majira.

  Kwa mujibu wa habari za ndani Serikalini, mabadiliko hayo makubwa, huenda yakatangazwa mwezi ujao, iwapo Rais ataamua, na yataibua mtikisiko katika utawala wa wilaya nyingi ambako wengi kati ya wakuu hao wameonekana kujisahahu kiutendaji na kufanyakazi aidha kwa mazoea au wakiacha kulinda maslahi ya wananchi badala yake wakikumbatia wawekezaji,matajiri au wengine kutokuwa na mbinu mpya katika utawala.

  Chanzo hicho kilicho katika safu andamizi za Serikali, kilisisitiza kuwa timu mpya ya wakuu hao wa wilaya tayari imeshapangwa na kitu kilichobaki kwa sasa ni hatua ndogo ndogo za mwisho.

  "Uamuzi huo wa mabadiliko utatangazwa hivi karibuni inawezekana kabisa mwezi ujao au mapema Januari na hii imetokana na baadhi ya wakuu hao kutowajibika ipasavyo hivyo kukwamisha juhudi za Serikali iliyoko madarakani," kilisema chanzo hicho.

  Kiliendelea kusema kuwa sura kadhaa mpya za wakuu hao zinatarajia kujitokeza na uteuzi huo ambao unafanywa na Rais Jakaya Kikwete akipata ushauri wa karibu kutoka kwa Waziri Mkuu wake, Bw. Mizengo Pinda, unaelezwa utakuwa makini zaidi ili kuhakikisha hawachukuliwi watu ambao utendaji wao utakuwa na upungufu tena hasa wakati huu Serikali inapoelekea kukamilisha malengo ya sera zake katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais Kikwete kabla hajaomba tena ridhaa ya kuongoza awamu ya pili mwaka 2010.

  Aidha chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa fungu la fedha ambalo lilikuwa limekwamisha uteuzi huo mpya tayari limepatikana ambalo litawawezesha watendaji wapya na wale wa zamani watakaobadilishwa kusafiri kutoka mahali walipo na kwenda katika vituo vyao vipya vya kazi.

  "Unajua sasa hivi mambo yamebadilika, hawataki tena kuangalia ukada wa chama au mambo ya siasa. Kinachotakiwa ni uchapakazi hivyo kuna hatari ya wengi kupoteza nafasi walizonazo kwani lengo kubwa lililokuwepo ni kuwajibika kwa wananchi lakini wamekuwa hawasaidii chochote kwenye nafasi walizopewa.

  “Wanatakiwa wakuu wa wilaya ambao watakaa kwenye nafasi zao na kuwajibika kama Serikali ya Awamu ya Nne ilivyokusudia. Ubabaishaji sasa hivi hautakiwi," kilisisitiza chanzo chetu.

  Wiki iliyopita Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda alifanya ziara mkoani Dodoma ambako aliwaambia wakuu wa mikoa na wilaya kuwa watapimwa kwa vigezo vipya ambavyo vitawekwa ili kubaini utendaji wao na watakaoshindwa wataondolewa.

  Bw. Pinda alisema kuwa viongozi wote wa ngazi hiyo wanatakiwa kuwajibika hasa kwa kuwafikia wananchi vijijini ambako watahamasisha kilimo chenye tija ili kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo.

  Rais Jakaya Kikwete pia amekuwa akikutana na vituko vya baadhi ya wakuu wa wilaya kuonekana wanafanyakazi kwa mazoea tu katika ziara zake nyingi za mikoani hali iliyomfanya katika baadhi ya maeneo alazimike kuwasimajisha watendaji kujibu maswali hadharani.

  Hata katika ziara za Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, matukio ya wakuu hao wengi kuonekana wanafanyakazi kwa kukurupuaka yalionekana huku malalamiko ya wananchi katika vyombo vya habari wakati fulani yakiwahusisha wakuu hao katika tuhuma kama vile kukumbatia wawekezaji wanaonyanyasa wananchi, kushindwa kwao kuwasikiliza wananchi na kutatua shida zao na wengi pia kukosa mbinu madhubuti za kiutawala.

  Wakuu wote wa wilaya 137 zilizopo nchini waliwahi kuitwa kwenye semina maalum iliyofanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto, Arusha, ambako 'walifundwa' na Rais Jakaya Kikwete mwenyewe na viongozi wengine waandamizi Serikalini ili wajue wajibu wao katika kuwatumikia wananchi.

  Vyanzo vyetu vimepasha zaidi kuwa mkutano huo uliohudhuriwa na wakuu hao kwa furaha na matumaini, ndio ambao sasa ni sehemu ya kitanzi chao, kwani utekelezaji wa yaliyokubaliwa katika mkutano huo, ni fimbo mojawapo itakayotumika 'kuwachapa' wale walioshindwa kutimiza wajibu wao.
   
 2. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kawaida yake! itafika sehemu atajibadilisha hata yeye! Na sijui atamweka nani sehemu yake!
   
 3. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Tatizo hayupo serious..
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ameshafanya hivyo mara ngapi na ikatokea nini??????
   
 5. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Tatizo na jamaa wengine wamejenga chuki isiyokuwa na maana kwani marais wengine waliopita walifanya mara ngapi.
   
 6. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  chuki nyingi dhiidi ya JK inatokana na dhamira yake ya kuondoa katika uongozi mafisadi.sasa waliokuwa wakipata mlo huko ndo wanajenga chuki isiyokuwa na mfano dhiidi ya rais.
   
 7. k

  kela72 Senior Member

  #7
  Nov 22, 2008
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamna chuki, tatizo mie naona yeye huwa mabadiliko anapotaka kuyafanya inaonekana kama ni ushujaa na wapiga debe wake waona baada ya hapo hali itakuwa shwari kabisa, lakin mara zote imekuwa bora ya jana.
  Tuwe wazi tu jamani kuwa Mkuu "alipakimbilia Ikulu na vijipesa alitumia" huku akijuwa wazi kuwa uwezo hana..mbona liko wazi hilo!
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu kwa hiyo wewe ni mmoja wa wale wanaofikiria kwamba JK ooh anaonewa wivu, nyota yake inang'aa na kuna watu wanataka kuizima ooh! anawindwa asigombee 2010!!!!!!!!!!!!

  Hao mafisadi ni washkaji zake yeye na ndiyoo sababu moja wpo ya yeye kuchukiwa maana nchi haiendi kwa kuwaogopa hao zimebaki porojo tu.

  Wewe kama unafikiri JK is serious hebu angalia watu waliomzunguka tuanze na his chief of staff!, Njoo mkuu wa itifaki, his press secretary............ This guy is a joke!!!!!!!!!!!!
   
 9. PoliteMsemakweli

  PoliteMsemakweli Member

  #9
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  JK hata akifanya mabadiliko vipi, kuna donda ndugu kwenye chama Tawala na viongozi wake. Jamani hamuoni kuwa jamii sasa imechoka? Mafisadi kuchota fedha kama zao, walimu wanagoma wadai haki...mishahara midogo, posho ndio hivyo na hazilipwi kwa wakati...wakubwa wapeta...Tunataka mabadiliko ya kweli ya kujali nchi yetu kwanza kama wanavyofa wamerikani...Tanzania nchi nzuri lakini bado viongozi na wananchi kwa ujumla wetu bado hatujaamka na kuipenda kwa dhati nichi yetu...
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  You gotta be kidding me, or yourself.
   
 11. M

  Mama JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  aah easy, Lowassa.
   
 12. C

  Chief JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2008
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mtu anayemchukia JK kutokana na dhamira yake tu, na wala si utendaji (or lack of it), hafikirii vizuri.
   
 13. Arsenal

  Arsenal Senior Member

  #13
  Nov 22, 2008
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Anaondoa mtandao wa Lowassa...
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi mapolisi na majeshi wao wanalipwa mishahala mizuri ? ukilinganisha na wabunge na uchotaji wa mabilioni yalioibiwa chini ya awamu ya Mkapa ? Sijui sehemu wanazoishi na familia zao kama zina kiwango cha kuwa ni polisi au wajeshi wa Tz nchi iliyobarikiwa utajiri.
  Hivi na wao wana weza kugoma ? Siku wakiona maslahi wanayopewa ni sawa na kupunjwa ? Mbali ya mabadiliko yanayowakumba maana na wao mara utasikia wanabadilishwa .
   
 15. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Atambadilisha nani amweke nani na kwa faida ya nani?
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280

  Lahaula! Yaani wewe huoni kushindwa kwa JK kuiongoza nchi katika mambo mbali mbali, huoni ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni zake za 2005 ambazo hadi hii leo hajatimiza hata moja ya ahadi hizo, na mabilioni ya Kikwete vyote kutofanikiwa kukumbatia kwake mafisadi. Bali unaona chuki dhidi ya Kikwete!!! Chuki hizo zimesababishwa na nini ikiwa miaka mitatu tu iliyopita alipata 80% ya kura za Watanzania. Ni fisadi gani Kikwete aliyemuondoa tangu aingie madarakani!?
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwenye highlight; nasita kukubalina kwa sababu ingekuwa ghivyo, sidhani kama Tanzania ingekuwa kama hivi ilivyo leo. Sisemi kuwa JK na serikali yake wamefanya vizuri, lakini kusema kuwa hajatekeleza ahadi hata moja, ni kumuonea
   
 18. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mh! mama! Hapo umenipa raha!
   
 19. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu jiulize,
  Kwa nini JK achukiwe why? kwa nini? Kuna watu wana ajira zinazolingana na uwezo/elimu yao na wengine wanafanya kazi kwa ufanisi sana, sio wezi na si wafuasi wa mtandao wa mafisadi na wanamchukia JK why? kwa nini?
  Mkuu Said jiulize na tuambie hapa!!
   
 20. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  As long as Mlishamuudhi ES kwa kumfungi mjue kuwa hamtopata breaking news tena

  tutabaki ni hizi speculations zisizo na kichwa wala miguu
   
Loading...