JK kufanya mabadiliko madogo baraza la mawaziri??

Tarishi

Senior Member
May 9, 2008
103
133
Kuna khabari kwamba JK anatarajiwa kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza lake la mawaziri, na wanaotajwa tajwa sana huko kwenye mitaa ni waziri kijana ambaye inaonekana kashindwa kazi hasa baada ya kuvurunda kwenye mstakabali mzima wa vitambulisho vya uraia, na pia waziri wa utalii ambaye inasemekana haeleweki wala haelewi, maji yamemzidi. Wazee wa baraza hili naomba data
 
hizo bado ni tetesi tena tetesi kubwa...hili sio baraza la kubadilisha tu ni la kuvunjilia mbali na yeye mwenyewe kujiuzulu apishe watu waongoze nchi kwa ufasaha kuliko huko tunakokwenda
 
Kuna khabari kwamba JK anatarajiwa kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza lake la mawaziri, na wanaotajwa tajwa sana huko kwenye mitaa ni waziri kijana ambaye inaonekana kashindwa kazi hasa baada ya kuvurunda kwenye mstakabali mzima wa vitambulisho vya uraia, na pia waziri wa utalii ambaye inasemekana haeleweki wala haelewi, maji yamemzidi. Wazee wa baraza hili naomba data

Kama tetesi zako ni za kweli, basi Rutabanzibwa (aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani) aingehamishwa hapo wizarani. Anyway, as long as ni tetesi ngoja zibaki kuwa tetesi.

Pia kwa JK kufanya mabadiliko sasa wakati akiwa anaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani lazima ajiulize mara 2 kabla ya kufanya hayo mabadiliko, unless awe anahamisha tu bila kuwatema.
 
Whatever he does will be too little too late.

Nakubaliana na wewe Mkuu na bora tu atamke kwamba kwa maslahi ya nchi hatagombea tena 2010 ili tupate kiongozi mpya.
 
hata kama angefanya mabadiliko makubwaa who cares!? He is just a big loser.
 
hata kama angefanya mabadiliko makubwaa who cares!? He is just a big loser.

jipe moyo utashinda....viroho vinauma saana lkn itabidi msubiri hadi 2100 kwa sasa bado tupotupo sana.
 
JK alikosea sana kununua uongozi, na utamgharimu ktk maisha yake yote na kizazi chake chenye tamaa ya madaraka, hata akibadilisha baraza zima bado halitamsaidia chakufanya hapo ni kuitisha uchaguzi mapema kama alivyofanya rais wa yanga MH MADEGA
 
  1. Kama ni kweli yapo Mabadiliko ni kwa sababu zipi?
  2. Kama leo ndio JK anajua kuwa mawaziri wake hawajui kazi, kwa zaidi ya mwaka tokea awapangue walikuwa wanaripoti nini kwake.
  3. Wanapokutana kwenye baraza la mawaziri, hapakuwa na 'milestones' ambazo alikuwa amewawekea ili kujua utendaji wao kwa haraka?
  4. Kama ni kweli wameshindwa kazi baada ya kukaa ofisini kwa muda mrefu kiasi hiki, kwa nini wasiondoke pamoja na supervisor wao, yaani J.M. Kikwete?
  5. Gharama za mabadiliko analipa nani?
 
Ni tetesi
 
Ukiona Employer anabadilisha wafanyakazi wake kila wakati ujue fika kuwa si mtendaji mzuri (Managerial and Administrative skills ni low almost zero). Ni kwa mantiki hiyo huyu Rais wetu mtanashati amekuwa akibadili mawaziri, makatibu wakuu, etc na realised impact interms of output ni zero. Afikirie njia nyingine bora zaidi ya kongeza ufanisi badala ya kubadili na kuvunja kabisa kama ile February 2008. Of history!!!! Tumechoka.
 
Wakati mwingine ukiwa msomaji mzuri wa JF utazani Tz inaundwa na JF tu, lakini ukiwa ndani ya Tz na kusikia sifa anazopata JK na jinsi CCM inavyotesa miongoni mwa wapiga kura utajiuliza uamini wako wa JF.
 
Ni kweli sana alikosea sana kwa Mungu wake na JKN kwa kununua uongozi.....kama alikuwa groomed ili aje awe akiongozi......akatumia pesa haramu na mchezo michafu sasa ndio ina cost......

angekubali kuwa one term pres ingemjengea sifa sana.....hana jipya...zaidi kucheka cheka
 
Wakati mwingine ukiwa msomaji mzuri wa JF utazani Tz inaundwa na JF tu, lakini ukiwa ndani ya Tz na kusikia sifa anazopata JK na jinsi CCM inavyotesa miongoni mwa wapiga kura utajiuliza uamini wako wa JF.

Mapinduzi ya kweli huwa yanaanza na watu wachache waliojitoa wanaoona mbali.Kwa hiyo siyo jambo la kukatisha tamaa.Aluta kontinua!
 
Wadau naombeni kuuliza hivi huyu kijana OBAMA amewezaje??!!! mimi naona so far he is doing very well, na watu wake wamemkubali, maana kuongoza nchi kubwa na ya watu wa aina tofauti kama US siyo mchezo, sasa kama tunajuwa mbinu alizotumia OBAMA jamani kwanini tusimsaidie raisi wetu mbinu za kuiongoza nchi yetu na hatimaye na sisi tufikie maendeleo tunayoyataka.
Tukibaki kumlaumu hatutafika popote, afanye nini ili atuletee maisha bora kwa kila mtanzania?
1. Mimi naona kwanza angefufuwa viwanda vilivyokufa ili watanzania wapate ajira, na mashamba pia tupate chakula.
Tuendelee kumpa raisi wetu mbinu za kutukomboa watanzania.
Karibuni wadau, ni lazima tuipende nchi yetu na tuipeleke mahali pazuri.
 
hata kama angefanya mabadiliko makubwaa who cares!? He is just a big loser.

I do care!!!

Kwa maana hayo mabadiliko yangweza [kama yatakuwa chanya] kuboresha wizara zetu muhimu, kuongeza uwajibikaji [hasa kwa watendaji wa kawaida serikalini] na kubadilisha mfumo wetu wa "kama kawaida" usio na tija wala maendeleo... angeweza hili pia si vibaya kama angeangalia wizara ya afya, kilimo, mambo ya ndani, utawala bora, miundo mbinu, nishati, mambo ya east africa......... eh list haiishi!! Yaani angeangalia wizara zote na hadi makatibu wakuu na wakurugenzi wa idara muhimu

Nitajali pia kwani akimtoa kiazi aliyeboronga hapa na kumuhamishia kwingine, na mambo kama hayo... basi ndio ntajua tanzania inaelekea kaburini rasmi kwani hata kale ka-hope ka mbaaaali katakuwa kameondoka
 
Back
Top Bottom