JK Kimbembe na BoT. Ukaguzi wabaini kasoro

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
Rais Jakaya Kikwete, ameamuru vyombo vya dola vifanye uchunguzi kuhusu gharama halisi za ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Bongo.

Uamuzi huo umetokana na kuwapo kwa tuhuma kibao, kwamba hadi sasa mbovu zipatazo Sh bilioni 522 zimeshatumika kwa ujenzi wa majengo hayo jijini Dar es Salaam na Zanzibar, ambazo ni nyingi mno.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na viongozi kadhaa serikalini,zilisema tayari uchunguzi huo umeshaanza kwa wahusika washaanza kuwekwa kiti moto.

Baadhi ya vyombo vinavyounda chombo kinachochunguza liskendo hilo ni Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa, Ikulu, Polisi, Tume ya Maadili, wataalamu wa ukadiriaji majengo.

Source: Darhotwire
 
Stori kama hizi tumeshazisikia mara kibao na hakuna chochote kinachofanyika. Imefika wakati sasa hakuna hata maana ya kuziandika, ni mazingaombwe tu yaleyale.
 
Tume zimekuwa nyingi sana majibu hayaonekani. There is no need to talk the talk, what we need is to walk the walk.
 
Posted Date::11/29/2007 MWANANCHI
Ukaguzi wa Benki Kuu Tanzania wabaini kasoro
*Ripoti za awali zaonyesha utata

*Baadhi ya vigogo BoT watajwa kuhusika

*Wahusika kuchukuliwa hatua

*Meghji asema hajaipata, iko kwa CAG

Na Ramadhan Semtawa

JOTO la tuhuma za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limepanda, kutokana na taarifa za awali za ukaguzi kuonyesha kuwa kuna utata katika matumizi ya akaunti hiyo.

Ukaguzi huo ulifanywa na Kampuni ya Ernst & Young katika kipindi cha siku 60, kuanzia Septemba na kukabidhi ripoti yake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wiki iliyopita.

Hata hivyo, ikiwa ni wiki moja tangu CAG kukabidhiwa ripoti hiyo, taarifa za awali kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya serikali, zinaeleza kwamba baadhi ya vigogo ndani ya BoT wanatajwa kuhusika na malipo hayo yenye utata.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, vigogo hao wanahusishwa na ama kuidhinisha au kuhusika kwa namna moja au nyingine katika malipo hayo.

Vyanzo hivyo vilifafanua kwamba, maamuzi kuhusu ripoti hiyo yanatarajiwa kuchukuliwa kabla ya mwaka mpya.

"Watu watapata zawadi ya mwaka mpya, uchambuzi unaendelea kufanyika, lakini taarifa za awali zinaonyesha hivyo," kilisema chanzo cha habari kutoka serikalini.

Vyanzo hivyo vilifafanua kwamba, kuna baadhi ya stakabadhi za malipo ambazo zimeanza kuchambuliwa na zinaonyesha kuwa zimejaa utata.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, uchambuzi huo umezingatia kwa kina nyaraka za msingi za malipo ili kuona utata huo unasababishwa na nini.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, ukaguzi huo ambao uliingia kwa ndani na kuhoji watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Fedha, Zakia Meghji unaweza kubadili hali ya kisiasa nchini katika kipindi cha kuingia mwaka mpya wa 2007/08.

Meghji alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana kuhusu ripoti hiyo, alisema hadi sasa bado iko kwa CAG.

Alisema hafahamu lolote kuhusu kilichomo ndani ya ripoti hiyo kwani hajaiona na wala hawezi kuzungumza yaliyomo kwa sasa.

"Hadi sasa ripoti iko kwa CAG, sijaipata kama ni suala la maamuzi na nini kilichomo ni hadi ichambuliwe, nikiipata, nitaipitia, atapewa Rais na maamuzi yatatangazwa kwa umma," alisema Meghji.

Kauli hiyo ya Meghji ni ya pili ambapo ya kwanza ilitolewa na CAG ambaye wiki iliyopita alisema ofisi yake inafanyia kazi mambo yaliyomo katika ripoti hiyo, lakini hakufafanua.

Ernst & Young, awali ilipaswa kuikabidhi ripoti yake serikalini Novemba 10 ikiwa ni kumalizika kwa siku 60 za kufanya ukaguzi huo, lakini haikufanya hivyo na kuiomba serikali wiki tatu kwa ajili ya kuandaa ripoti ambayo ilifanyikia London, Uingereza.

Ripoti hiyo inasubiriwa kwa hamu na Watanzania kuona ukweli wa tuhuma za ufisadi ambazo zinadaiwa kufanywa katika EPA kwa ajili ya malipo ya vocha mbalimbali.

Nchi wafadhili pia zimesema zinasubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi huo kwani ni kipimo cha kuona mwelekeo wao wa kuongeza misaada kwa Tanzania katika bajeti ya mwaka 2008/09.

Kampuni hiyo ilipitia mahesabu katika kumbukumbu za vocha za malipo yaliyofanywa na BoT katika kipindi cha mwaka 2005/6, kubaini kama kuna ukweli juu ya madai ya ubadhirifu wa fedha katika benki hiyo katika kipindi hicho.

Agizo la kutafuta kampuni ya kukagua vocha hizo na mahesabu ya BoT, lilitolewa na Waziri Meghji Desemba 3, mwaka jana akimtaka CAG kuteua kampuni huru ya wakaguzi wazoefu wenye sifa za kimataifa kupitia baadhi ya kumbukumbu za matumizi ya fedha za benki za mwaka 2005/2006 ili kuondoa utata.
 
Nakumbuka kuna kiongozi mmoja alipokuwa Geita alisema wazi kuwa "kelele za wapinzani ni kama za mlango, hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi". Dalili hata hivyo zinaonesha kuwa ingawa amefumba macho, tunaona macho yanavyopepesa pepesa huku akijegeuza geuza.. sasa kama ni usingizi basi anajinamizi huko bora aamke au mtu amwagie maji!
 
Mimi nilikwisha sema tangu zamani credibility ya JK ina walakini mkubwa sana na ndio sababu nilianzisha hii topic: Hivi anafahamu dhamana aliyokabidhiwa ya kuliongoza taifa? Jukumu amepewa yeye na tunachoshuhudia ni kusuasua tu kama utingo wa dala dala la kwenda Manzese. Je, ni kwa nini hawawajibishi wale wenye kuonekana kabisa wamekosea katika majukumu yao? Karamagi aliyesaini mkataba wa Buzwagi tena kwenye hoteli aliyokuwa anakaa halafu anakuja kutusanifu ati alikuwa hajui, hili linawezekana vipi?

BWM ambaye anamiliki Kiwira kwa njia za udanganyifu. EL ambaye alituletea Richimonduli gate pamoja na madudu kem kem ambayo anapewa kila siku bila kusahau madudu haya yaliyo BOT. Tutamsubiri hadi lini huyu rais kufanya kazi yake aliyokuwa anaililia.
 
..aaha haaa aa aa habari ndiyo hiyo aah habari ndio hiyo aah haha hhaa habari ndiyo...nasikia harufu ya ankara...ahaaa haa mambo ya fleva hayo!
hayo ya BOT tusbiri report tuone JK atasema nini,na hili waandishi wasimwachie!
 
522 billions? hizo ni kama 450m USD hizo ni pesa nyingi sana,nina uhakika wanaotusaidia wakijua watakata misaada yote mara moja maana huo ni umafia wa hali ya juu
 
Sisi ndo viongozi wa kitaifa na wabunge wa Karne hii ya 21.

Hawa vigagula wasituletee utani kwenye uchumi wetu.

Hizo mali walizo iba naomba wajiandae tu, tena wajiandae hasa, kwani tutawadai wao, watoto wao, wajukuu zao mpaka vilembwe wao.Wasijidanganye hata kidogo.

Bila kujali kwamba mtu alikuwa Rais, Waziri mkuu, Mkurugenzi wa usalama wa Taifa au tarishi, hakuna mtu ataachwa kubanwa kisheria na kudaiwa mali aliyoiba Tanzania na kuamriwa kuirudisha kwa hiari yake mwenyewe au kufilisiwa na kuonja adha ya KEKO.

Tena kwa taarifa yao hawa Manyang'au mambo haya yatafanyika na kufanikiwa katika uhai wetu si wakati tukiwa wafu.

Nimesema.
 
Mambo ndio hayo. Sasa majibu ya report ndio hivyo yametoka. Mwanzoni hayakutolewa na tukaambiwa finishing yake inafanyika London, sasa imemalizika, na ilikuwa ipelekwe kwa waziri wa fedha Meghji, sasa kumbe amekabidhiwa Mwanasheria Mkuu, akishapitia huyo then anakabidhi kwa Meghji na ndio Meghji amkabidhi Rais aichambue naye pia atoe uamuzi wa yes or no kuwasomea wananchi maamuzi haya. Naona mlolongo unakuwa mwingi. Mimi nilifikiri baada ya chombo hicho kumaliza kazi na wananchi wakakubali kuwa watavuta subira ikamaliziwe Uingereza, sasa imemalizika, Rais angeipata mara moja. Hawa wanaojidaio kuipitia labda majina yao yamo humo, sasa unafikiri watajiwashia moto?????? Kuna utata hapa. Mara tutasikia wamemuajiri tena Mwanasheria Nimrod Mkono naye kuipitia upya hiyo report wakati naye ni mwizi namba wa one aliyetumia mtandao huo huo!
Tunataka wote kuanzia Mkono, viongozi waliostaafu na waliopo wakitajwa kwenye hiyo report, hatua zichukuliwe...sidhani kama kutaitajika uchunguzi mwingine maana hapo itakuwa ni kutumia vibaya pesa ya walipa kodi.
 
Hivi ni pesa ngapi hiyo kampuni imelipwa kufanya huo uchunguzi??? Mimi nafikiri kuwe na utaaratibu kwamba taarifa ya report hiyo ikisomwa na kuonekana kuna utofauti na kampuni ilivyoiandaa, basi kampuni iwajibike kutusomea the original one. Ila sasa hapa hatujui mikataba yao kufanya hii kazi ilikuwa vipi! Hapa kuna moto mkubwa...nina uhakika walio wengi matumbo moto....na Thomas Ngawaiya akiwemo!
 
Tunaanza kuchekelea mimba ilhali mtoto hajazaliwa! Hiyo ripoti imepakwa rangi tu hakuna kitu ni magumashi matupu... yale yale ya kushughulikia dagaa na kuacha mipapa na karambisi....
 
Tunaanza kuchekelea mimba ilhali mtoto hajazaliwa! Hiyo ripoti imepakwa rangi tu hakuna kitu ni magumashi matupu... yale yale ya kushughulikia dagaa na kuacha mipapa na karambisi....

Hata sisi tunajua kusoma, watupe report kama ilivyo ili tuchambue wenyewe.

Wakuu, hakuna anayeweza kutuibia hiyo report ili tuanze kuifaidi?

Hata wakiificha tutaipata tu, the question is not if we will get it but when we will get it.

Umevuja mkataba wa Buzwagi ndio iwe hii report ambayo watu kibao watapewa copies?
 
Hivi Report za Audit zinatoka mbili in one assigment au Moja.
Maana Enerst & Young wametoa sasa hiyo ya CAG ya Nini au ndio katika taratibu za kui-water down ya Young and Enerst? plus Vice Versa
 
Ujinga tupu wanaleta maluelue, kwa nini wasiweke hiyo ya E & Y ili tujue nani kaweka pumba.
 
Posted Date::11/29/2007 MWANANCHI
Ukaguzi wa Benki Kuu Tanzania wabaini kasoro
*Ripoti za awali zaonyesha utata

*Baadhi ya vigogo BoT watajwa kuhusika

*Wahusika kuchukuliwa hatua

*Meghji asema hajaipata, iko kwa CAG

Na Ramadhan Semtawa

JOTO la tuhuma za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limepanda, kutokana na taarifa za awali za ukaguzi kuonyesha kuwa kuna utata katika matumizi ya akaunti hiyo.

Ukaguzi huo ulifanywa na Kampuni ya Ernst & Young katika kipindi cha siku 60, kuanzia Septemba na kukabidhi ripoti yake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wiki iliyopita.

Hata hivyo, ikiwa ni wiki moja tangu CAG kukabidhiwa ripoti hiyo, taarifa za awali kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya serikali, zinaeleza kwamba baadhi ya vigogo ndani ya BoT wanatajwa kuhusika na malipo hayo yenye utata.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, vigogo hao wanahusishwa na ama kuidhinisha au kuhusika kwa namna moja au nyingine katika malipo hayo.

Vyanzo hivyo vilifafanua kwamba, maamuzi kuhusu ripoti hiyo yanatarajiwa kuchukuliwa kabla ya mwaka mpya.

"Watu watapata zawadi ya mwaka mpya, uchambuzi unaendelea kufanyika, lakini taarifa za awali zinaonyesha hivyo," kilisema chanzo cha habari kutoka serikalini.

Vyanzo hivyo vilifafanua kwamba, kuna baadhi ya stakabadhi za malipo ambazo zimeanza kuchambuliwa na zinaonyesha kuwa zimejaa utata.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, uchambuzi huo umezingatia kwa kina nyaraka za msingi za malipo ili kuona utata huo unasababishwa na nini.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, ukaguzi huo ambao uliingia kwa ndani na kuhoji watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Fedha, Zakia Meghji unaweza kubadili hali ya kisiasa nchini katika kipindi cha kuingia mwaka mpya wa 2007/08.

Meghji alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana kuhusu ripoti hiyo, alisema hadi sasa bado iko kwa CAG.

Alisema hafahamu lolote kuhusu kilichomo ndani ya ripoti hiyo kwani hajaiona na wala hawezi kuzungumza yaliyomo kwa sasa.

"Hadi sasa ripoti iko kwa CAG, sijaipata kama ni suala la maamuzi na nini kilichomo ni hadi ichambuliwe, nikiipata, nitaipitia, atapewa Rais na maamuzi yatatangazwa kwa umma," alisema Meghji.

Kauli hiyo ya Meghji ni ya pili ambapo ya kwanza ilitolewa na CAG ambaye wiki iliyopita alisema ofisi yake inafanyia kazi mambo yaliyomo katika ripoti hiyo, lakini hakufafanua.

Ernst & Young, awali ilipaswa kuikabidhi ripoti yake serikalini Novemba 10 ikiwa ni kumalizika kwa siku 60 za kufanya ukaguzi huo, lakini haikufanya hivyo na kuiomba serikali wiki tatu kwa ajili ya kuandaa ripoti ambayo ilifanyikia London, Uingereza.

Ripoti hiyo inasubiriwa kwa hamu na Watanzania kuona ukweli wa tuhuma za ufisadi ambazo zinadaiwa kufanywa katika EPA kwa ajili ya malipo ya vocha mbalimbali.

Nchi wafadhili pia zimesema zinasubiri kwa hamu matokeo ya uchunguzi huo kwani ni kipimo cha kuona mwelekeo wao wa kuongeza misaada kwa Tanzania katika bajeti ya mwaka 2008/09.

Kampuni hiyo ilipitia mahesabu katika kumbukumbu za vocha za malipo yaliyofanywa na BoT katika kipindi cha mwaka 2005/6, kubaini kama kuna ukweli juu ya madai ya ubadhirifu wa fedha katika benki hiyo katika kipindi hicho.

Agizo la kutafuta kampuni ya kukagua vocha hizo na mahesabu ya BoT, lilitolewa na Waziri Meghji Desemba 3, mwaka jana akimtaka CAG kuteua kampuni huru ya wakaguzi wazoefu wenye sifa za kimataifa kupitia baadhi ya kumbukumbu za matumizi ya fedha za benki za mwaka 2005/2006 ili kuondoa utata.
Ndg zangu watanzania,ni hatari kua na waandishi kama huyu wa gazeti hili la mwanachi bwana SEMTAWA.

Ukitazama kuanzaia mwanzo hakuna uthibitisho wa hayo anayosema all he is trying to tell us ni mawazo yake
Ukitazama bwana semtawa anatumia historia ya yaliyokua yakisemwa bila facts iam asking my self siku ripoti ikitoka na kuthibitisha kua hakuna issue GAZETI hilo lita fanya nini?

ni hatari ktk jamii kua na gazeti ambalo linheshimika na kuruhusu waandishi wake kutumia zaidi hisis bila FACTS i thought wange andika hayo kua wanu wanamatumbo joto semtewa angewataja hao vigogo anao wasema,ukitazama MEGHJI amesema hajapata ripoti CAG amesema anaipitia bado no comment sasa kama ana facts hauna mwandishi anaandika nini kama si speculations only?

Nakumbuka kampuni hii anayofanyia kazi bwana semtewa iliwahi kufikishwa mahakamni na bwana Mramba kwa kudai kua ALEX STUART MD WAKE NI MTOTO WA MRAMBA kitu ambacho walishindwa kuproove.huu ni mfano tu wa kuonyesha hatari ya kuandika bila facts.

Narudi ktk hoja sipingi kua kuna uchunguzi unaendelea ila ninachopinga hapa ni kua why mwandishi anaandika bila kua na facts.

Najiuliza is it elimu yake ina shida au ni agenda ya gazeti au ni wahariri wana agenda bcs nimekua nafatilia habari nyingi zinakua sensational na hazina facts a good example ni hii habari ya SEMTAWA inaonyesha hakuna facts but its full of speculation na hisia zake tu.

THANKS

ZIDUMU FIKRA ZA MUASISI WATAIFA HILI
 
Hiyo taarifa ya huyo Semtawa ni BS ya mwaka!!

Speculations speculations........

Siku hizi nakuwa sina hata gazeti la kusoma..... Magazeti udaku mtupu!
 
Hizi stori za JK na Tume, upepelezi bora zingeonekana kwenye udaku maana ishakuwa bla bla hadi uchaguzi ufike hakuna kinachoendelea. Ni shimo lingine la kupotezea hela zilizobakizwa na mafisadi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom