JK kazindua umeme Njombe Lakini kashindwa kuzindua umeme unaopita Kwa Kakobe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK kazindua umeme Njombe Lakini kashindwa kuzindua umeme unaopita Kwa Kakobe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Jan 20, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Jk ameshindwa kuzindua umeme unaopita Kwa Kakobe kwa taariha kwamba hauwaki na mpaka sasa matengenezo yanaendelea kwenye nguzo 19 kwa miaka 2 sasa
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Kikwete azindua mradi wa Umeme uliojengwa na Kanisa Katoliki[/h]
  [​IMG]


  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) na aliye kulia kwa Mbunge Deo ni ambaye amevaa shati jeupe lenye roman collar ni Askofu wa jimbo katoliki la Njombe, Mhashamu Alfred Maluma, mara baada ya kutua mkao makuu ya tarafa ya Mawengi Ludewa kufungua mradi wa umeme ulioasisiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki kupitia Parokia ya Madunda.


  [​IMG]  Aliye katikati ya Rais Kikwete na First lady Mama salma, ambaye ana shati jeupe lenye roman collar ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe Mhashamu Alfred Maluma. Ni mchezaji mzuri sana wa mpira wa miguu, na siku za nyuma kabla hajateuliwa Na Pope kuwa Askofu akiwa jimboni Njombe kwa kushirikiana na Padre Chaula mkurugenzi wa vijana, alianzisha timu ya mpira wa miguu kutokana na umoja wa vijana katoliki Njombe (UVIKANJO) timu ambayo ilipanda daraja hadi kucheza Ligi kuu na ilizoeleka kuitwa timu ya Baba Askofu, wakati huo askofu wa jimbo la Njombe alikuwa Askofu mstaafu Raymond Mwanyika. Timu hiyo ilisuasua wakati Mhashamu Alfred Maluma alipohamishiwa Peramiho Songea kuwa Rector (gombera) wa Serminari Kuu Peramiho ambako uteuzi wa kuwa askofu ulimkuta akiwa instructor wa Seminari hiyo baada ya kuhitimu chuo kikuu cha Rome, Italy, alikosoma Dr. Slaa.  RAIS KIKWETE APONGEZA KANISA KWA MRADI WA UMEME ,ATAKA WANANCHI KULIPA BILI KWA WAKATI


  RAIS Jakaya Kikwete amelipongeza kanisa la Romani Katoliki jimbo la Njombekwa kusaidia serikali kutatua tatizo la umeme kwa wakazi wa kijiji cha Mawengiwilaya ya Ludewa huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza nyanzo vya maji ilikuwezesha maradi huo wa umeme wa gharana nafuu kwa wananchi kuendeleakusambazwa zaidi katika vijiji vingine vya wilaya ya Ludewa kwa msaada wa kankisa hilo.Akiwahutibia wananchi wa kata ya Mawengi mara baada ya kuzindua mradi wa umeme wa Lumama Electrical Asosoation jana ,Rais Kikwete alisema kuwa hatari ya maradi huu kufa itasababishwa na wananchi wenyewe wa kata hiyo iwapohawatatunza vyanzo vya maji na kusababisha mradi huo ambao unategemea zaidi maji ili kuendeshwa kushindwa kufanya kazi kwa uhakika .


  "Waswahili wanasema hivi kitunze kidumu ,kitunze kikutunze ….sasa nawapongeza mmeanzisha chombo chenu cha kusimamia mradi Lumama …..sasa nawaombeni Lumama iendelee kusitawi ili kuhakikisha mazingirahayaharibiwi na maji yanaendelea kuwepo kwani kama vyanzo vya maji vitaharibiwabasi mradi utakufa….pamoja na kuwa maji haya ni neema ya Mungu ila Mungu ametua maarifa ya kuvitawala vyanzo hivyo ili vidumu zaidi kwa kutumia kanunizinazotawala mazingira ili yaendelee kuwepo" Hivyo aliwataka wananchi kupitia umoja wao wa Lumama kuhakikisha wanatunzavyanzo vya maji kwa kutoharibu ovyo mazingira , kuchangamkia fursa hiyo kwakuingiza umeme katika nyumba zao huku akiwakumbusha kulipa bili kwa wakati . Aidha alisema kuwa serikali kupitia shirika lake la huduma ya umeme vijijiniitaendelea kusaidia mradi huo ili uweze kusonga mbele zaidi na kuwanufaishawananchi wengi .


  Rais Kikwete pia aliwahakikishia wananchi na wahisani hao kuwa serikaliimeendelea kutoa mchango wake katika mradi huo na itaendelea kuaunga mkonojitihada za kanisa hilo na wahisani wake kwa kusaidia fedha zaidi kwa awamu ya pili ili kuwezesha mradi huo kujitanua zaidi. Alisema kuwa hadi sasa makao makuu ya wilaya ya Ludewa kuna umeme wa Genereta ila bado mkakati wa serikali ni kuiunganisha wilaya hiyo ya Ludewa na umeme wa uhakika wa Gridi ya Taifa ambapo kazi hiyo kubwa mchakato wakeunaandaliwa. Pia alisema kuwa mkakati mwingine wa serikali ni kupeleka umeme wa gridi yaTaifa wenye uwezo wa KW 232 kutoka Makambako wilaya ya Njombe kuelekeaSongea mkoni Ruvuma na kuwa umeme huo utapoonza madaba ili kufikia KW 11na baada ya hapo wananchi wa vijiji vya Ndolela ,Mkongobaki, Shauri moyo ,Mavanga , Mndindi ,Lugarawa ,Mbwila,Mkiu ,Mlangali na Luana . Alisema kuwa wananchi wa kata hiyo ya Mawengi mbali ya kuwa na mradi huo wa umeme wa Lumama bado serikali ipo katika mchakato wa kupitisha umeme wa gridi ya Taifa utakaotokea katika kituo cha Madaba na kupitishwa katika maeneo yao kwenda makao makuu ya wilaya.


  Rais Kikwete kabla ya kufika katika kijiji hicho alizuiwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali kata ya Mlangali ambao waliziba barabara na kulazimika kusimama kuwasikiliza na kujibu madai yao mbali mbali likiwemo na kuchelewa kufika kwa gari la wagonjwa ambao alipata kuwaahidi wakati wa kampeni ,tatizo la soko la Mahindi kusimama na kero ya maji ambapo aliwahakikishia kuwa malalamiko hayo yatafanyiwa kazi na majibu ya madai yao atampa mbunge wao Deo Filikunjombe iliawafikishie. "kwanza niwashukuru sana wananchi wa Ludewa kwa kukichagua chama cha mapinduzi (CCM) na kumpitisha mbunge wenu Deo Filikunjombe bila kupingwa ….sasa nawahakikishieni madai yenu yatafanyiwa kazi na kuhusu soko la mahindi wiki ijaya fedha za kununua mahindi zitakuja hapa"


  Kuhusu liganga na Mchuchuma Ludewa ,Rais Kikwete alisema kuwa sasa umefikawakati wa kuanza kutekeleza mradi huo kwa kampuni kutoka nchi ya China ambaokuanzia wiki ijayo wawekezaji hao watafika na kuanza kutekeleza mradi huo na ajira 8000 hivyo kuwataka vijana kuacha kuhoji juu ya maisha bora na badala yake kwenda kuomba kazi . Hata hivyo alisema barabara ya lami ya uhakika na Reli kwa ajili ya kupitisha makaa ya mawe na chuma kutoka wilaya ya Ludewa na kwenda kuyauza nchi za nje mkakati wake kuanza kuandaliwa . Alisema kuwa kila jambo lina wakati wake na kuwa sasa ni zamu ya wilaya ya Ludewa kubadilika kimaendeleo .  Awali mbunge wa jimbo hilo la Ludewa alimweleza Rais Kikwete kuwa pamoja naTaifa linasherekea miaka 50 ya Uhuru ila wakazi wa wilaya ya Ludewa wao baada ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika mwaka huu chini ya utawala wa RaisKikweye ndio wanapata uhuru wao baada ya kuwa na uhakika wa barabara ya lami na kuanza kuchimbwa kwa mradi wa Lingana na mchuchuma.

  Kwa upande wake meneja wa mradi wa umeme wa Lumama Alice Michelazziakisoma taarifa ya mradi huo mbele ya Rais Kikwete alisema kuwa mradi huo ulianza toka mwaka 1998 kwa kufanyiwa utafiti uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 8.900. Hata hivyo alisema kuwa shughuli za mradi kwa sasa ni kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha KW 150 ambao tayari umekamilika mwaka 2010 nakuwa kanisa Katoliki jimbo la Njombe linatekeleza mradi huo kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ACRA.

  Aliwataja wahisani wengine kuwa ni wizara ya mambo ya nje ya Italia,mkoa wa Lombaridia-Ilaty,Itervita,Foranzione Cariplo na umoja wa nchi za Ulaya

  Last edited by Candid Scope; 14th November 2011 at 15:07.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mbona hii habari inataka kupnyesha kama vile ni kweli?...Hivi hakuna wanaoishi maeneo ya tukio pale mwenge kwa Kakobe watujuze kama umeme kweli haukatizi kanisani kwake?
   
 4. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  umeme uliojengwa na Wakatoliki JK amezindua lakini umeme uliojengwa na serikali yake na Japani Jk kagoma kuzindua
   
 5. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Acha uzushi, amekataa lini?
  Mradi umekamilika?
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wewe huna kumbukumbu,umeme ulikuwa uzinduliwe Oct 2010.Na Mh Ngeleja aliwambia Media hivyo. Engn Stella Manyanya alihoji Bungeni kwa nini Jk hajazindua
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Na lini JK atazindua mradi mkubwa kama huu uliojengwa na waislam?
   
 8. SAMMY DANNY

  SAMMY DANNY Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukweli ni huo ememe wa msongo mkubwa unaopita katika kanisa la Askofu Kakobe bado haupiti. Umeme unatoka kwa nguvu kwenye kituo cha ubungo lakini ukifika kanisani hapo ambapo ni kituo cha 19 nguvu inapuangua na kushindwa kufika katika kituo cha makumbusho. Zaidi habari hii inapatikana katika gazeti la ANIKA UKWELI la tarehe 19 alh -25 2012 for reference, pia serikali inajua ukweli wote lakini imekaa kimya kuogopa aibu kwa sababu Askofu Kakobe alishawaonya wakamzarau na msimamo wake ni Ngeleja na wenzake wakatubu ndipo mambo yatatulia. Pia emesema yaliyompata Jairo ni madogo makubwa yanakuja. Jamani haya sio maneno yangu lakini Anika ukweli limeeleza yote!!
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  kumbe waislam ndio wameujenga?
   
 10. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Jina la gazeti tu linatia wasiwasi .... Haya magezeti yatawadanganya wasiokwenda shule tu ..
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Kwa wanaoishi nyumba za viongozi hapo victoria/merry water wanaweza kutujuza pia!
   
 12. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Efficiently brainwashed!

  But with an element of superstition.
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kwa hivo kakobe ni mchawi sio?
  kama kweli umeme haupiti hakuna mtu wa mungu aweza fanya hivo kuzuia umeme
  sasa ataumbuka yeye na sio serikali.
   
 14. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  BAN ni halali yako
   
Loading...