JK Katika Uzinduzi wa Jengo Jipya la CAG, Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,449
Wanabodi,

Nimetokeo kuwepo maeneo ya Kirua Vunjo, Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro, katika pita pita zangu Moshi mjini, nikalisikia gari la Matangazo likitangaza mwaliko kwa wananchi wote kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, (NAO) unaofanywa na Rais wa JMT, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kwa vile na mimi ni mwananchi, nimejisoge eneo la tukio, na nitawaletea live uzinduzi huo.

Kiukweli mkiliona jengo lenyewe lilivyo, wale mnaodai serikali ya CCM haijafanya chochote, mnakuwa hamuitei haki serikali hii ya JK imefanya mengi na inaendelea kufanya mengi, mpaka kufikia 2015, kama tutaamua kuipumzisha CCM na ipunzishwe kwa sababu tuu imechokwa, na sio ipumzioshwe kwa sababu haijafanya kitu!.

Mpaka sasa wananchi waliojitokeza ni wengi, wakiwemo wabunge Azan, Vulu na Lyatonga Mrema.

Mgeni rasmi JK ndie anaesubiriwa.

Fuatana nami nikuzue kinachoendelea.

Pasco.
NB. Pasco wa jf sio mwanachama, mshabiki wala mfuasi wa chama chochote, bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli na muumini wa falsafa ya ukweli daima "nothing but the truth".
 
kuna nafasi za kazi huko...maana kama ni mambo ya ukaguzi lazima kuna hela sana hapo..mi nipo tayari wanilipe mshahara 20000 kwa mwezi unantosha
 
sio' umetokea kuwepo' sema uko kazini kwako utatokeaje mahali bila sababu maalum?
 
Mzee Lyatonga amenikaribisha TLP na ameniahidi kuniachia jimbo la Moshi Vijijini mwaka 2015!. Nimemwambia Wachagga wana ukabila mbaya sana, hawezi kumchagua mtu asiye Mchagga, wataniita "Chasaka", amesema yoyoye ambaye yeye Mrema atakayemshika mkono ndio mbunge wa Moshi Vijijini 2015, akasema hata diwani wake aliyewapokunya jimbo CCM kwenye huu uchaguzi wa juzi ni Mhaya!. CCM walipiga kelele za "chasaka, chasaka, yeye akawasisitizia hakuna cha chasaka wala nini, CCM imepigwa chini na Mhaya ndiye diwani uchagani!. Kama kwa Moshi limewezekana, na tusubirie Mchagga huko Bukoba!.
Kumbe Tanzania hakuna ukabila wa kikwelii bali ni watu tuu ndio wanauzingizia!.
P.
 
pasco.
Nb. Pasco wa jf sio mwanachama, mshabiki wala mfuasi wa chama chochote, bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli na muumini wa falsafa ya ukweli daima "nothing but the truth".

:ranger:
 
...wale mnaodai serikali ya CCM haijafanya chochote, mnakuwa hamuitei haki serikali hii ya JK imefanya mengi na inaendelea kufanya mengi, mpaka kufikia 2015, kama tutaamua kuipumzisha CCM na ipunzishwe kwa sababu tuu imechokwa, na sio ipumzioshwe kwa sababu haijafanya kitu!....
Pasco , sifikirii kama wanaosema CCM haijafanya kitu literally wanamaanisha "haijafanya kitu"! Nadhani mara nyingi wanakusudia kuwa 'haijafanya vya kutosha' au 'haijakidhi matarajio ya wananchi walio wengi' (at least that how I interpret). Kwa mfano kama matarajio kutoka kwa serikali ya JK yalikuwa ni maisha bora kwa kila mtanzania, suala la kujiuliza je ni kwa kiasi gani maisha ya kila mtanzania yamekuwa bora tangu ashike madaraka 2005? Je tukiangalia potential ya resources tulizonazo katika kutuletea maendeleo, je tumeweza kuzitumia vizuri? Bado Rais wetu mpendwa amekuwa ni wa kuzunguka kutembeza bakuli tu mpaka mara nyingine inatia aibu kujitambulisha kama mtanzania!

Nasubiri kwa hamu kusikia jengo hilo linalofunguliwa limetugharimu shilingi ngapi na kama zimetokana na kodi yetu au ndio hivyo tena wakubwa "wametusaidia" kujenga!
 
Mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete, ameshawasili, amepokelewa na ngoma na kufuatia utamu wa ngoma, Waziri Magufuli, akajitosa kuwa miongoni mwa wapiga ngoma, na kumbe jamaa ni mpiga ngoma mahiri!.
 
Ukafuatia utambulisho rasmi, mtambulishaji akaanza kwa kumtambulisha M/Kiti wa CCM wa Mkoa!, as if hii ni sherehe ya Chama cha Mapinduzi!, hakuishia kwenye kumtambulisha tuu bali kumkaribisha asalimie!. Kwenye shughuli ile, kulikuwepo mawaziri, wabunge, CAG, Mkuu wa mkoa, wote hawa hakuwaona kuanza nao bali M/Kiti wa CCM wa Mkoa!.
Bahati nzuri, MC wa shughuli hiyo, hilo akaliona na kulitolea ufafanuzi kuwa sherehe hii ni ya kitaifa na sio ya chama fulani!. Hivyo akamuomba rais, kwa vile M/Kiti wa CCM mkoa ametambulishwa, na Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na miongoni mwa waalikwa ni M/Kiti wa Taifa wa TLP, Lyatonga Mrema yupo, nae apewe furasa ya kusalimia.
 
Ofisi za CAG Mkoa wa Kilimanjaro zimejengwa 'Vunjo? Kwanini sio Moshi mjini?
 
sio' umetokea kuwepo' sema uko kazini kwako utatokeaje mahali bila sababu maalum?
Mkuu Nivea, mimi nina kaji connection fulani kule Kirua Vunjo, from tome to time, nimekuwa nikipandisha sana mgombani. Breaki yangu ya kwanza hukuwa ni kusimama mahali panaitwa Kawawa Rodi!, pale pana kaji bar fulani, inauza "ile kitu" ni Balaa!. Nikipandisha juu lazima nisimame mahali nipige kitochi!.

Kwa wakazi wa Moshi na vitongoji vyake, hii iventi, inatangazwa live na redio ya Moshi FM.
 
Mzee Lyatonga amenikaribisha TLP na ameniahidi kuniachia jimbo la Moshi Vijijini mwaka 2015!. Nimemwambia Wachagga wana ukabila mbaya sana, hawezi kumchagua mtu asiye Mchagga, wataniita "Chasaka", amesema yoyoye ambaye yeye Mrema atakayemshika mkono ndio mbunge wa Moshi Vijijini 2015, akasema hata diwani wake aliyewapokunya jimbo CCM kwenye huu uchaguzi wa juzi ni Mhaya!. CCM walipiga kelele za "chasaka, chasaka, yeye akawasisitizia hakuna cha chasaka wala nini, CCM imepigwa chini na Mhaya ndiye diwani uchagani!. Kama kwa Moshi limewezekana, na tusubirie Mchagga huko Bukoba!.
Kumbe Tanzania hakuna ukabila wa kikwelii bali ni watu tuu ndio wanauzingizia!.
P.

wakati mwingine unakosa point,unataka kuanza kueneza ukabila bila sababu za msingi,mwandishi wa habari kama wewe habari zako ni uccm to kaka,2015 sio mbali sana
 
Hi sasa rais ndio amellifungua rasmi hili jengo, amekata utepe, amepanda mti wa kumbukumbu, sasa anahutubia!.
 
wakati mwingine unakosa point,unataka kuanza kueneza ukabila bila sababu za msingi,mwandishi wa habari kama wewe habari zako ni uccm to kaka,2015 sio mbali sana
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo niko huru kujiunga na chama chochote!. Na nikiamua kugombea kupitia TLP utasema nini?.
 
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo niko huru kujiunga na chama chochote!. Na nikiamua kugombea kupitia TLP utasema nini?.

Pasco wewe huwezi kuaminika hata kidogo,hata ukienda TLP watakutilia mashaka Mkuu,sijui elimu yako lakini sipendi utendaji wako wa kazi,usinielewe vibaya mara nyingi nimekuwa na wewe kwenye mikutano na makongamano mbalimbali,thats all
 
CAG katika maelezo yake amekiri, Awamu hii, imefanya mengi!, wanaojifanya hawaoni kitu, wanajifurahisha tuu kwa nafsi zao, vitu vya kuonekanika, vinaonekanika!.
 
Update itaishia hapo simu betri dowm. aliyeko kwenye moshi fm endelea kutu update!
 
Back
Top Bottom