JK katika mgogoro huu, bado hufikiri kuwa umeshindwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK katika mgogoro huu, bado hufikiri kuwa umeshindwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwalufunamba, Jun 29, 2012.

 1. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2005 Jakaya Kikwete alijibu mara mbili kwa waandishi wa habari sehemu mbili tofauti, katika nyakati tofauti, kuwa “sifikirii kushindwa”. Majibu hayo aliyatoa baada ya kuulizwa swali kwamba “itakuwaje iwapo licha ya maandalizi yote aliyofanya atakosa kuteuliwa”{na CCCM kuwa mgombea wa Urais}

  Akiandika makala yake ya tarehe 8 Agosti, 2010 yenye kichwa cha “JK bado hafikirii kushindwa?” Ansbert Ngurumo anasema,
  “Lengo ni kuhakikisha kwamba kwa njia safi au chafu, mtu wao anashinda. Muhimu kwao si wananchi kuchagua mtu wanayemtaka, bali kuhakikisha kwamba yule asiyefikiria kushindwa, anashinda.
  Huu ni uchafu wa kisiasa. Unajenga urithi mchafu kwao na vizazi vyao. Wanacheka leo, lakini wanaweza kujikuta wanaliingiza taifa katika maafa yale yale tunayosikia katika nchi nyingine”
  Mwishoni alimalizia kwa kusema “Wafanye watakavyo, lakini hili halikubaliki. Wanatengeneza bomu ambalo siku litakapolipuka, wao pia hawatabaki salama.”
  Makala hiyo haikuifurahisha Ikulu, ikaisakama MAELEZO, nao wakamita Ngurumo aliyekwenda pamoja na Mhariri wa Tanzania Daima, Absalomu Kibanda pale MAELEZO. Katika kikao hicho, Ngurumo anaandika kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO (kwa wakati huo) Rapahel Hokororo alisema, “Mashuja wote hawako hai” Naye akajibiwa na msomaji wa www.ngurumo.blogspot.com kuwa “Raphael Hokororo, hata mashujaa wakifa, hawafi na ushujaa wao; bali huuacha nyuma wananchi wakautumuia kujikomboa kimawazo, kisiasa, kiuchumi, na kijamii.”
   
 2. M

  Mwalufunamba JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nami narudia mawazo ya Ansbert hapo mwishoni “Wafanye watakavyo, lakini hili halikubaliki”

  Nasema halikubaliki kwasababu maafa yote yanayotokea katika mgomo wa madaktari wa awamu hii ya sasa (na hata kukamatwa,kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka) hakuwezi kumweka kando JK.
  Wengi wataniuliza kwanini nafikiri hivyo? Vema, majibu yangu mepesi ni haya. Katika mgomo wa awamu ya kwanza, Pinda alimaliza kwa kutoa ahadi alizoshindwa kuzitekeleza. Katika ule wa awamu ya pili, Kiwete alimaliza kwa kuwapa ahadi Kamati ya madaktari walipokutana IKULU, lakini utekelezaji wake ndiyo huu unaotajwa kuwa ni sawa sufuri.

  Ikiwa suala lilikwisha kuwa katika mikono ya Kiongozi wa juu, na mgomo unatokea katika awamu nyingine ya tatu, anayewajibika kuutatua, si mwingine ni yeye, la kama hili si sahihi basi aliye juu yake na aje autatue.
  Kitendo cha kusema Pinda aushughulikie ni kama kutaka kumvua nguo mkubwa endapo akija na suluhu ya uhakika. Katika utawala bora hakuna kitu kama hicho.

  Je bado JK hafikirii kushindwa katika kuutatua mzozo huu? Kama anafikiri kushindwa kwanini asiombe msaada kwa viongozi wengine na kukubali kuipunguza bajeti ili pesa nyingine ziende kununua vifaa tiba upesi? Je, serikali iendelee kuwatesa wananchi wake kwa kuwanyima huduma za afya ambayo ni msingi wa shughuli za uchumi? Je, tusuburi viongozi wengine wa madaktari waendelee kutekwa, kuteswa na kuuawa kwa sababu huyu wa kwanza aliponea katika tundu la sindano? Je, wanachi wataendelea kuyakubali haya yanayofanyika”
  JK unawajibika katika hili. Ndiyo! Wewe binafsi na wala si mwingine na wala asitupiwe mzigi huu mtu mwingine.
   
Loading...