JK Kanyaga twende, ukombozi wa watanzania u mikononi mwako!

Mpaka hapa kweli naona mambo yamegoma kabisa. Kama ni mashine basi ndio kusema imenoki jumla.
 
Unasuggest kipengele cha Katiba kitakachoaccomodate haya maoni yako kisomeke vipi, I mean toa mfano.
Wataalamu wa kuandika hayo mambo ya katiba should know it better. Cha msingi tu mfumo ulinde hiyo misingi niliyoianisha. Hapo nadhani mambo yatakuwa poa.
 
Na huo ugumu wa maisha uwaendee zaidi wale waliochagua ccm, hawataki mabadiliko ukiwauliza ccm imewafanyia nini? wanajibu ooh baba zetu ni ccm nasi ni ccm! Pumba tupu kichwani mwao.

wameweka CCM kama dini vile! dini zenyewe watu wanahama kilasiku! wana mtindio wa akili

Ok fine

Sasa dawa ni nini? Uchaguzi? Siasa? i don't think so.

Shida ikitokea, wakati haujui familia yako itakula nini usiku, hujui utapata wapi pesa za kununulia dawa za watoto! akili itakuja we will not wait elections or politics, we will do actual things at that particular time kujikomboa na hali hiyo, matokeo ya kitakachofanyika kinaweza kikawa kibaya sana na cha kukumbukwa!!! mapinduzi yatatokea na hii ni kila nyanja.

Dawa ni kuanza upya, kwa kuweka mfumo mpya wa kujitawala usiotegemea maono ya vikundi au individuals. Mfumo utakaohakikisha uwajibikaji, uhuru, ubunifu, uwazi et c ..pengine starting point iwe katiba.

safi mkuu!


Jamani.. uchaguzi una matokeo yake. Binafsi sitaki kabisa kusikia mwana CCM au mtu yeyote aliyeunga mkono JK kurudi madarakani analalamikia iwe mafuta au dawa ya vipodozi. Watu lazima wajifunze kuishi na maamuzi waliyoyachukua.

wengi wao wanauza kahawa na kucheza bao! wengi wao ni wale wenye vipato vya hakika ambao kutuelewa tunasema nini mpaka waguswe na hali halisi!!!
 
Na bado..mpaka amalize muda wake maharage yatakua yamefikia bei ya nyama..soda bei ya bia..mafuta ya taa bei ya gesi n.k!Sasa tuombe tu muda wa kuchagua mwingine ukifika watu wakutosha wawe wameamka kiasa cha kufanikiwa kumpata kiongozi atakaejali maendeleotya nchi na watu wake.Otherwise itafika kipindi kufa itakua bora kuliko kuishi.
 
Natamani bei ya kupanga chumba kimoja Mwananyamala ifike kama millioni tatu kwa mwezi na viwanja vya nyumba kule Boko na Chanika vifikie billioni 8!!!

Cha ajabu, mpaka tunafikia hapo hakuna atakayekuwa amewajibishwa au kujiwajibisha!
 
Aliyesema "Thank God kwa kutupatia Kikwete" hakukosea... I think he epitomizes a falsified fallacy, there then only a reality check becomes vital!!
 
Na tukipata nafasi hatutaichezea!!!! upinzani wakijipanga vizuri CCM imeishatoka 2015!

Kwa watanzania hawa hawa tunaowafahamu, wa kupewa khanga, tshirt, scarf, pombe na ubwabwa!!

Halafu ukichanganya na TISS na NEC ya Kiravu na Makame, bado sitegemei maajabu yoyote toka kwa hawa watanzania tulionao.

Labda tuendelee kuombea bei zizidi kupanda hata ifike mara mia moja ya hivi sasa, huenda wakakataa kudanganyika na kuamua kufanya maamuzi sahihi hata ikiwezekana kabla ya 2015 au kama tutafika na uongozi huu 2015 basi hasira za kupanda kwa gharama za maisha zitoe majibu ya kweli.
 
Ngoja twendele tu kutumia maji ya visima, na mgao wa umeme.....
Na shule nyingi zisizo na ufanisi kwa kukosa facilities.
Na hospitali....
Na barabara mbovu mijini na vijijini...
 
Natamani bei ya kupanga chumba kimoja Mwananyamala ifike kama millioni tatu kwa mwezi na viwanja vya nyumba kule Boko na Chanika vifikie billioni 8!!!

Cha ajabu, mpaka tunafikia hapo hakuna atakayekuwa amewajibishwa au kujiwajibisha!

Umenena! vingi vimefikia bei ya kufa mtu! nyumba za kupanga mijini unazungmza USD.... per square metere.Wengi wanakimbilia chamazi na kisarawe, watu wanatafuta Bagamoyo na Mlandizi... jiji linapanuka kwenda morogoro na Tanga! watu hawaangalii kwa nini wanajazana mijini! shida kuanzia vijijini mpaka mijini!!!!! ACHA hali ngumu iongezeke..mpaka bazoka zifikie mia tano!!
 
Jamani.. uchaguzi una matokeo yake. Binafsi sitaki kabisa kusikia mwana CCM au mtu yeyote aliyeunga mkono JK kurudi madarakani analalamikia iwe mafuta au dawa ya vipodozi. Watu lazima wajifunze kuishi na maamuzi waliyoyachukua.

Mimi nilishaanza baada tu ya uchaguzi wale wananchi kule Njombe ambao kila ninapopita kwenda kwetu songea nimeacha kununua viazi na matunda yao.:frusty:
 
Na bado..mpaka amalize muda wake maharage yatakua yamefikia bei ya nyama..soda bei ya bia..mafuta ya taa bei ya gesi n.k!Sasa tuombe tu muda wa kuchagua mwingine ukifika watu wakutosha wawe wameamka kiasa cha kufanikiwa kumpata kiongozi atakaejali maendeleotya nchi na watu wake.Otherwise itafika kipindi kufa itakua bora kuliko kuishi.

bei ya chumba kimoja ambacho hakina umeme iwe laki moja kwa mwezi!!!!
 
Yale ya TUNISIA yale ndo yataikumba serikale ya jeykey..


VERY SOON
 
Sisi tunaoandika comments zetu humu jamvini sidhani kama tuna maisha magumu kama hawa wana CCM wanaovalishwa kanga, kofia, fulana na takataka nyingine kila uchaguzi ukaribiapo. Sasa hivi mtu akiniomba msaada hata kama ni ndugu yangu au mtu wangu wa karibu, namwambia aende kwa JK atamsaidia maana tumechoka na hawa watu wanaojifanya wanasahau shida zao kila uchaguzi ukifika and then ukipita wanatulilia shida.
 
Wabeloya umeginusa sana, maisha kweli yamepanda mno mimi sisikitiki sana sababu sijamchagua hata mmoja kati ya hawa wanaotuongoza kwa sasa. ndiyo maana nasema tutatia akili baada ya shida hizi kupamba moto huu ni mwanzo tu. Hili garimoshi la JK na Makamba ndiyo tumeshalipanda na sasa limeshashika kasi ya ajabu kuelekea tusikokujua.

Kwa wale tunaojidai na magari ya mikopo petrol juu, Kwa wale tunaopanga kama mimi mitaa ya Sinza, Mwenge, Kijitonyama kodi ya pango ni komesha na lazima ulipe kodi ya mwaka wakati we unalipwa kwa mwezi. Chakula bei juu, umeme bei huu na haupatikani - bado ada ya shule, matibabu kwa wale wenye watoto.

Wakenya hawakuwa mataahira kupigana bakora, Tunisia si machizi kuchapana makonde - nasisitiza tena HUWEZI KUPATA HAKI YAKO ukiwa umekaa - NEVER.

Naungana na yule mchangiaji wa mjadala wa katiba pale chuo aliyesema bila Kalinyekalinye tusitegemee mageuzi ya kweli, hakuna mtawala ambaye atakupatika madaraka kirahisi angalieni ya Ivory cost, kenya, Zimbabwe na kwengineko.

Sasa nasubiri Amani na Utulivu wetu tunaojivunia duniani baada ya hali hii kupamba moto.
 
Wafanyabiashara wengi walitoa michango yao kusuport CCM sasa ni zamu yao kurudisha fedha walizotoa! Mdhamini mkuu wa campain za ccm ni wewe mlalahoi. Nimepata taarifa kuwa mafuta ya kupikia sasa ni Tshs 52,000/= kwa ndoo kubwa! Mkate wa supa loaf sasa ni 800 kwa eneo letu!
 
Gesi (15kg) from 45,000 to 70,000
Sadolin ya mkaa iliyokuwa inauzwa 1500 sasa ni 3000

kwa sisi wajenzi nondo zile za 12,000 sasa ni 17,000! kwa kifupi vifaa vya ujenzi vimepanda sana! kama hujajenga kihalali....

Mechi inaendelea natamani hali hii iendelee ifikie watu kushindia maji tu! shida zikiongezeka haya yatatokea:

1. Akili ya kuchagua viongozi bora itakuja tu!


2. watu watakuwa sensitive na hali ya nchi na sio kukurupuka tu

3. Mijadala ya kidini haitakuwepo, maana woote wamakonde, wamalira, wanyakyusa, wachaga, wangindo, wapogo wote wana suffer the same. waislamu na wahindu, wakristo na wapagani watapata shuruba ile ile! tutaona kama akili hazitakuja kichwani,

4. wale wasomi 'graduate' wanaotembelea magari ya mikopo na kupanga Sinza, huku wakiwa weredi wa vikao vya harusi na kushinda kuchoma mafuta yaliyopanda bei HUKU WAKIWA HWANA MPANGO NA ISSUE ZA KITAIFA wataamka!!

we need same platform ili TUELEWANE!!, shida tu zitawakomboa watanzania, kelele tumepiga watu bado wanawachagua CCM!!!

Acha maisha magumu yaongezeke JK kanyaga twende!!!!

HONGERA WABEROYA. Umepiga kichwa barabara kabisa
 
Si jambo zuri unapokkuwa na wananchi wasiojua uhusiano wa maisha yao na maamuzi yao (in the first place) na serkali inayotawala (next in line). So this article is hugely a big wake-up call.

Tuombe wanapoamka hali isiwe mbaya mno (irrepearable). Sio lazima iwe 2015, kwa nini 2011 haiwezekani kurekebisha mambo?
 
Back
Top Bottom