JK Jitoe kwenye Kinyang'anyiro. Huwezi kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Jitoe kwenye Kinyang'anyiro. Huwezi kazi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Oct 22, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Mkwere ndugu yangu, mtani wangu, ninakuomba tu ujitoe kwenye kinyang'anyiro cha Urais.

  Huwezi kazi Mkwere. Kazi unayoweza Mkwere ni kukaa na Salma tu. Siyo Urais.

  Uliingia kwa mbwembwe Mkwere, lakini umeona. Unadharaulika na hata na vitoto vidogo Mkwere. Pole Mkwere.

  Mkwere unaleta utani kwenye cheo kikibwa kabisa kwa nchi yetu?

  Mkwere unatuahidi utabadili Kigoma kuwa Dubai? Aaah Mkwere? Kweli? Are you serious?

  Yaani mkwere unajisifu kuwa Rais wa kwanza Afrika kukutana na Obama. Aah, siamini mtani. Sasa kama umekutana na Obama ndo tufanye nini sisi? Hiyo nayo ni sera kweli ya kuombea kura Mkwere? aah Mkwere acha masihara bwana.

  Mkwere unawasifia Lowasa, Rostam na Mramba kuwa wachapakazi? Mkwere vipi? Unatuona sisi manyang'au vipi?

  Mkwere umezungumza mengi kwenye kampeni zako, sikuwahi kusikia hata siku moja unazungumzia ufisadi? Unaimba habari za chandarua. Kama ni chandarua hata mimi ninacho Mkwere. Acha masihara Mkwere.


  Mkwere skiza. Kwanza nikupongeze kupata nafasi ya kuiongoza Tanzania kwa miaka mi5 iliyopita.

  Inatosha mkwere. Urais siyo mchiriku wala Mnanda wa Bagamoyo. Urais ni tunu. Hiyo tunu huna Mkwere. Ni bahati tu inakufanya uitwe Rais leo.

  Tafuta shamba zuri huko kwenu Chalinze ukalime tu mihogo. Urais achia wanazuoni wenye fikra dynamic.

  Usije kusema sikukuonya mkwere.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tumsaidie wanaccm woote JK kipindi kijacho aongoze vyema bcs hatutoki madarakani kwa nguvu yeyote ilee! nani chama kimfie subirini mwaka 2015 ndo mtachukua, kwa sasa tupo fit!
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unajaribu kutumia dhima ya utani kuendeleza prejudices zako kwa watanzania wenzako. Halafu unajivika joho la UZALENDO NA UKOMBOZI.....

  Lakini pia hili ombi la kumtaka mgombea mmoja ajitoe katika uchaguzi linanikumbusha yale yaliyotokea CHADEMA wakati wa Uchaguzi uliopita na kumtaka/kumshinikiza.kumuomba Zitto ajitoe. Huu ni mfano hai kuwa wengi wenu mnaona na kuimba demokrasia pale tu inapoonyesha dalili za kuhakikisha maslahi yenu lakini sio kuwa ni waumini wa kweli wa demokrasia.

  Na hili linanipa wasiwasi kuwa demokrasia hii inaelekea kuzaa laana badala ya baraka. Naona dalili za NARC with their turn to eat agenda na zaidi hata UNAZI wa Hitler ambao ulitumia demokrasia kuhalalisha utawala na baadae itikadi yao dhalimu. Unfortunately, elements za aina yako zimejaa katika ushabiki wa UKOMBOZI wa Dr Slaa na kiasi fulani ndani ya mfumo wa CHADEMA....

  Haya ni baadhi ya mambo ambayo yananifanya nisikubaliane na UKOMBOZI wa Dr Slaa na CHADEMA kwa kipindi hiki.......
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Pole bwana.

  Najua njaa ndiyo inakufanya uipende CCM, japo kwa unafiki

  Lakini ilipaswa ujue kuwa Watanzania wengi ni masikini. Hapo hapo JK anatuambia miaka mi 5 ya uongozi wake alikuwa anafanya majaribio.

  Jamani Mkwere? Yaani can that really hold water? Tanzania, miaka 50 baada ya Uhuru, bado kuna mtu nchi hii anaweza kuomba kuwa Rais ili afanye majaribio?

  Hii inaweza kukubalika na watu kama wewe Omarilyas tu.

  Kwa mtu kama mimi bado naendelea kusisitiza kama Mtanzania kuwa Mkwere hafai. Inatosha.
   
Loading...