JK, ingekuwa faida zaidi kwenda ziara Rwanda na Botswana kuliko majuu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK, ingekuwa faida zaidi kwenda ziara Rwanda na Botswana kuliko majuu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by commonmwananchi, Feb 26, 2012.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  kwa maoni yangu, kutokana na safari nyingi za rais wetu mheshimiwa Dk kikwete,zenye kugharimu mahela kila uchao,ninapendekeza kama ifuatavyo.nikizingatia kwamba nchi hizi ziko karibu yetu na tuna mengi ya manufaa kujifunza huko kwa faida yetu na vizazi vijavyo.

  Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka taifa jirani la Rwanda,ni takriban miongo miwili tangu wanyarwanda watoke kwenye mauaji ya halaiki,ambayo si tu yalikiangamiza kizazi cha wanyarwanda kwa kiasi cha kutisha.Lakini pia yaliangamiza na kuvuruga uchumi na miundombinu ya nchi hiyo kwa kiasi cha ground zero. Na kuiacha nchi hiyo ikianza moja katika ujenzi wa taifa.kupitia serikali ya RPF chini ya rais Kagame.

  Leo hii ninapoandika sisi wote ni mashahidi kwasmba Rwanda iko juu ya tanzania,katika nyanja za uchumi,ulinzi,Elimu na hata usafi na utunzaji wa mazingira.faranga moja ya rwanda ni sawa na shilingi mbili na senti sitini za Tanzania.wanyarwanda wanasoma michepuo ya kiingereza na kifaransa kwa wakati mmoja. Na wanafanya vizuri katika soko la ajira kimataifa kuliko sisi.

  Peggine mnaweza kusema ni kwa sababu walipewa misaada mingi na jumuia ya kimataifa baada ya mauaji yale,na mimi hilo sina ubishi nalo.Lakini mkumbuke kuwa kwa sasa Tanzania ni moja ya nchi barani Afrika zinazopokea misaada mingi toka jumuia na wahisani mbalimbali
  Toka nje lakini pia hata jinsi ya kuisimamia misaada ya wahisani nalo ni somo ambalo tunapaswa kujifunza toka rwanda.na tukumbuke Rwanda hawana bandari bali wanatumia bandari yetu kupitishia maendeleo yao,lakini pia tuna raslimali nyingi za asili kuliko hiyo rwanda tena kwa kiwango cha juu sana.

  Sasa basi,wakati hali halisi ikiwa hivyo tulitarajia Rais Kagame awe ndio anasafiri zaidi ya Rais wetu.kwa kwenda huko majuu,kuliko hali ilivyo sasa.na rais wetu angebaki hapa nchini akisimamia ujenzi wa taifa kwa kutumia raslimali zetu pamoja na misaada hiyo inayotujia na kurudi ilikotoka,badala yake angehakikisha inawafikia walengwa na kutimiza makusudio ya utolewaji wake.

  Kwa vile hiyo imeshindikana,nashauri Rais wetu kwa nia nzuri tu.kwamba angekuwa anamtembelea jirani yake kagame na kumuuliza ampe mikakati mbalimbali anayoitumia yeye pale rwanda,katika kupata hayo mafanikio waliyoyafikia katika kipindi kifupi namna hiyo huku wakitutimlia vumbi wahifadhi wao tuliowatunza hapa kwetu wakati wakiwa hawana kitu.

  Baada ya hapo angekwenda zaidi Botswana ili apate mbinu mbalimbali walizozitumia katika kuhakikisha wananchi wananufaika na utajiri wa madini mbalimbali waliyonayo kule,kama sisi tulivyo hapa kwetu..lakini sisi tukiishia kupewa takwimu kila uchao bila kuyaona hayo mafanikio.

  Baada ya hayo machache ni imani yangu wanajamii forums mtaweza kutoa maoni yenu pale nilipoishia na kunikosoa pale nilipokosea ,
  Ahsanteni na ninaomba kuwakilisha...
   
 2. B

  BMT JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  hujakosea hata kidogo,ushauri mzuri,mbona marais wengne hawatembei hvi jaman,au si mahandsome?unajua jk anaboa hee,kwanni hajfunz tka kwa wenzake kibaki,mseven na kagame?anazdiwa na rais wa madagasca huyu rajorina,au kwann hajifunz kwa marais waliopta kama mkapa,anaboa bwana
   
 3. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Tena umenikumbusha wakati ule TBC walituonyesha kipindi cha ziara ya JK ya huko Mauritius nikamnukuu rais JK akisema ameona mengi ya kujifunza toka nchi ile ndogo,ambayo inatewgemea utalii tu.
   
Loading...