JK ili aaminike aliyoyasema Kwa Katiba mpya, kwanza awang'oe Werema na Kombani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ili aaminike aliyoyasema Kwa Katiba mpya, kwanza awang'oe Werema na Kombani

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Not_Yet_Uhuru, Jan 1, 2011.

 1. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakika, Tumeyapokea maneno ya JK kuhusu dhamira yake ya kuleta mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa tahadhari, isiwe tena ghiliba za kisiasa kama ilivyokwishatokea ktk utekelezaji wa tume za majaji Nyalali na Kisanga kuhusu katiba hiyo hiyo. Tunayajua yaliyokwishatokea Tanzania toka miongo mitatu iliyopita.

  Hii ya JK itakuma maamuzi yaliyokamilika kama atawang'oa kabisa hawa watu wawili ktk utawala wake yaani Jaji Werema-mwanasheria mkuu na Celina Kombani-Waziri wa sheria na katiba ambao wameshalionyesha taifa kwa kauli zao kuwa hawako njia moja na JK na Pinda.

  Hawa watu wawili ni hatari na watakuwa vikwazo na kamwe hawatamsaidia JK na watanzania kufikia lengo la Katiba mpya. Wana muono finyu, hawana lengo na ni wavivu wa fikra kuhusu dira, matakwa na future ya taifa na watanzania na hawafai kuwepo tena serikalini. Tunaomba wawajibishwa mapema.

  Naomba kuwasilisha, tulijadili.
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nianze kwa kuipongeza chadema kwa kufanikiwa kufunga hili goli la mapema maana kitendo cha serikali kuunga mkono hoja mlioianzisha ya kuandikwa upya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, siyo mafanikio kidogo. Pamoja na kuwapa pongezi hizo napenda nitoe tahadhari ya kwamba huu siyo wakati wa kubweteka. Serikali imekubali hoja yenu si kwa kupenda, bali kwa kusoma vyema matakwa ya nyakati. Katika hali hiyo, serikali itafanya kila linalo wezekana kuhakikisha ya kwamba mchakato wa uandikaji wa hiyo katiba mpya unakuwa chini ya udhibiti wake. Ndiyo maana katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya rais Kikwete amezungumziasuala la kuteua japo la kuendesha shughuli hiyo. Ikumbukwe hizi tume zinazoteuliwa na rais, hupeleka taarifa zake kwake; na ni yeye tu anayeweza kuamua kuziweka wazi kuzibakiza ni za siri. zaidi ya hapo halazimiki kutekeleza mapendekezo yake. Kutokana na hayo, jopo la wataalamu la kuratibu uandikaji wa katiba mpya, lichaguliwe na mkutano wa kuandaa katiba mpya utakao shirikisha makundi yote katika jamii, na wala siyo rais Kikwete. Kwa njia hiyo jopo hilo litawajiba kwa mkutano huo wala siyo kwa serikali.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  Naam, kama akichagua jopo ambalo limejaa wasanii basi hatuna budi kulikataa kwamba jopo hilo halistahili kwa kazi hiyo, lakini akichagua watu makini ambao wanakubalika miongoni mwa Watanzania walio wengi basi tutampongeza.
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wengi Tumesikia na Kuafuatilia Hili Swala Kubwa la Kujenga Katiba Yetu kwa Upya. Wananchi Tunataka Kujenga Katiba Kutokana na Abuses za CCM Tangu Uhuru. Leo Kuna Habari JK Maji Yamemfikia Shingoni na Anaelekea Kukubaliana na Taifa Zima. Tusisahau Jambo Lililoleta "Kuzaliwa kwa Matakwa ya Katiba" Yote Yamezaliwa Baada ya Jk Kuiba Kura Mwaka Huu Oct 31, 2010. Hii Kwanza Inadhihirisha Kukubali Kwake Kwamba Aliiba Kura na Sasa Anataka Influence Kubwa ya Kutengeneza Katiba. Hii Naamini Wananchi Hawatakubali Kumwacha JK Manipulations Kwa Kuanza Kujenga Tume ya Katiba Kutoka kwa Watu Wanaotaka Yeye na Kuripoti Kwake Apige Mhuri. This is not going to Happen.
  Kamati Itaundwa na Wanajumbe Kutoka (Sauti za Taifa Zima)

  1. Wanasheria Kutoka Chuo Kikuu
  2. Wafanya Biashara
  3. Wanawake na Wakina Mama
  4. Vijana na Wanafunzi
  5. Wawakilishi Kutoka Mikoa Mbalimbali
  6. Wawakilishi Kutoka Nje - UN Specialise in Constitution

  Utaratibu wa Kukusanya Maoni Kutoka kwa Wananchi na Vyama vya Siasa Lazima Uwe Wazi na Kukubalika na Wananchi. Chombo cha Habari cha Serikali (TBC) Kihusike Kutangaza Live Discussion na Public Tuweze Kuona Nchi Nzima. Taratibu Zitolewe Kwenda kwa Wananchi na Public Forum Iwepo. Tume Ikimaliza Kazi, Kopi ya Katiba Mpya Wananchi Wapewe Tarehe ya Kupiga Kura na Siku Maalumu Itolewe ili Wananchi Tupige Kura Kuhalalisha Katiba Mpya ya Taifa Letu. CCM ni Lazima Wajitoe Kuongoza Hii Discussion na Wananchi Watoe Maamuzi.

  "Mapambano ya Katiba Yataendelea Mpaka Tuweze Kupiga Kura Kukubali Haki Zeki na Sheria"
   
 5. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena ila kama wana busara wajiuzulu wenyewe kabla ya kuwajibishwa
   
 6. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa CCM kuongoza zoezi la katiba mpya sina imani nayo kabisa. wametuonenea sana wataogopa kujichinjia bahari kwa katiba.
  Watu ambao hawako tayari kuachia madaraka. Kuna jipya gani Zanzibar baada ya katiba mpya. Uchakachuzi kama kawaida.

  Nasema no kwa CCM wanataka ku-buy time tu.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  mkuuu,,,nakubaliana na wewe.....sikuhitaji kuwa na id mpya kusema hili. ila huo ni ukweli, uwezi kuungonzwa na crap ukategemea m.abadiliko kutoka kwa crap...
   
 8. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningekuwa mimi ndio JK, ningepigania katiba mpya ili kutimiza uzalendo katika nchi hii ya Nyerere ningeshupalia katiba mpya ipatikane na historia inikumbuke kwa hilo kwasababu miaka 5 iliyopita sina cha kukumbukwa.
   
 9. nyondoloja

  nyondoloja Senior Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wanaakili timam walijuwa wanacho kifanya usifikiri wanabahatisha tz vita hutangulia migambo wehujuwii?
   
 10. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa wana busara basi wao wenyewe wajiuzuru ili kuepuka aibu mbele ya jamii kwa kutofautiana na boss wao.
   
 11. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao ni migambo walitangulizwa kupima upepo,walipouawa ndo bosi wao akakubali ili mambo yaishe
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  JK ameshajua kwamba akikwepa suala la Katiba Mpya itakula kwake for sure kama ilivyokuwa kwa suala la ufisadi! Sijajua Kombani na Werema walitoa wapi mawazo ya kuzuia suala la Katiba Mpya huku wao wakijua kwamba hawana final say!
  Shame on them!
   
 13. j

  jitu la kale Member

  #13
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kiukweli mi binafsi Jk nampongeza sana kwa ili
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  JK aridhia Katiba Mpya
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 31st December 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 341; Jumla ya maoni: 0


  [​IMG]  BAADA ya malumbano, mijadala, maandamano na kauli za hapa na pale kudai uundwaji wa Katiba Mpya, hatimaye Rais Jakaya Kikwete amesikia na ameunda Tume maalumu ya Katiba.

  Tume hiyo kwa mujibu wa Rais, itaongozwa na mwanasheria aliyebobea na kuwa na wajumbe kutoka makundi mbalimbali ya jamii za pande zote mbili za Muungano.

  Hayo yamo katika hotuba ya salamu za Rais Kikwete aliyoitoa jana kwa Taifa katika kuaga mwaka 2010 na kukaribisha mwaka mpya wa 2011.

  “Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaoshirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya yatakayohusu Katiba ya nchi yao,” alisema Rais katika hotuba yake.

  Alisema baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya kikatiba kwa kufanyiwa uamuzi.

  “Baada ya makubaliano kufikiwa, Taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika,” alisema Rais.

  Alieleza matumaini yake kwamba mchakato huo utaendeshwa vizuri, kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya nchi na mazoea ya kujadiliana bila kugombana, ambapo wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na kwa uvumilivu wa hali ya juu pale watu wanapotofautiana kwa mawazo.

  “Pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana.

  Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema.

  “Na inapohusu Katiba ya nchi, itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa.

  Nawaomba Watanzania wenzangu wenye maoni yao, wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huu,” alisema.

  Rais alisema uamuzi huo unatokana na makubaliano yaliyofikiwa kati yake na viongozi wenzake kufanywa, hili la Katiba likiwa ni moja miongoni mwa mambo manne yaliyokubaliwa.

  Aliyataja mengine kuwa ni kuutangaza mwaka 2011 kuwa wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambayo kilele chake kitakuwa Desemba 9, ambapo kutafanyika sherehe kubwa na za aina yake nchi nzima na wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu.

  Pili, kufanyika tathmini ya kina ya mafanikio yaliyopatikana nchini, katika juhudi za wananchi kujiletea maendeleo katika miaka hiyo 50.

  “Kila wizara, idara na taasisi za Serikali na hata sekta binafsi, zifanye tathmini ya eneo lake. Tathmini hizo ziandikwe katika vitabu ili kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwetu na kwa vizazi vijavyo,” aliagiza.

  Alisema vitabu na nyaraka hizo vitakuwa kumbukumbu zenye manufaa makubwa kwa watakaokuwapo mwaka 2061 wakati wa kusherehekea miaka 100 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

  Pia ilikubalika yafanyike maonesho maalumu katika Uwanja wa Maonesho wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na mikoani, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tangu Uhuru wa Tanzania Bara.

  Na lingine ndilo la mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye kuwa na Katiba inayoendana na Taifa lenye umri wa nusu karne.

  “Katiba yetu ya sasa tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa letu, imeifanyia nchi yetu mambo mengi mazuri na kuifikisha Tanzania na Watanzania hapa tulipo.

  “Tuna nchi moja huru, ya kidemokrasia na inayoendesha mambo yake kwa kuzingatia utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili mikuu ya Dola.

  Nchi yenye amani, utulivu na watu wake ni wamoja, wanaopendana na kushirikiana na maendeleo yanazidi kupatikana,” alisema.

  Hata hivyo, aliwahadharisha Watanzania kuacha kupoteza muda muhimu wa kujiendeleza na badala yake kugeuzwa ‘mbuzi wa kafara’ kwa ajili ya kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani.

  “Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.

  “Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo, ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali.

  Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara. Kwao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa, ili kujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015,” alisema.

  Alikumbusha kuwa uchaguzi ulishaisha Oktoba 31, na malumbano ya kampeni za uchaguzi yalimalizika wakati huo. Sasa ni wakati wa kuendelea kufanya shughuli za kawaida za kujiletea maendeleo.

  “Kuendeleza malumbano na kuendelea kuishi kama vile kampeni za uchaguzi bado zinaendelea si sahihi hata kidogo.

  Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wabinafsi na wasivyokuwa na huruma na wenzao, wako tayari kuchochea ghasia bila kujali madhara yatakayowakuta watu watakaoshiriki,” alisema.

  Alisema wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya Dola kuingilia kati ili waiambie Jumuiya ya Kimataifa jinsi Serikali ilivyo katili.

  “Nawasihi ndugu zangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hawa. “Nawaomba, wakiwafuata wakumbusheni kuwa wao wana fursa nyingi za kusema wayatakayo bungeni na kwingineko, waache kuwatumia kama chambo au wahanga wa maslahi yao,” alisisitiza.

  Akifafanua kuhusu uchaguzi, alisema ulikuwa na ushindani mkali na nguvu ya vyama vya upinzani iliongezeka na kwamba ni jambo jema kwa utawala bora na uwajibikaji nchini.

  “Bila shaka Bunge litachangamka kama tunavyotarajia sote. Nimewakumbusha mawaziri wajibu wao wa kuwa makini na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi bungeni.

  Kwa upande wa Chama tawala, hatuna budi kujipanga na kujijenga upya kwa kuzingatia mazingira mapya ya kisiasa nchini,” alisema.

  Kuhusu umeme, alisema mwaka jana haukuwa na utulivu wa kutosha kwa upatikanaji wa umeme kwani mara kadhaa yalikuwapo matukio ya kukatika na mgawo wa umeme, kutokana na uharibifu wa mitambo ya kuzalisha umeme hasa katika kituo cha Songas na vituo vya Tanesco.

  Alisema kwa sasa Tanesco ina mipango kadhaa inayoendelea nayo ya kuongeza uzalishaji wa umeme nchini ambapo kwa msaada wa Serikali, ndani ya miezi 12 ijayo, Tanesco itaongeza uzalishaji wa umeme kwa megawati 160, (100 Ubungo kwa kutumia gesi asilia na 60 Mwanza kwa kutumia dizeli nzito).

  Alisema kwa kushirikiana na sekta binafsi pia, ndani ya miezi 36 ijayo Tanesco wanatarajia kukamilisha ujenzi wa vituo vya umeme Kinyerezi (megawati 240) Somanga Fungu (230) na Mtwara (300).

  Inatarajiwa pia kwamba katika kipindi hicho mradi wa kuzalisha megawati 200 Kiwira utakamilika. Kuhusu bei ya umeme, alisema anatambua kuwapo mazungumzo katika jamii kuhusu uamuzi wa Ewura wa kukubali ombi la Tanesco kuongeza bei ya umeme.

  “Wakati mwingine mazungumzo yamekuwa na hisia kali na hata jazba kutawala”. Alisema Wizara, Tanesco na Ewura wameeleza kwa ufasaha misingi iliyotumika mpaka kufikia uamuzi huo. “Sina maelezo mazuri zaidi ya hayo.

  Ninachotaka kusema ni kuwaomba Watanzania wenzangu kutokubali suala hili la kibiashara na kiuchumi, kugeuzwa kuwa la kisiasa na kutafutiwa majawabu ya kisiasa”.

  Aliwaomba Watanzania waamini na kukubali maelezo ya Tanesco na Ewura kwamba katika miaka minne hii gharama za uendeshaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme zimepanda kama zilivyopanda katika shughuli nyingine.

  “Hivyo basi, kutaka bei ya umeme ibaki kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita hautakuwa uamuzi sahihi kiuchumi na kibiashara kwa Tanesco.”

  Aliwatakia wananchi mafanikio mema katika shughuli za kujiletea maendeleo na kuendeleza hali zao za maisha na Heri ya Mwaka Mpya.
   
Loading...