JK, Hizi ni Ishara Mbaya Fanya Kitu

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Nchi yetu iko kwenye kipindi kigumu sana, pengine kuliko awamu zote zilizotangulia; kwa bahati mbaya ni katika kipindi cha awamu ya JK ambaye kwa bahati mbaya au nzuri (sijui nitumie ipi kati ya 'mbaya' au 'nzuri') ndiye Rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi mno (asilimia 20)! na ambaye kwake Wananchi tuliweka matumaini makubwa mno mimi ni mmoja wao! Si kutokana na ahadi kedekede zilizotolewa na Mh. JK kupitia Ilani ya Uchaguzi na zile ambazo alizozitoa kwenye Kampeni za uchaguzi ambazo nyingi mno hazijatekelezeka na pengine zisitekelezeka kabisa kwa kuzingatia muda uliobaki kabla ya Uchaguzi.

Ni kipindi hiki cha awamu ya JK ndipo ambapo tumeshuhudia mfumuko mkubwa wa bei na uchumi kulegelega pamoja na majivuno ya kuongezeka kwa makusanyo ya kodi!

Ni kipindi hiki cha awamu ya JK ndipo ambapo kumeripotiwa UFISADI mkubwa sana na wizi wa hali ya juu wa Raslimali za Taifa letu tukufu na lililopendelewa na Mungu Menye enzi! Si kwamba UFISADI huo umefanyika katika kipendi chake, la hasha ila ni kwa kuwa tuliamini kuwa kwa ajili ya upaya wake, Ari, Yake, na Nguvu yake mpya alikuwa na nafasi ya kulipa fadhila ya kura zetu nyingi tulizompa kwa vitendo. Ukimya wake ni mwanya wa kutosha kwa Mafisadi waliopo kuendeleza UFISAFI wao na ni Limbuko kwa Mafisadi wajao maana hawana sababu ya kuhofu!

Ni kipindi ambacho tunategemea uvunjaji wa Mikataba ya kinyonyaji ambayo MAFISADI waliingia kwa manufaa yao binafsi kwa "maslahi" ya Taifa.

Mh.JK, mwenye macho haambiwi tazama, ukweli ni kuwa Watanzania tumechoka sana na KUFISADISHWA kweny kila eneo na tunasubiri hatua zako.

Yanayotokea sasa ni Ishara ya nje ya kuchoshwa; Migomo ya Waalimu na Madaktari, Maandamano ya Wanafunzi (wapiga kura wa leo na kesho) bila sababu ya maana ni kiashirio tu maana wanahoji yaleyale.: Iweje gharama za maisha zipande kwa wananchi wengi ilhali wachache maisha yao yazidi kuwa bora?

Ni vema akumbuke kauli mbiu zake-MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA NA TANZANIA YENYE NEEMA INAWEZEKANA

Watanzania tunaamini inawezekana ikiwa JK ameamua maana nchi yetu imejaa asali na Maziwa ndo maana waporaji wanazidi kuongezeka kila kukicha; kama kungekuwa hakuna Maziwa na Asali za kupora wasiongkuja wala kuongezeka.

Ni kwa kuzingatia hotuba yako ya kwanza uliyoitoa Bungeni mara baada ya kuchaguliwa

Ni vizuri Mh. achukue hatua, Watanzania tumechoka kuona nchi yetu ikiibiwa na Watanzania tunaendlea kuwa maskini.
 
mafisadi wanafahamika na ni wanaCCM wenye vyeo ndani ya chama na serikali. JK angeanzia huku. 2010 si mbali ndugu yangu JK. utawaeleza nini watanzania uliowaahidi maisha bora? kila kukicha bora ya jana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom