JK: Hawajui una mamlaka gani - HONGERA!! - BARUA YA WAZI WA JK

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,458
Hongera JK kwa uamuzi wako mgumu, mimi binasi sikutengemea kama ungetamka mambo hayo magumu kwa mustakabali wa taifa letu kwa sababu kuu kwamba katiba haikuwa ilani kuu ya chama chako.

Lakini kwa kusoma kwako alama za nyakati umegundua kwamba watanzania waliokupenda sana mwaka 2005 wakati unaingia madarakani ndiyo hao hao wamekugeuka na kukuona wewe ni msanii tena msaani wa kutupwa, ila ukawadhihirisha kwamba wewe ni moto wa kuotea mbali baada ya kuja na kete mpya ka KATIBA mpya! hilo umeamua na kulitamka rasmi kwamba KATIBA MPYA ndiyo key objective yako kwa miaka hii mitano ya ungozi wako.

Mtani wangu ( Mimi mnyamwezi). Wakati wa kampeni umehangaika sana, ni ukweli kwamba ilifika hatua ukawa unaona utawala wako unapotea, nakumbuka ukaitisha kikao maalum cha Kamati kuu, nafikiri hilo lilikuwa kuwahabarisha kwamba jamani mambo ni magumu, wengine wakasema watakusadidia na wengine hawakuonyesha msimamo wao moja kwa moja.

Mtani ukaona lazima majeshi yasonge mbele mama na mtoto wakaze buti, kwa kweli walifanya kazi nzuri sana hata kama hawakutumia sheria lakini walihakiliksha mkuu unarudi madarakani kwa kutumia katiba hii hii tuliyonayo, mimi nakupongeza kwa ushindi wako sababu katiba tuliyonayo ndiyo iliyokurudisha wewe madarakani.

Ulivyomaliza kuapa tu pale uwanja wa taifa , mimi mwenye akili nikajua sasa mtani watamkoma, hasira zake za kususiwa kampeni hizi, ukizingatia kampeni ilikuwa ngumu mno wacha nione. Ni Juzi tu baada ya wateule wako ( Kombani na Werema) kubwabwajaa kuhusu katiba wewe umesema " KATIBA MPYA NI MUDA MUAFAKA KWA WATANZANIA:" hapa nijajua haya ndiyo majibu na mengine yanafuatia.

Binafsi huwa sisikilizi hotuba zako, asubuhi mamsapu kwa kwanza kusoma magazeti ananihabarisha - mtani wako kasema katiba mpya RUKSA " sikunywa chai ikabididi nisome magazeti yote kwanza, kwa kweli hiyo ilikuwa breaking News kwangu na hapo hapo nikachukua akiba yangu " haya wote twendeni out" ikawa new year yangu nzuri sana.

Mtani, Ulipotamka tu KATIBA MPYA basi na wambeya nao hawakuwa mbali, baada tu ya masaa machache Makamba naye akaibuka toka shimoni ( Mtani wangu mwengine) eti Tamko lako ndilo tamko la CCM ha hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji, mmhh sikubisha maana ni kweli mtani una mamlaka makubwa sana sababu wewe ndiyo Mwenyekiti wao, ila akaenda bali na kusema CCM ndiyo iliyotamka na si serikali, Kombani na Mwenzake Werema walikurupuka au lugha rahisi kuchemka hapo ndipo aliponiacha mimi salenda.

Wanachama wako wa CCM nao wakasema umepata mamlaka gani? toka kwa nani? na mimi naungana nao kwamba hivi mtani kwenye ilani yako kulikuwa na kitu kinaitwa katiba mpya? mmhh hapa mtani unanikumbusha kwenye vitabu vitakatifu, Yesu alishawahi kuuliwa na wakuu wa makuhani "Haya mamlaka umeyapata wapi?" sitaingia ndani sana ila wachambuzi wa mambo watanielewa kwamba nina maana gani.

Mimi kijana wa kinyamwezi nacheka tu kuwacheka haswa hawa wana CCM senior members eti wanahoji kwamba hoja yako haikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 umeichakachua toka CHADEMA, Pili hujaipeleka hata kwenye kwenye baraza la mawaziri kupata baraka na tatu hata kwenye vikao vya juu kabisa vya chama chako yaani ( Kamati Kuu ya CCM ) hujaifikisha, mtani haya hata mimi sasa naafiki kabisa ni ya kweli, ningependa kupata maelezo.

Anyway, sisi wenye akili zetu tunaelewa kuwa huhitaji balaza la mawaziri wala eti kamati kuu ya CCM kutamka kwamba " WATANZANIA WANATAKA KATIBA MPYA" una mamlaka yote ki katiba na hakuna mtu wala chombo chochote chenye mamlaka ya kuhoji kauli yako hii.

Watu bado hawajui kwamba kesho asubuhi unaweza kusema haya yafuataya kama ukitaka kwamba:-
1. DOWANS HALIPWI NA MJADALA UMEFUNGWA
2. HAKUNA BEI YA UMEME KUPANDA na mengineyo mengi tu ambayo watanzania hawana majibu naya kama hili ya RADA na Yale ya habari ya DR. Hosea wa Takukuru na yule kachero wa kimarekani.

Hongera Rais ( Rais kwa mujibu wa katiba yetu) tunakuamini na wewe ndiye utatuongoza kufikia yale tuliyokuwa tumeyapangilia kwenye fikra zetu. Binafsi nina imani na wewe tena kupita kiasi, kitendo cha kuwatosa hao wanajiita eti KAMATI KUU YA CHAMA CHAKO na wengine wanaojiita eti BALAZA LA MAWAZIRI wanaohoji wapi na lini ulipewa MAMLAKA YA KUTAMKA KWAMBA WATANZANIA WANATAKA KATIBA MPYA?

Hao hao kwenye kampeni ndiyo walikuachia mzigo mkubwa ukabaki unakukuruka wewe, mama salma na dogo Liz, Makamba na Kinana, eti ndiyo hao hao wanataka eti uwashirikishe kwenye maamuzi yako, NO, WATOSE MTANI.

Natoa pongezi zangu za dhati kwako, kwa mama na dogo lizi kwa kazi kubwa wakati wa kampeni, yaani ushindi wenu mliupata dk ya 90, ingawa sina uhakika kama sheria na kanuni zilifuatwa - sikuwapo uwanjani - lakini kwa sisi tunaojua soka ushindi huwa HAUHOJIWI. hata kama goli ni la mkono mtani huwa linasimama - mtani si unakumbuka ile game ya Ghana kombe la dunia yule jamaa aliyedaka mpira ukienda wavuni?

KATIBA MPYA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!! ------ HONGERA MTANI WANGU nina jogoo nakuletea hapo mjengoni mle na mama, ila sina uhakika kama nitaruhusiwa kupita hapo getini kwako.

Angalizo: Baba wa taifa pia alitamka wazi kwamba Kwa katiba hii tuliyonayo ukipata rais ambaye ni mbinafsi ( Fisadi) ni hatari sana sababu inampa mamlaka makubwa mno.
 
Mkuu,

Hata hiyo kauli aliyotoa inaacha masuali mengi mkuu kuliko kutolea majibu.
Amesema ataunda kamati,jopo...
Kama wewe umefurahi na kauli, sawa mkuu,
Sasa tusubiri atoe kauli nyengine lini ataunda hiyo kamati...itafanya kazi kwa muda gani...hadidu rejea za kamati....inawajibika kwa nani....
na nani ana maamuzi za mwisho juu ya mapendekezo ya kamati..

Mkuu, CCM na serikali zake kwa kauli tu, pitia historia wameshatoa kauli nyingi, na tume au kamati nyingi zimeshaundwa na kumaliza kazi zake..jee mapendelezo yao yalifanyiwa kazi?
 
Nonda, Kinachonifanya nifurahi ni kwamba hatukutegemea JK atafikia uamuzi hata huo tu wa kusema kwamba katiba mpya ni muda muafaka sababu hata kwenye ilani ya chama chake kilichomuweka madarakani hakuna hata msitari mmoja uliosema kuhusu katiba mpya.

Kwa hiyo binafsi nampongeza kwa hatua hiyo, angeweza kabisa kusema katiba mpya NO, sidhani kama kungekuwa na chombo chochote cha kumpinga, sana sana tungeandamana na kupigwa madomu na watanzania walivyo waoga basi wangemwachia mungu tu.

Hayo ya tume itaundwaje mimi sitayaongelea sana, ila hiki kitendo cha kutamka KATIBA MPYA YES mimi ndipo nampompongeza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom