NgomaNzito
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 559
- 26
WANANCHI wa Wilaya ya Njombe, Mkoa wa Iringa, wameeleza kukerwa kwao na kauli ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba hakutembea na fuko la fedha za kuwagawia.
Wakielezea kuhusu kauli hiyo ya Rais Kikwete, wananchi wa kada mbalimbali wilayani humo walisema wamechukizwa na kauli hiyo, wakidai kuwa ni ya kuwadhalilisha.
Kwa kweli tumesikitishwa mno na kauli ya rais wetu. Hii ni dharau na udhalilishaji dhidi yetu, sisi si ombaomba, tunafanya kazi zetu kwa kujitegemea. Tumetumia rasilimali na nguvu zetu kujenga madarasa ya shule zetu, lakini hatukukamilisha kazi kwa sababu uwezo wetu ulifikia kikomo, hivyo tulimwomba msaada ili tukamilishe miradi yetu.
Isitoshe hatukumwomba msaada wa fedha kutoka mfukoni mwake kama Kikwete binafsi, tumemwomba msaada akiwa rais wa nchi, ambaye tunajua ana fedha za umma za kusapoti nguvu za wananchi katika miradi ya maendeleo.
Na hili si jambo jipya, marais waliomtangulia walikuwa wakifanya hivyo, na hata yeye amekuwa akichangia fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali anapokuwa katika ziara za kikazi kama hii, alisema mkazi wa Kijiji cha Imalinyi aliyekataa kutaja jina lake, kwa sababu ya kukwepa usumbufu.
Mwananchi mwingine kutoka Kijiji cha Ilembula, wilayani humo, ambaye pia hakutaka kutaja jina lake kwa sababu za kiusalama, alikuwa na maoni haya: Kama rais hataki kusikiliza shida zetu, ni bora asingekuja kabisa, hakuna maana ya ziara yake kwetu. Anatuona sisi ombaomba, mbona yeye amekuwa akisafiri mara kwa mara nje ya nchi kuomba misaada - Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Canada, Denmark, Sweden, Uholanzi n.k.
Hapa Presidaa alisema,
Hivi mmejipanga kunieleza matatizo yenu kwa lengo la kunichomoa fedha? Mbunge wewe ndiye umewapanga watu wako waniombe fedha? Mmekosea sana, mimi sijatembea na fuko la fedha za kuwagawia.
Elezeni matatizo makubwa ambayo yameshindikana kutatuliwa na uongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa. Nielezeni matatizo ya mbolea, maji, barabara na afya. Mambo ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari na msingi yanaweza kutatuliwa na uongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa, alisema Rais Kikwete huku akionekana dhahiri kukasirika.
Hapa KWeli JK amesahau kuwa aliwaahidi Wakati alipokuwa anaomba "Kula" kila kitu alisema tutafanya meengine wala hayakuwepo kwenye ilani ya chama chake lakini sasa ameshapata anawapa majibu ya mkato.ama kweli alishiba hamjui mwenye Njaa.