JK Hatembei na Fuko La Fedha

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
WANANCHI wa Wilaya ya Njombe, Mkoa wa Iringa, wameeleza kukerwa kwao na kauli ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba hakutembea na fuko la fedha za kuwagawia.

Wakielezea kuhusu kauli hiyo ya Rais Kikwete, wananchi wa kada mbalimbali wilayani humo walisema wamechukizwa na kauli hiyo, wakidai kuwa ni ya kuwadhalilisha.
“Kwa kweli tumesikitishwa mno na kauli ya rais wetu. Hii ni dharau na udhalilishaji dhidi yetu, sisi si ombaomba, tunafanya kazi zetu kwa kujitegemea. Tumetumia rasilimali na nguvu zetu kujenga madarasa ya shule zetu, lakini hatukukamilisha kazi kwa sababu uwezo wetu ulifikia kikomo, hivyo tulimwomba msaada ili tukamilishe miradi yetu.
“Isitoshe hatukumwomba msaada wa fedha kutoka mfukoni mwake kama Kikwete binafsi, tumemwomba msaada akiwa rais wa nchi, ambaye tunajua ana fedha za umma za kusapoti nguvu za wananchi katika miradi ya maendeleo.
“Na hili si jambo jipya, marais waliomtangulia walikuwa wakifanya hivyo, na hata yeye amekuwa akichangia fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali anapokuwa katika ziara za kikazi kama hii,” alisema mkazi wa Kijiji cha Imalinyi aliyekataa kutaja jina lake, kwa sababu ya kukwepa usumbufu.
Mwananchi mwingine kutoka Kijiji cha Ilembula, wilayani humo, ambaye pia hakutaka kutaja jina lake kwa sababu za kiusalama, alikuwa na maoni haya: “Kama rais hataki kusikiliza shida zetu, ni bora asingekuja kabisa, hakuna maana ya ziara yake kwetu. Anatuona sisi ombaomba, mbona yeye amekuwa akisafiri mara kwa mara nje ya nchi kuomba misaada - Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Canada, Denmark, Sweden, Uholanzi n.k.

Hapa Presidaa alisema,


“Hivi mmejipanga kunieleza matatizo yenu kwa lengo la kunichomoa fedha? Mbunge wewe ndiye umewapanga watu wako waniombe fedha? Mmekosea sana, mimi sijatembea na fuko la fedha za kuwagawia.
“Elezeni matatizo makubwa ambayo yameshindikana kutatuliwa na uongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa. “Nielezeni matatizo ya mbolea, maji, barabara na afya. Mambo ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari na msingi yanaweza kutatuliwa na uongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa,” alisema Rais Kikwete huku akionekana dhahiri kukasirika.

Hapa KWeli JK amesahau kuwa aliwaahidi Wakati alipokuwa anaomba "Kula" kila kitu alisema tutafanya meengine wala hayakuwepo kwenye ilani ya chama chake lakini sasa ameshapata anawapa majibu ya mkato.ama kweli alishiba hamjui mwenye Njaa.:eek:
 
Duh! kweli hapo mkuu wa kaya alichemka. Sasa kama matatizo yote aliyoyaorodhesha ambayo siku zote ndiyo kilio cha wananchi wa hali ya chini yanatakiwa yamalizwe na uongozi wa wilaya au mkoa, basi yeye alitaka aelezwe kero zipi ambazo ndiyo za saizi yake?

Na ni kero zipi basi za saizi yake ambazo ameshaweza kuzitatua katika kipindi chote alichokaa madarakani?

Hapa kweli kazi tunayo!
 
Hivi kweli alisema haya? basi huyu bwana sio tu kwamba amechoka, lakini nafikiri pia anazeeka na anazeeka vibaya!
 
Jamani tatizo hapa ni huyo mbunge wao yono, huyu yono ndie Yono action mart, anaemiliki yale malandrova ya kuvuta magari! akikuta hiace imepaki vibaya wala hagusi! egesha benz uone! huyu aliwadanganya wananchi kuwa yeye ni kibopa atafanya kilakitu.

Ni yono yuleyule aliyepewa pande na kandoro la kukata mishahara kwa nguvu kuchangia ujenzi wa sekondari dar, nusura wafanyakazi wamtoe kamasi.

Kwa ambao hamjakaa vijijini mtalaumu, ila hizi shule kata zimefanywa mashamba ya watu, ukifika tu kijijini hata kama umeenda msibani utaambiwa uchangie ujenzi!

Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hutoa mabati nondo cement na mbao. wananchi hutakiwa kusomba mchanga na mawe tu, ambapo vijijini mawe yanapatikana bure, mchanga husombwa kwa kichwa na akinamama.

Sasa wanaposema nguvu zimaisha inamaana walikuwa wagonjwa au walikuwa na njaa!

Mkuu alitegemea aulizwe habari za epa, umeme na maji, sio kuambiwa hawana nguvu za kubeba mawe, sasa walitaka abebe yeye mabegani?

Mbona tarime hawachangishwi hela na shule zinajengwa kama kawaida, waende wakajifunze huko sio kumlalamikia mkuu wa kaya.
 
Kwa ambao hamjakaa vijijini mtalaumu, ila hizi shule kata zimefanywa mashamba ya watu, ukifika tu kijijini hata kama umeenda msibani utaambiwa uchangie ujenzi!

Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hutoa mabati nondo cement na mbao. wananchi hutakiwa kusomba mchanga na mawe tu, ambapo vijijini mawe yanapatikana bure, mchanga husombwa kwa kichwa na akinamama.

Sasa wanaposema nguvu zimaisha inamaana walikuwa wagonjwa au walikuwa na njaa!

Mkuu alitegemea aulizwe habari za epa, umeme na maji, sio kuambiwa hawana nguvu za kubeba mawe, sasa walitaka abebe yeye mabegani?

Mbona tarime hawachangishwi hela na shule zinajengwa kama kawaida, waende wakajifunze huko sio kumlalamikia mkuu wa kaya.
 
Ni sawa na aliyekuwa waziri wa maji enzi za nyuma alipowaambia wanafunzi wa Same Secondary school kuwa hakwenda na maji mgongoni.
Na neno hilo alilitowa mara baada ya wanafunzi hao kufurahia ujio wake pale shuleni kwani tatizo la maji lilikuwa sugu sana na nadhani bado ni sugu.
Tulukuwa tukigombea maji na wafungwa na kufanya kazi za kitumwa badala ya kusoma.
Sasa matokeo yake ndiyo hayo a kuwa na viongozi wasiojali.
Ni kweli kabisa sitokaa niisahahu hiyo siku...Kwani mimi nikiwa kama kijana mdogo sana wa miaka takriban 14...Nilidhtushwa na kauli hiyo kutoka kwa waziri mwenewe wa maji kwani lilishangazwa kuwa ni kwa kiasi gani serikali haiwajali wananchi wake.
Na nilipotembelea bongo 2006 maeneo hayo bado ni makame sana!
Shule yenyewe ilikuwa na mabafu na vyoo vya kisasa lakini zimepigwa kufuli na watu huoga kwenye kituo cha treni ama hata nje a bweni nk.
ani serikali a ccm ilishanikatisha tamaa kitambo sana na sina matumaini nayo tena.
 
Wananchi sasa ndo waelewe kuwa madarakani yupo mtu ambaye si sahihi kukaa pale, kauli kama hizi wengi najua tumezizoea, fikiria kauli mbalimbali zilizowahi kutolewa na tuliowaamini madaraka mbele ya umma. Fikiria kauli za Mramba, Mkulo na Malecela na wengine ambao unakumbuka kauli zao.

Kuna kitu kimoja mimi naamini tunapaswa kujifunza sana, kwa wenzetu hata makirani zetu tu hapo kaskazini, kauli ya kiongozi anayoitoa wakati wowote kuhusu umma huchukuliwa kwa uzito mkubwa. Watawala wetu akiwemo kikwete waliahidi wenyewe kabisa kuwa watawasaidia wananchi na kwamba maisha bora yanawezekana lakini nadhani hizi kauli ndizo walizokuwa wanamaanisha wakati wanaomba kura kwa umma wa watanzania. 'wapigaura' wao hawapaswi kulaumu kwani sasa ni zamu ya umma wote kujipanga na kuwafutilia mbali.Mabadiliko huanzia kijijini, mjini huja vitendo
 
Tunavuna tulichopanda, eti huyo muungwana ndiye chaguo la mungu!

Kaangalieni wilaya ambayo amekuwa mbunge miaka na miaka, hakuna la maana, tulitegemea kweli ailetee TZ maendeleo?

Jamaa hata ukimwangalia kwa mbali, unamwona ni msanii tu!
 
Mdau (Mtanzania) nimependa sana ulichoandika katika post yako ya 3208. Huyu hana jipya na kwa kuwa uongozi umemshinda anadhani kutukana ni tiba. hajatulia
Tukishindwa leo, lini!
 
Si alijifanya kugawa mabilioni na akadai ni yake. Sasa wananchi wantaka kamchango kake tena hata anakasirika. Anyway, bora wananchi wanaanza kujua ni jinsi gani hatuna kiongozi.
 
Kama tunakumbuka hapa JF tumeandika sana kuhusu Presidaa tuliyenaye sasa majibu kama haya wananchi wa vijijini unapowaambia kuwa huna fuko la fedha na wao wanasikia vigogo wanagawana fedha za EPA na Dowans huko Benki kuu wanategemea watapata unafuu wa michango lakini ziara za Mh. zina majibu ya namna hii kweli wanachoka labda tusubiri ahadi nyingine 2010 zisizotekelezeka

Time will Tell
 
Huyu ndiye mtu aliyekaa miaka kumi MOFA, diplomacy zero kabisa, inspirational language zero kabisa.Hata kama alikuwa na point, delivery yake zero kabisa, empathy zero kabisa.

This is the stuff that fuels revolutions.
 
..........“Hivi mmejipanga kunieleza matatizo yenu kwa lengo la kunichomoa fedha? Mbunge wewe ndiye umewapanga watu wako waniombe fedha? Mmekosea sana, mimi sijatembea na fuko la fedha za kuwagawia.
“Elezeni matatizo makubwa ambayo yameshindikana kutatuliwa na uongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa. “Nielezeni matatizo ya mbolea, maji, barabara na afya. Mambo ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari na msingi yanaweza kutatuliwa na uongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa,” alisema Rais Kikwete huku akionekana dhahiri kukasirika............

.......it is a very bad attitude........
 
Naona Mbunge nae aliamua kumtolea uvivu Mh Rais!


--------------------------------

Akizungumzia kauli ya Rais Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Njombe – Magharibi, Yono Stanley Kevela, ambaye alituhumiwa hadharani na Rais Kikwete kuwa alikuwa amewaandaa viongozi wa vijiji kumwomba fedha, alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa Rais Kikwete alikuwa amepotoshwa na baadhi ya wasaidizi wake mkoani Iringa.

“Si kweli kabisa, wale ni viongozi wa watu hivyo wanayajua matatizo ya watu wao. “Hawawezi kupangwa na mbunge wazungumze mambo yasiyokuwepo, naamini rais alipotoshwa na wasaidizi wake mkoani na wilayani.

“Halafu si kosa kwa wananchi kumwomba rais msaada katika miradi ambayo nguvu zao zimefikia kikomo, ni wajibu wake kuwasaidia. Mbona mimi nimekuwa nikichangia miradi ya maendeleo ya wananchi kwa kutumia fedha zangu binafsi, na hata wakati wa maandalizi ya ziara yake hii katika wilaya yetu nimechangia fedha zangu zaidi ya shilingi milioni moja, lakini sijalalamika,” alisema Kevela.
 
...kwani mh. Rais angepitisha harambee ya chap chap ingekuwaje hapo? ...anyway, kama watakumbuka, wamsubirie 2010 akienda kuomba kura zao!
 
Ile siasa yetu ya kujitegemea tumeicha wapi? Au ilikuwa ni wimbo tu, rais anaenda nje kuomba na wananchi wanamuomba rais!
 
Mwanakijiji,

..yaani Raisi ameshindwa kuzungumza na wananchi kwa njia za kiungwana anaamua kung'aka kwamba hatembei na fuko la fedha.

..vilevile kuna matukio mengi tu ambapo imetangazwa kwamba Raisi amechangia kiasi fulani cha fedha. kuna hata kipindi hapa tuliambiwa Mkuu wa Majeshi amechangia fedha mamilioni jimboni kwa Raisi.

..badala ya ukweli kuelezwa kwamba ni SERIKALI ndiyo imechangia wanasema Raisi/Waziri Mkuu/Mkuu wa Majeshi. hiyo ndiyo imezua dhana na mazoea kwamba wananchi wanaweza kumchomoa fedha Raisi.

NB:

..anayedekezwa hapa ni Raisi Kikwete. kauli hiyo ingetolewa na Mramba/Sumaye/Malecela ungesikia jinsi ambavyo wangepigwa vita
 
Back
Top Bottom