JK hana kosa hata moja, wenye kosa wakubwa ni hawa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK hana kosa hata moja, wenye kosa wakubwa ni hawa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kongosho, Mar 23, 2011.

 1. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu utendaji wa JK kama kiongozi mkuu na serikali yak. Lakini kila ninapomtizama kiongozi huyu sioni hata kosa lake moja katika utendaji wake. Historia ya uongozi wake tangu anaanza hajawahi kuwa na tatizo hata moja. Shida kubwa naiona kwa tuiomweka madarakani kwani historia ya JK inajieleza vizuri kabisa hajawahi hata fanikisha kununua sindano ya kushonea kwa maslahi ya taifa. Na wakati wa kampeni ya 2005 nilikuwa almost natoka machozi nikiona watu wanavyompigia kampeni kwa matumaini makubwa kabisa usoni mwao pale chuo kikuu, nikawa najiuliza hawa watu wana matumaini ya makubwa sana kwa historia ipi. Historia ya JK ilimweka wazi kabisa lakini bado akachaguliwa, mie naona watanzania bado tunapaswa kulaumiwa kwa kumweka mtu huyu madarakani.
  Kinachosikitisha zaidi ni kuwa, je hatuwezi kujifunza kutoka makosa yetu? maana 2010 tumefanya kosa hilo hilo.

  Anyway, we made the same mistake 2 times, lakini maisha lazima yaendelee. Kwa hiyo tuna wajibu wa ku-support serikali pale inapofanya kitu kizuri hata kimoja hata kama ni kidogo kama punje ya ngano at the same time tunawajibu wa ku-demand haki zetu za msingi maana tukikaa kimya mkulu anweza kwenda vacation boraboya miaka 2.
  Wenye kosa ni waliompitisha kugombea, na sie tuliomwidhinisha kukaa hapo..
   
 2. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa lakini bado watanzania wengi hawalioni hilo. Wanadhani JK ni kiongozi mwenye uwezo lakini kaamua kuwasahau wananchi wakati ukweli ni kwamba hawezi kabisa na hajui hata namna ya kuwafanya watumishi wa umma watimize wajibu wao wa kila siku.
   
 3. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye RED, maswali mawili

  (1) "Sie"......we na nani? manake kama ni wapiga kura, kura hakupigiwa yeye, walipigiwa wengine akiwemo padre slaa, ila kura zikachakachuliwa akapewa yeye!

  (2) "tuliyemuidhinisha"........hapa una maana gani? kumchagua kwa kura au kumruhusu awe rais mkiwa kama TISS na Kamati ya maadili ya CCM? au mkiwa kama MAFISADI, mliyekubali kumpa support financially wakati wa kampeni zake, huku mkijua kuwa he will pay you back hansomely??

  (3) "Kukaa hapo"...............hapa unamaanisha kukaa wapi?? kwenye kiti cha urais?? au kwenye kaa la moto alilolikalia sasa ivi?? au kukaa kwenye kuti kavu atakalo kalia siku zijazo ambalo litamuangusha avunjike mgongo na uwe mwisho wake???
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Angalia Heading yako mzee.
  "Jk hana kosa hata moja"??
  Hata yeye mwenyewe ukimuuliza atakwambia anayo makosa yake hata kama ni machache lakini anayo.
   
 5. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,896
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, wenye makosa ni wananchi waliomchagua. Maana walijua kuwa hawezi kuongoza lakini wakaendelea kumchagua tena.
   
 6. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  tatizo jengine huyu JK anaona anapiga mzigo kinoma, ni bora angesema kwamba uwezo wake ndio umeishia hapo! wote ni wanadamu Mungu hajupata uwezo wa kufanya kila kitu kwa ufanisi , tumuelewa na itakua mwanzo mzuri!
   
 7. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Binafsi naomba hali iwe ngumu kwa wale wasiona haja ya kuchagua watu kutoka chama kingine. Tena iwe ngumu zaidi hata mara kumi ili wazinduke. Kwa namna hii 2015 watu watabadilika la sivyo hakuna kitu vichwa vingi havifikiri sawa sawa.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi hoja yako ni kwamba JK ni mweupe zaidi ya pamba, chokaa na sufu ki-utawala sio?? Acha hizo janja za kutaka kumpimia joto kiaina huku kwa wananchi juu ya huyo shujaa wako!!!

  Kwa kuwa naamini kwamba asiye na kosa hata moja duniani bado kuzaliwa basi inaamaana kwamba JK bado yuko tumboni kwa mzazi wake hadi hivi sasa.
   
Loading...