JK: Fumba Macho Umeze Kiwembe kwa Faida ya CCM.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Fumba Macho Umeze Kiwembe kwa Faida ya CCM..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gagurito, Mar 22, 2011.

 1. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa wale waliopata kuangalia kipindi cha JE TUTAFIKA Channel ten kinachoongozwa na Mwanahabari, Kada mfu wa ccm ndugu Makwaiya wa Kuhenga nadhani hii habari sio ngeni kwao.. Kwa walemliopitwa basi ndio kazi yetu wanajf kujulishana.
  WanaJF ni kwamba ktk mazungumzo, mchangia mada mmoja amepasa kumuasa kwa kutoa Rai kwa mh. Mwenyekiti wa chama kufumba macho na kula kiwembe, akiwa na maana ya kutowafumbia watu macho wote wachafuao chama, kwan kwa kufanya hivyo itasaidia kukijenga chama chake na kukifanya kiwe na mvuto kwa wananchi kwan kwa hali ya sasa kimechafuka, kimechokwa na kipo taabani. kwa kuongezea ndugu makwaiya alisema, kwa sisiem kujijenga mh mwenyekiti wake anapaswa kuchukua nafasi ya DOCTA WA MENO PINDI ANG'OAPO JINO MWANAE coz hali inatisha na ufagio wa chuma ni mhm!
  Hivyo JK anapaswa kuja na suluhu ya matatizo haya!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sikio la kufa halisikii dawa!...CCM watabebwa na mbeleko gani wakabebeka?
  Ni gunia la misumari hilo!
   
 3. p

  plawala JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda wakifanya mabadiliko kama alivyoahidi mwenyekiti,aka kujivua gamba
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani JK hana muda wa kufikiria hayo na hata ule uwezo wa kufikiri hayo hana....mwambie mambo ya kula visheti na kahawa na kwenda kugida kombe kwa babu hapo ndo mtaelewana
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  bt tatizo la Ccm mpaka uvccm limefika, watoto wao duh! Watoto wanamalez ya hovyo sana!
   
 6. S

  Salimia JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huwa mnafuatilia maendeleo nchini kote au mnapiga soga tu?


  Kaya 87 zapata maji bure


  na Danson Kaijage, Dodoma  JUMLA ya kaya 87 zinazoishi kwenye mazingira magumu mjini Dodoma zimeunganishwa na huduma ya maji safi na salama bila malipo kwa gharama ya Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dodoma (DUWASA).
  Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Injinia Peter Mokiwa, alisema hayo juzi mjini hapa alipozungumza na Tanzania Daima kuhusu mpango wa mamlaka hiyo kuyasaidia makundi maalumu ili yapate huduma ya maji safi na salama.
  Katika maelezo yake, Injinia Mokiwa alisema mamlaka hiyo inahudumia kaya 87 kwa kuwapatia maji safi na salama ili kuwawezesha kupata maji ya kutosha kama walivyo wananchi wengine.
  Alisema kimsingi huduma hiyo ya bure inatolewa kwa kaya zenye maisha magumu ambazo hazina kipato cha kuunganisha maji na kulipia ankara za kila mwezi hata kama wanahitaji maji hayo.
  Kwa mujibu wa Injinia Mokiwa baada ya DUWASA kuliona tatizo hilo iliamua kufanya utaratibu wa kusambaza huduma hiyo bila gharama kwa kaya hizo ili nao waone furaha sawa na wengine.
  “Hawa ni Watanzania wenzetu, ni wananchi wenzetu, tatizo la kutokuwa na uwezo wa kifedha lisitufanye watu kuwekeana matabaka sisi wana DUWASA tuliliona tatizo hilo na kufanya utaratibu wa kuhakikisha tunawapatia huduma ya maji wana kaya ambao kipato chao ni cha chini kabisa.
  “Lakini pia na watu ambao ni walemavu wa viungo nao kwa sasa wanafurahia huduma za familia ya DUWASA kwa sababu tumewaunganisha na huduma zetu hivyo kaya zote zinazohudumiwa bila malipo na mamlaka yetu zipo 87,” alisema.
  Aliongeza kwamba utaratibu wa mamlaka hiyo kuwapatia maji bila gharama unalenga kuwaondoa watu hao katika unyanyapaa na kuwafanya kuwa karibu na jamii inayowazunguka kisha kujivunia kuwepo kwa vyanzo vya maji ambayo ni muhimu kwa matumizi ya binadamu na mifugo.
  Akitoa ufafanuzi zaidi alisema mpango wa mamlaka ni kuhakikisha kila kaya inayopatiwa maji bila malipo itatumia lita 100 kwa siku, sawa na dumu tano za lita 20.
  Kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Maji, Injinia Mokiwa alisema kwa sasa mamlaka inafanya mikakati ya kuhakikisha kuwa maji si tatizo tena japo kuna upungufu wa lita milioni 24 kila siku. Alisema kwa kawaida mji wa Dodoma unatakiwa kupata maji lita milioni 54 kwa siku lakini kwa sasa yanayopatikana ni lita milioni 30 kwa siku na kusababisha upungufu, jambo alilodai kuwa linatokana na ongezeko la watu na taasisi mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma.
   
 7. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Duuuhh.... Kwenye CAPITAL WORDS jamaa kumbe nae yumo,
  hata kule samunge kumbe alienda!:D:D
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kata tanzania zipo zaidi ya 6000, sa kupata maji kwa kata 87 sio story, naungana na wale washaurio serikali kufanya mabadiliko makubwa! Ccm ilipofika imefika pabaya, wanaitaji mabadiliko, tuwashauri juu gani wajirekebishe!
   
 9. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyu Makwaia wa Kuhenga huwa ni mtu wa udini sana, nimepoteza appetite naye siku nyingi! Anyway, hata saa mbovu huwa inasema ukweli mara 2 kwa siku, angalau namuunga mkono kwa hili la kiwembe, japokuwa Rais wetu ni sikio la kufa!
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  je nikweli ccm yaweza jirekebisha?
   
 11. S

  Songasonga Senior Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusilalamike tufanye kazi
   
 12. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hata ikirekebika, umeshasikia msukule uliorudishiwa uhai wake ukarudia hali yake ya kwanza kikamilifu?
   
 13. Chiwaso

  Chiwaso JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,560
  Likes Received: 1,732
  Trophy Points: 280
  BIG UP, anataka kukuza mambo yasiyo na mpango. Kwetu kaya zote zinapata maji ya mto bure, nini hizo 87 za DOM bwana.
   
 14. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hata wapate maji kila nyumba na kata zao 87 maisha yao bado magumu, na hzo kata sijui za wap? UDOM VYOO HAVIFANYIKAZI MAJI HAKUNA KABISA, HIZO KATA 87 SIJUI ZA WAP?!! CCM jirekebisheni.
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nawasiwasi mambo makubwa ya ajabu kutokea 2015 ktk chama hiki!
   
Loading...