JK: Elimu bure haiwezekani, ila kompyuta kwa kila mwanafunzi inawezekana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Elimu bure haiwezekani, ila kompyuta kwa kila mwanafunzi inawezekana

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Faru Kabula, Oct 15, 2010.

 1. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,631
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  JK amekuwa akiwabeza wapinzani wake kuwa wanatoa ahadi ya kutolewa elimu bure wakati haitekelezeki. Lakini ni JK huyo huyo ambaye siku si nyingi alisema atatoa computer (desktop) kwa kila mwanafunzi nchini na laptop kwa kila mwalimu. Nadhani amesahau kwamba alichoahidi ni kigumu kutekelezeka kuliko wanachoahidi wenzake sasa. Kuweka computer kutahitaji computer set yenyewe, kiti na meza kwa ajili ya kuwekea computer (bila kujali kama kila mwanafunzi wa sasa anakalia dawati au la!), miundombinu km vile umeme kwa ajili ya kuendesha computer (sina hakika km aliwauliza TANESCO umeme umeishia wapi), solar panel zenye Watts za kutosha (iwapo hawatatumia umeme wa TANESCO, na sina uhakika kama aliuliza power consumption ya CRT desktop pekee), mafundi wa kuzifunga, maintanance costs na walimu wa kuwaelekeza wanafunzi walau namna ya kuzitumia.
  Swali langu: Iwapo aliahidi computer + laptop, kwa nini awashangae wanaoahidi elimu bure? Kipi ni rahisi kutekelezeka, computer/laptop AU elimu bure?
  Gharama ya jumla ya matumizi ya computer/laptop per student/teacher haiwezi kumsomesha mwanafunzi mmoja mmoja wa sekondari na chenji zao zikabaki kwenda kuwachangia wale wachache wa elimu ya juu?

   
Loading...