JK dhaifu mwenye nchi kubwa hana ubavu wa kuwa sawa na HUGO CHAVESH mwenye nchi ndogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK dhaifu mwenye nchi kubwa hana ubavu wa kuwa sawa na HUGO CHAVESH mwenye nchi ndogo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Nov 27, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Rais Hugo Chaves wa Venezuela ameyashitua mataifa ya magharibi hasa nchi za Ulaya kwa kutangaza kuwa anaanza mpango wa kukusanya dhahabu yote ya nchi yake iliyokuwa inahifadhiwa katika mabenki mbali mbali katika nchi za Ulaya na Marekani. Rais huyo amechukua uamuzi huo baada ya uchumi wa mataifa hayo ya magharibi kuanza kuporomoka kwa kasi. Dhahabu ya nchi hiyo iliyo katika mabenki hayo inakadiliwa kuwa na uzito wa tani 100 zenye thamani ya dola za Kimarekani zaidi ya bilioni 10......CNN news.... Kwa nini watawala wetu wasiige misimamo ya watu kama akina HUGO CHAVESH. Naamini nchi hii inazo rasilimali na madini mengi kuliko nchi ndogo kama Venezuela. .ama kweli AFRIKA INAKWENDA KOMBO. Afrika sawa na mwembe wa bibi, kila mpita njia anapopoa tu.
   
 2. Biznocrats

  Biznocrats JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hugo ana malengo yake. Ameshaona jinsi Hosni Mubarak na Col Gadhafi walivyonyan'ganywa mali zao huko nje (asset freeze) baada ya serikali zao kupata msukosuko ya kisiasa. Nadhani ameona ahamishe mali zake zote mapema kabla mambo hayajawa mabaya. Unajua hawa wazungu watakusaidia hata kuiibia nchi yako ili upeleke mali kwao zikasaidie uchumi wao. Siku kibao kikibadilika utasikia wa me freeze asset za "Dictactor" fulani. Wakati hela zinakwenda huko hawakujua kwamba ni za Dictotor? Kwa nini wasizifreeze wakati ule bado yupo madarakani? Ama kweli dunia hii wasanii wako kila pembe ya dunia!
   
Loading...