JK chukua hatua kali dhidi ya huu uonevu wa makato ya mishahara ya walimu kwa ajili ya maabara

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
0
Tanzania kama nchi inayofuata utawala wa sheria,ikiwa wewe na rais wetu huu ubabe na ukandamizaji dhidi ya walimu hauvumiliki.Una nafasi kubwa ya kuwashughulihikia hawa watumishi wahuni hasa wakurugenzi wa Halmashauri waliojichukulia maamuzi ya kibabe ya kudhulumu walimu kwa kukata mishahara yao bila ya ridhaa yao.

Huu ni uhuni uliopitiliza.Hawa watendaji wanaichonganisha serikali na wananchi.Iweje walimu wawe wahanga wakudhulumiwa haki yao eti kisa ujenzi wa maabara ? Mbona watumishi wangine hawajakatwa mishahara yao kwa ajili ya maabara? Ukizingztia watumishi hao wana hali nzuri kiuchumi kwani kazi zao zinalipa zenye mishahara minono na marupurupu mengine mengi. Hawa watendaji mbona hawana utu na huruma kwa walimu ? Hawawaonei hata huruma walimu kwa maisha duni wanayoishi ? Badala yake wanazidi kuwakandamiza.

HIVI HAWA WATENDAJI WAHUNI WANAWAJENGEA KITU GANI WALIMU MIOYONI MWAO ? HIVI NCHI KUWA MWALIMU NDO TIKITI YA KUDHULUMIWA,KUONEWA,KUKANDAMIZWA NA KUDHARAULIWA ?

HAWA WATENDAJI WANAWACHUKULIAJE WALIMU ? MBONA KWA NINI HAWAKUKATA MISHAHARA YA WABUNGE NA WANASIASA WENGINE WENYE KIPATO KIKUBWA ? AU WANAWAONA WALIMU WANYONGE KATIKA NCHI HII ?

Kwa kuwa Watanzania wengi tunaimani na utendaji wako wa kazi,basi tunaamini utawachukulia hatua kali hawa watendaji kwa kuhujumu na kuonea walimu.Kwa nini walimu nchi hii hawathaminiwi?

HUU UMAFIA DHIDI YA HAWA WALIMU UKOMESHWE MARA MOJA,KWANI WALIMU WENGI WAMEKATA TAMAA YA MAISHA.........
KWA MANYANYASO HAYA DHIDI YA WALIMU KWELI ELIMU NCHI HII ITAIMARIKA ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom