Jk bado anaendekeza wanamtandao, sahau maendeleo nchi hii hadi aondoke

gotolove

Member
Apr 30, 2012
20
5
Baada ya kusemwa sana katika mabaraza mawili aliyowahi kuyavunja, nilitetegemea jk ataacha kudili na kundi kubwa lililofanya kampeni chafu za kumwingiza madarakani maarufu kama wanamtandao. Lakini inaonyesha tabia hii ni sugu kwake na imejizihirisha katika baraza hili la jana. Jk tena amemteua amos makala kuwa naibu waziri. Amos ni mpiga tarumbeta wa bendi ya vijana jazi inayomilikiwa na umoja wa vijana. Bendi yenyewe inaelekea kufa mikononi mwa shigela.

Amos makala ni mwanamtandao mkubwa. Naona alikuwa nje akiomba mungu siku yoyote baraza livunjwe aingie ndani kulipwa fadhila alizomfanyia jk hadi akaingia ikulu. Ni makala huyu akitumia ofisi ya umoja wa vijana wakati huo alikuwa kaimu katibu mkuu alikuwa akikodineti mambo mbalimbali miongoni mwa wanaumoja wa vijana zikiwemo fitina zote.

Huyu na emanueli nchimbi wanajua fitina zote zilizofanyika ndani ya umoja wa vijana hadi kupata kundi kubwa la kumwezesha jk kuwa mgombea wa ccm kwenye kinyang'anyiro cha urais. Makala, nchimbi na francis isack waliwahujumu wenzao kumpigia debe jk. Leo jk amempa unaibu kama fadhila.

Jk alipasa kujiuliza kwanza makala amepata wapi hela za kununua kompyuta na kuzigawa kwenye mashule kule mvomero? Makala amepata wapi hela ya kumng'olea murad kule mvomero kama si wizi akiwa kaimu katibu wa umoja wa vijana na baadae mhasibu mkuu wa ccm kabla hajang'olewa? Kuna msafi kweli hapo au ndio toa galasa ingiza galasa? Kuna maendeleo kweli hapo?
 
WATANZANIA BWANA! Katika hali ya kawaida kabisa haiwezekani RAIS akafanya kazi na watu wote asio wafahamu kwa namna moja au nyingine.huo ndio ukweli.Hata wewe ukiwa kiongozi utateua watu unao wafahamu na unaimani kuwa watakusaidia kuongoza.wapo watakao weza na wengine watashindwa.hata mitume hawakuwa na uwezo unaolingana.Kama MH Makala ameaminiwa na wapiga kura wake,na mheshiwa RAIS anamfahamu kiutendaji kwanini asimteue? MHIMU APEWE NAFASI AFANYE KAZI TUONE.
 
Amemwamini akamteua. Hayo we ndo unayaona kama maajabu lakini kwa Jk aka!
 
Jk alipasa kujiuliza kwanza makala amepata wapi hela za kununua kompyuta na kuzigawa kwenye mashule kule mvomero? Makala amepata wapi hela ya kumng'olea murad kule mvomero kama si wizi akiwa kaimu katibu wa umoja wa vijana na baadae mhasibu mkuu wa ccm kabla hajang'olewa? Kuna msafi kweli hapo au ndio toa galasa ingiza galasa? Kuna maendeleo kweli hapo?

mkuu ndani ya chama cha CCM haya mambo ya amepata wapi hawajiulizi kwani wanajua wote wanafanya hivi..jk yeye mwenyewe angejiuliza pesa za kampezi au za kutengenezea mabango alizitoa wapi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom