JK azuia uvuvi ziwa victoria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK azuia uvuvi ziwa victoria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Apr 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  *Amri hiyo itadumu kwa miezi mitatu

  [​IMG]

  RAIS Jakaya Kikwete amepiga marufuku uvuvi katika Ziwa Victoria kwa siku 90.

  Amesema uamuzi huo unalenga kuhakikisha kuwa samaki wanaongezeka katika ziwa hilo kubwa kuliko yote katika Afrika. Tanzania inamiliki asilimia zaidi ya 50 ya ziwa hilo. “Lazima mfanye patrol (doria) katika Ziwa Victoria, kama suala ni la mafuta ya boti ndiyo yanawakwamisha tuambieni ni kiasi gani na sisi tutawapa. “Wazuieni watu wasivue kwa siku 90 ili samaki waongezeke maana samaki wamepotea pale ziwani kwa kuwa tulifanya over fishing (uvuvi wa kupindukia),” alisema.

  Rais alitoa agizo hilo alipotembelea na kusomewa taarifa ya shughuli za Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, jijini Dar es Salaam, jana.

  Kuhusu mifugo, aliiagiza Wizara ifanye mapinduzi kwa kutenga maeneo maalumu ya malisho kwa ajili ya kupunguza uchungaji wa kuhama hama.
  Alisema hatua hiyo itasaidia kuzipa soko la uhakika nyama za mifugo inayonenepeshwa katika malisho hayo.
  “Sekta ya ufugaji na uvuvi ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi yetu na katika kupambana na umasikini. Pamoja na kwamba tuna fursa hiyo kwa kuwa na mifugo mingi, lakini shughuli za sekta hiyo hazina tija na matokeo yake wavuvi na wafugaji wanazidi kuwa masikini.

  “Kutokana na hali hiyo, lazima tufanye mageuzi na safari yetu ya mapinduzi hayo lazima ianze sasa hivi kwa kuboresha aina ya mifugo yetu ambayo itatuletea maziwa mengi na nyama nyingi ambazo zitakuwa na soko la uhakika katika nchi za Kiarabu na kwingineko.
  “Kila siku ng’ombe anaongezeka uzito wa kilo mbili kama ukiwatengea eneo maalumu la malisho yao, lakini kama wakiwa wanahama hama kila siku maana yake uzito wao nao unapungua na wakiendelea kuhama matokeo yake watakosa eneo la malisho,” alisema Rais Kikwete.

  Alisema eneo la malisho kwa mifugo ni muhimu kwa sababu litaondoa wafugaji katika uchungaji hadi katika ufugaji wa kisasa.
  “Tusipofanya hivyo tutakuwa katika zama zile zile za ujima na watu hao wataendelea kuwa wachungaji badala ya wafugaji maana mwaka mzima unamuhudumia ng’ombe. Wenzetu Namibia na Botswana wana ng’ombe milioni mbili, lakini wanafaidika nao kwa sababu ngombe wao mmoja aliyelishwa vizuri ana kilo 430.
  “Sisi tuna ng’ombe milioni 20, lakini hawatufaidishi kiasi kwamba hata mchango wao katika Pato la Taifa ni mdogo. Tunajisifia kuwa tuna ng’ombe wengi wakati hawatufaidishi kwa kuwa hawachinjwi,” alisema Rais Kikwete.
  Alisema kitendo cha mifugo kuwa na eneo maalumu la malisho kitaisaidia nchi kuwa na viwanda vingi vya kutengenezea bidhaa zinazotokana na mazao ya mifugo.
  “Mkishakuwa na maeneo hayo, maana yake viwanda vya kusindika nyama na maziwa vitaongezeka, sioni kwa nini tushindwe kufanikiwa katika eneo hilo na malisho hayo lazima yawe karibu na viwanda hivyo,” alisema Rais Kikwete.
  Mbali na hayo, aliitaka Wizara kuendelea na utafiti wa mifugo kwa kuwa ni muhimu; na aliahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha katika eneo hilo.
  “Utafiti ni muhimu katika mifugo, endeleeni na utafiti katika mifugo na uvuvi na Serikali itazidi kutoa fedha katika eneo hilo, kwani bila kufanya utafiti mambo yatakuwa si mazuri,” alisema Rais Kikwete.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine ninatamani niwe na kiboko kireeeefuuuuuuuuu!!!! au mkwaju.
   
 3. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hii ni kali sana!!

  Embu tuone kama agizo hilo litatekelezwa.... Kwani hii nchi kila mtu ni rais au waziri..
   
 4. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  April fool,altenative ya ajira hiyo walaji wa samaki itakuwaje?
   
Loading...