JK awashukia Uamsho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK awashukia Uamsho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Kikwete
  [​IMG]


  Rais Jakaya Kikwete amelaani na kukemea vikali matukio ya vurugu yaliyotokea hivi karibuni Zanzibar na kukionya kikundi cha Jumuiya ya Uamsho kurejea kwenye lengo lililokusudiwa kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo.

  Rais alitoa kauli hiyo jana kwenye hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi, ambapo alisema haoni sababu kikundi hicho kilichosajiliwa kama cha kidini kujiingiza kwenye masuala ya siasa na kusababisha vurugu.

  “Naungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kauli yake aliyoitoa jana (juzi) katika mkutano wake na waandishi wa habari ya kukemea vikali na kulaani uhalifu huo,” alisema.

  Alisema ni jambo la kushangaza hata kama kikundi hicho kimeamua kujiingiza kwenye siasa ni vipi madai yao ya Muungano yakahusishwa na uchomaji wa makanisa.

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, kikundi hicho kimeingia katika kuwahamasisha wananchi na kuchochea vurugu hizo, ambapo ni kwenda kinyume na dini zao lakini na demokrasia pia.

  “Baya zaidi, katika uchochezi huo majengo na mali za makanisa mawili zilichomwa moto, maduka ya watu kuvunjwa na mali zao kuibwa. Kwa kweli vitendo hivi ni uhalifu ambao haukubaliki na wala hauvumiliki,” alisema.

  Alisema kama hoja ya muungano, ni vema taratibu zikafuatwa na kuudai, kwani makanisa yaliyopo Zanzibar hayana uhusiano na kinachodaiwa, lakini pia Muungano umeukuta ukristo.

  “Ni jambo la kusikitisha na kushangaza kwamba, wenzetu hawa wamefanya uhalifu huo kwa hoja ya kupinga Muungano. Haiwezekani mtu anayepinga Muungano akaitetea hoja yake kwa kuchoma moto makanisa au kuvunja maduka ya watu na kupora mali zao.

  Ukristo haukuingizwa Zanzibar na Muungano, bali ulikuwepo karne kadhaa kabla ya Muungano na wala haukutokea Tanzania Bara,” alisisitiza.

  Katika hotuba yake ya juzi, Rais wa Zanzibar Dkt. Shein, pamoja na kueleza kwa ufasaha ukweli wa suala hilo, pia alisisitiza suala la haki na uhuru wa Kikatiba wa mtu kuchagua au kubadilisha dini au imani yake.

  Katika kutumia uhuru huo, alisema mtu hastahili kuingiliwa au kulazimishwa na mtu yoyote na kwamba hayo pia ni matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Aidha, Rais Kikwete alishangazwa na matukio hayo kwa kisingizio cha Muungano wakati Serikali yake imetoa fursa kwa watu kutoa maoni yao kwenye mjadala wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

  “Kama tujuavyo sote, Tume ya Katiba imekwishaundwa na inajiandaa kupita kote nchini kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya waitakayo. Kama mtu ana maoni yake kuhusu Muungano, hiyo ndiyo fursa ya kufanya hivyo.

  Utaratibu mzuri umewekwa kwa ajili yetu sote, vurugu za nini? Alihoji.
  Alisema haipendezi wala haifurahishi kwa Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya raia wake, lakini, kama hapana budi,

  Serikali lazima ifanye na haitasita kufanya hivyo na kuwasihi viongozi na wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho kurejea kwenye madhumuni ya msingi ya jumuiya yao.

  Pamoja na hayo, Rais pia alitumia muda mwingi kuelezea jitihada zinazofanywa na jumuiya za kimataifa na dunia kwa ujumla katika kukabiliana na baa la njaa duniani.

  Alisema suala la usalama wa chakula duniani ni muhimu na kwamba inakadiriwa kuwa kuna watu milioni 925 wanaokabiliwa na njaa na lishe duni ambapo kati ya hao, Afrika ina watu milioni 239 ambao ni karibu theluthi moja ya watu wote wenye tatizo la njaa na lishe duni kote duniani.

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, nchi za Afrika zenye tatizo la njaa kiasi cha kuhitaji msaada wa chakula kutoka nje ni 27 ambapo kati ya hizo 11 zina matatizo makubwa zaidi na Tanzania siyo miongoni mwa nchi hizo ingawa haijafikia kiwango cha kujitosheleza kabisa.

  “Mwaka 2009, katika mkutano wa L’Aquila, Italia, viongozi wa nchi nane tajiri kuliko zote duniani waliamua kuchukua hatua ya kuzisaidia nchi zinazoendelea duniani kukabiliana na tatizo la njaa na lishe duni. Katika mkutano ule waliahidi

  kutoa dola za Marekani bilioni 22 kwa ajili hiyo. Tanzania tunategemea kupata dola milioni 22.9,” alisema.
  Alisema kwenye mkutano wa nchi hizo, maarufu kwa jina la G-8 uliofanyika Camp David, Marekani Mei 19, 2012,

  pamoja na mambo mengine, viongozi hao walizungumzia suala la usalama wa chakula na lishe barani Afrika lengo likiwa ni kuchangia katika juhudi zinazofanywa na mataifa ya Afrika yenye shabaha ya kutokomeza matatizo hayo.

  “Tofauti na walivyofanya L’Aquila, safari hii waliamua kuchangia katika utekelezaji wa mipango na progamu ya kuendeleza kilimo katika nchi za Afrika hasa zile zinazolenga kujenga usalama wa chakula na lishe… waliamua kuwa

  wataanza na nchi tatu na kuendelea kuziongeza kila baada ya muda fulani, badala ya kuanza na nchi zote mara moja,” alisema na kuzitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Ethiopia na Ghana.

  Rais Kikwete alisema mpango wa Tanzania wa kuendeleza kilimo katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania ulichukuliwa kuwa ni wa mfano na wameona kuwa unafaa kuenezwa barani Afrika kama mkakati sahihi wa kuendeleza kilimo, kujitosheleza kwa chakula na kupunguza umaskini.

  Mpango huo kwa Bara la Afrika ambao unaitwa Grow Africa Partnership, tayari nchi saba zimeshajiunga nao ambazo ni Tanzania, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Ethiopia, Ghana na Burkina Faso.
  Katika mkutano wa Camp David, Rais Kikwete alisema nchi za Marekani, Japani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na

  Urusi zimeahidi kuichangia Tanzania katika juhudi za kuendeleza kilimo na hasa zile zenye lengo la kujitosheleza kwa chakula na kuboresha lishe na kwamba ahadi iliyotolewa na Umoja wa Ulaya katika mkutano huo ni dola za Marekani milioni 897 katika kipindi cha sasa na 2015.

  Katika kuwakarimu wawekezaji katika sekta ya kilimo ili kutekeleza mpango huo, Rais Kikwete alisema upo utaratibu mzuri wa kuwapatia wakulima wakubwa ardhi ya kilimo na ufugaji, utaratibu wenyewe ni kwa kila wilaya kutenga ardhi kwa ajili ya wakulima hao na kisha kutoa taarifa kwa Kituo cha Uwekezaji na kuingizwa katika kituo kinachoitwa Benki ya Ardhi.

  “Mwekezaji anapojitokeza, kulingana na aina ya kilimo anachotaka kujihusisha nacho, hugawiwa ardhi hiyo.
  Ardhi hiyo ni ile ambayo siyo inayotumiwa na wakulima wadogo. Katu hawanyang’anywi ardhi wakulima wadogo ili kuwapa wakulima wakubwa,” alisema na kusisitiza kuwa hiyo siyo sera ya Tanzania.

  Alisema Watanzania wakijitosheleza kwa chakula na kwa maana pana ya chakula chenye lishe bora, watakuwa wamefanikiwa kupata ufumbuzi wa tatizo kubwa la ukosefu wa lishe bora miongoni mwao.
  Kuhusu mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, alisema kwanza ni mara ya kwanza kufanyika katika ardhi ya

  Tanzania tangu kuanzishwa kwake 1964, na kwamba ni fursa adimu kupatikana na anaamini Watanzania waliowakilishwa na wenzao wa Arusha, wametumia ipasavyo fursa hiyo katika suala la kibiashara.

  Ameishukuru benki hiyo kwa mchango mkubwa waliotoa na wanaoendelea kuutoa kuchangia maendeleo ya nchi yetu ambapo imekuwa ikitoa mikopo na misaada muhimu kwa maendeleo ya sekta mbalimbali nchini pamoja na zile za elimu,

  afya, maji na miundombinu ya barabara, reli, umeme na mingine mingi.
  Alisema benki hiyo imewezesha kujengwa kwa barabara ya Namanga – Arusha, Minjingu – Singida, Namtumbo –

  Tunduru, Iringa – Dodoma, Mayamaya – Babati na Tunduru – Mangaka – Mtambaswala ambapo awali pia waliwezesha kujengwa kwa barabara ya Mutukula – Muhutwe na sasa wanagharamia upembuzi yakinifu na usanifu wa reli mpya kutoka Dar es Salaam hadi Rwanda na Burundi.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Rais wenu anapenda misiba. namshangaa naye analaani bila hatua. ama kweli futari siyo lishe nzuri.
   
 3. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndo mjiandae tena waislamu wote mrudi zenji na wakristo warudi bara,ndo tasfiri ya kilichotokea zenji,na ule mkutano wenu wa tarehe 27may wa kutaka rais muislamu na mahakama yakazi Tz hamuwezi hata kidogo,hata mumshawishi jk vipi ameishia kuwapa vyeo tu akitoa mguu na nyinyi wenye vyeo vya udini mjiandae kuchomoka maana kila kukicha amemteua mwanaasha,hamisi,shabani.mmezoea roho mbaya tangu kuzaliwa mpaka makuzi yenu,hivi kweli kuna Mungu kwenu?Mungu gani wa Machafuko
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hana jinsi zaidi ya kulaani wanachokifanya
   
 5. B

  BORGIAS Senior Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
   
Loading...