JK awaruka 'wabunge'

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Rais Jakaya Kikwete jana wakati 'anakamata' Fanta yake wakati wa kuwapongeza wabunge waliopitisha hoja aliyoiita muhimu kwa uchaguzi wa demokrasia, aliwaponda na kuwaruka watu wanaojipitisha kwenye majimbo kuomba kupendwa ili waweze kuwa wabunge kwenye Bunge lijalo.

JK akiwa mjini Dodoma alisema wapo 'wabunge' wanaoeleza kuwa wametumwa naye kutangaza nia na kujipitisha kwa wapiga kura ili baada ya ushindi wachaguliwe kuwa mawaziri.

"Hao wanaojipitisha wakitumia jina langu kuwa nimewatuma ni waongo, siwezi kutuma mtu kuwania ubunge, siko hivyo."

"Mimi nina nafasi zangu 10 kuwachagua watu ambao naamini watanisaidia kuwaletea maendeleo Watanzania wenzangu, sasa niwatume hao wanini, wakati hizo 10 zinanitosha sana," aliongeza JK kwa tabasamu kama kawaida na kufuatiwa na kicheko cha kiaina.
-------
Kazi kweli kweli, ingawa kwenye nafasi zake najua anateua wabnge wake wakati wa lala salama, sina uhakika na hatua hiyo. Tuchangie mawazo
 
obama-avatar.jpg



anyone seen Avatar?
 
Alikuwa anafutahisha genge!
Kwani kilolo walifanyaje kumtoa mwamoto?
Msola alianza kampeni mapema huku akiwaeleza wananchi
Kuwa ametumwa kwa sababu wanataka kumpa uwaziri
Na ikawa hivyo.
 
Kawambwa usimsahau!!!woote bagamoyo waliogopa kuchukua form maana walishajua kuwa ameambiwa akachukue form!!
 
Na bado tunaambiwa kwamba amemtuma Kandoro kule kalenga ili ampe uwaziri wa TAMISEMI!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom