JK awaonya wabadhirifu fedha za miradi

Jul 24, 2012
81
6
lhamisi, Agosti 16, 2012 09:55 Na Mwandishi Wetu, Dodoma *Awataka wakuu wa idara, wananchi wawataje
*Asisitiza watachukuliwa hatua kali za sheria
RAIS Jakaya Kikwete amewaonya baadhi ya watumishi wa taasisi za serikali wanaotumia vibaya na kufuja fedha za miradi inayotolewa na wafadhili kutoka mataifa mbalimbali.

Kikwete pia amewahimiza wakuu wa idara na raia wema kuwataja watu wanaoendekeza tabia ya wizi ama ubadhirifu wa fedha za miradi hiyo waweze kuchukuliwa hatua kali za sheria.

Onyo hilo alilitoa jana alipozindua awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) mjini Dodoma.

Alisema wananchi hawana budi kuwafichua wezi na wabadhirifu wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo inawalenga kuwaondolea umasikini.

Rais aliwaagiza wananchi kutowaonea aibu watu ambao wamekuwa kikwazo katika miradi mbalimbali ya serikali kwa maendeleo ya wananchi.

“Tusiwaonee haya watu hawa, tuwafichue waweze kuchukuliwa hatua na fedha zitakazotolewa ziwanufaishe wananchi ambao ndiyo walengwa na siyo mtu mwingine,” alisema Rais Kikwete.

Alisema serikali itaendelea kuwaunga mkono wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakionyesha nia ya kusaidia kuondoa umaskini katika kaya mbalimali nchini.

Rais alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na Tasaf katika kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo itasadia kupunguza umasikini katika kaya nyingi nchini.

Aliziagiza halmashauri nchini kuwa na uataratibu wa kuajiri watumishi kwa ajili ya miradi yote ambayo itakuwa inakamilika iweze kutoa huduma katika wakati muafaka.

“Miradi mingi imekuwa ikikamilika bila ya kuwa na wataalamu katika maeneo husika hivyo kusababisha miradi kama ya hospitali kushindwa kufanya kazi kwa kukosa waganga.

“Kwa hali hiyo basi nitoe wito kwa halmashauri kuwa na utaratibu wa kuajiri kila mradi unapoanza,” alisema.

Hata hivyo alitoa wito kwa Tasaf kubuni vyanzo vya mapato ili miradi yote inayobuniwa na wananchi ipate fedha kwa ajili ya kuiendesha.
 
"He doesn't mean what he said" Ndio maana Deni la nchi linazidi kupaa, kwa kujilimbikizia mapesa Uswizz
 
Hii ni sawa na changudoa kuwaonya machangudoa wenzake waache uchungudoa ili afaidi yeye peke yake hela ya mabuzi.

Ndyali: Aisee umenivuja mbavu. You have real made my day. Hii lazima niitoe leo baa wakati napata moja baridi.
 
Ndyali: Aisee umenivuja mbavu. You have real made my day. Hii lazima niitoe leo baa wakati napata moja baridi.

Asante Mkuu Bobuk, kusema kweli tumechoshwa na usanii wa mwanamazingaombwe huyu ndo maana tunatumia maneno ya mifano halisi ili wananchi wajue usanii wake.
 
mbona yeye kapiga za richmond,epa,wanyamapori na hajapewa onyo?katiba mpya iruhusu rais ashitakiwe
 
Back
Top Bottom