Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Nimetulia muda kidogo na kupitia kwa kina tamko la "serikali kuhusu uchunguzi wa Benki Kuu" ambalo lililotelewa leo na Katibu Mkuu kiongozi Bw. Phillemon Luhanjo. Unaweza kujipatia nakala yako ya pdf kwenye "Pics and Docs" hapo KLH News.
Baada ya kupata muda wa kutafuna na kumeza tamko hilo, ninajikuta hamasa na uchangamfu wote umenitoka baada ya kugundua kuwa Watanzania tumefungwa goli tena siyo la mkono wa Mungu, na wala si la kuotea, ni goli ambalo Kapteni wetu wa timu alikuwa anaelekea kwenye lango la adui lakini kwa sababu anazozijua yeye akageuka na kuchomeka kimiani goli moja safi sana ambalo sisi sote tukajikuta tumenyanyuka kwenye viti vyetu kushangalia!
Kwanini nasema tumefungwa goli na Rais Kikwete na tumebaki kushangilia na kutoa pongezi kwa goli zuri?
a. Tamko hilo limeacha impression bila ya kusema moja kwa moja kwanini uteuzi wa Balali umetenguliwa. Je, Balali ameondolewa Ugavana kwa sababu ameshiriki kukomba fedha hizo, kuzembea, kula njama au kwa namna yoyote ile kuhusika na upotevu huo? Je, Gavana Balali ni mtuhumiwa wa Uhalifu au ameondolewa ili kuleta mabadiliko na "atapangiwa kazi nyingine serikalini"?
b. Rais ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa BoT kukutana mara moja na "kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hii kwa taifa." Tatizo ni kuwa Bodi hii ndiyo ilikuwa inatakiwa kuisimamia Benki Kuu! Inakuwaje Bodi iliyoshindwa kusimamia fedha zetu leo ndio iwe ya kwanza kuchukua hatua? Je watu wote waliomo kwenye bodi hawakuhusika kwa namna moja au nyingine na upotevu huo? Jinsi Mwenyekiti wa Bodi ya ATC alivyoingilia utendaji kwenye sakala la BoT ni kwanini tuamini kuwa hakuna mjumbe wa Bodi ambaye alihusika na upotevu wa fedha zetu BoT? Kwanini Rais asiivunje Bodi yenyewe ya BoT na kuunda mpya ambayo ingepewa jukumu hilo?
Kwanini Watanzania waamini kuwa Bodi ya Wakurugenzi watafanya kile walichoshindwa kufanya miaka yote hii? Kwanini Rais Kikwete kama kweli "amesikitishwa na kukasirishwa" na kitendo hiki asivunje na kupangua nafasi zote za ajira ya serikali huko BoT (ana nguvu na uwezo wa Kikatiba kufanya hivyo) na kuindua BoT upya!?
c. Kutokana na (b) hapo juu, Rais Kikwete anataka kutuambia kuwa mtu pekee ambaye yeye ana uwezo wa kutengua ajira yake Benki Kuu ni Gavana pekee? au anataka tuamini kuwa kati ya watu wote wenye nafasi za kuteuliwa Benki Kuu ni Balali pekee anayehusika na upotevu wa fedha?
d. Kwa vile Benki Kuu iko chini ya Wizara ya Fedha, ni kwa kiasi gani Wizara ya Fedha imeshindwa kusimamia Benki Kuu na kuruhusu upotevu mkubwa wa fedha kiasi hicho? Je wale waliokuwa watumishi wa Wizara ya Fedha wakati wa upotevu huu wao wamechukuliwa hatua gani?
e. Inaonekana kuwa Rais Kikwete hataki kwenda nje ya hiyo ripoti tu na hivyo kuwanusuru rafiki na jamaa zake wengine wanaotajwa katika upotevu mwingine. Kuna uwezekano wowote wa Rais Kikwete kuruhusu full investigation wa Benki Kuu miaka 10 iliyopita na kuona ukubwa wa tatizo hilo badala ya kuangalia ka "akaunti" kamoja tu?
f. Kwa vile tatizo hili la EPA ni kidogo tu na bila ya shaka kuna uhalifu umetendeka je Rais Kikwete haoni ulazima wa kualika timu ya kitaalamu kama toka "US Secret Service" au the New Scotland Yard kufanya uchunguzi wa Benki Kuu kuanzia juu hadi chini na kupanua wigo wao hadi nje ya mipaka yetu ili kuona na kutafuta wahalifu waliokwapua fedha za Watanzania?
g. Kwa upande wa Balali, ripoti inasema uteuzi "umetenguliwa" lakini haisemi kama amefukuzwa kazi au kuondolewa katika utumishi wa serikali ya Muungano. Je, Gavana Balali bado ni mwajiriwa wa serikali ya Muungano? Kama anatuhumiwa kufanya uhalifu je serikali ya Tanzania ina mkataba wowote wa kutumiana watuhumiwa na Marekani (extradition treaty) au Balali akiomba political asylum Marekani ndio itakuwa imetoka hiyo?
h. Rais ameagiza kuwa vyombo vya usalama licha ya kuchukua hatua dhidi ya watu na makampuni (hata kama hayapo tena na yamefilisiwa) pia wahakikishe fedha zilizolipwa bila uhalali zinarudishwa. Je hili halitukumbushi mawazo yake kuhusu suala la Rada kuwa "tutaidai serikali ya Uingereza waturudishie fedha zetu kama tutakuwa tumelipa zaidi kwani BAE ni kampuni ya serikali"? Kama makampuni haya hayapo na yamejitangaza kufilisiwa ni kwa kiasi gani atarudisha fedha hizo?
Nikiendelea kutafuta majibu ya maswali hayo najikuta sina jinsi ila kukaa chini na kuacha kushangiia goli tulilofungwa na Kapteni wetu! Naweza kuwa nimekosea mahali fulani lakini siko mbali sana na ukweli.
Hata hivyo hatua moja ya alizozichukua haina budi kupongezwa nayo ni kusitisha malipo kwenye akaunti hiyo. Lakini Rais angeweza kwenda mbele zaidi kwa kuvunja kitengo kizima cha EPA na kukiweka chini ya uangalizi maalumu na kuomba msaada toka IMF au WB kukiendesha kwa muda.
Nitaendelea kuandika kwa kadiri mawazo yangu yanavyotiririka!