JK Awafunga goli watanzania, wao washangilia!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,399
39,550
Nimetulia muda kidogo na kupitia kwa kina tamko la "serikali kuhusu uchunguzi wa Benki Kuu" ambalo lililotelewa leo na Katibu Mkuu kiongozi Bw. Phillemon Luhanjo. Unaweza kujipatia nakala yako ya pdf kwenye "Pics and Docs" hapo KLH News.

Baada ya kupata muda wa kutafuna na kumeza tamko hilo, ninajikuta hamasa na uchangamfu wote umenitoka baada ya kugundua kuwa Watanzania tumefungwa goli tena siyo la mkono wa Mungu, na wala si la kuotea, ni goli ambalo Kapteni wetu wa timu alikuwa anaelekea kwenye lango la adui lakini kwa sababu anazozijua yeye akageuka na kuchomeka kimiani goli moja safi sana ambalo sisi sote tukajikuta tumenyanyuka kwenye viti vyetu kushangalia!

Kwanini nasema tumefungwa goli na Rais Kikwete na tumebaki kushangilia na kutoa pongezi kwa goli zuri?

a. Tamko hilo limeacha impression bila ya kusema moja kwa moja kwanini uteuzi wa Balali umetenguliwa. Je, Balali ameondolewa Ugavana kwa sababu ameshiriki kukomba fedha hizo, kuzembea, kula njama au kwa namna yoyote ile kuhusika na upotevu huo? Je, Gavana Balali ni mtuhumiwa wa Uhalifu au ameondolewa ili kuleta mabadiliko na "atapangiwa kazi nyingine serikalini"?

b. Rais ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa BoT kukutana mara moja na "kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hii kwa taifa." Tatizo ni kuwa Bodi hii ndiyo ilikuwa inatakiwa kuisimamia Benki Kuu! Inakuwaje Bodi iliyoshindwa kusimamia fedha zetu leo ndio iwe ya kwanza kuchukua hatua? Je watu wote waliomo kwenye bodi hawakuhusika kwa namna moja au nyingine na upotevu huo? Jinsi Mwenyekiti wa Bodi ya ATC alivyoingilia utendaji kwenye sakala la BoT ni kwanini tuamini kuwa hakuna mjumbe wa Bodi ambaye alihusika na upotevu wa fedha zetu BoT? Kwanini Rais asiivunje Bodi yenyewe ya BoT na kuunda mpya ambayo ingepewa jukumu hilo?

Kwanini Watanzania waamini kuwa Bodi ya Wakurugenzi watafanya kile walichoshindwa kufanya miaka yote hii? Kwanini Rais Kikwete kama kweli "amesikitishwa na kukasirishwa" na kitendo hiki asivunje na kupangua nafasi zote za ajira ya serikali huko BoT (ana nguvu na uwezo wa Kikatiba kufanya hivyo) na kuindua BoT upya!?

c. Kutokana na (b) hapo juu, Rais Kikwete anataka kutuambia kuwa mtu pekee ambaye yeye ana uwezo wa kutengua ajira yake Benki Kuu ni Gavana pekee? au anataka tuamini kuwa kati ya watu wote wenye nafasi za kuteuliwa Benki Kuu ni Balali pekee anayehusika na upotevu wa fedha?

d. Kwa vile Benki Kuu iko chini ya Wizara ya Fedha, ni kwa kiasi gani Wizara ya Fedha imeshindwa kusimamia Benki Kuu na kuruhusu upotevu mkubwa wa fedha kiasi hicho? Je wale waliokuwa watumishi wa Wizara ya Fedha wakati wa upotevu huu wao wamechukuliwa hatua gani?

e. Inaonekana kuwa Rais Kikwete hataki kwenda nje ya hiyo ripoti tu na hivyo kuwanusuru rafiki na jamaa zake wengine wanaotajwa katika upotevu mwingine. Kuna uwezekano wowote wa Rais Kikwete kuruhusu full investigation wa Benki Kuu miaka 10 iliyopita na kuona ukubwa wa tatizo hilo badala ya kuangalia ka "akaunti" kamoja tu?

f. Kwa vile tatizo hili la EPA ni kidogo tu na bila ya shaka kuna uhalifu umetendeka je Rais Kikwete haoni ulazima wa kualika timu ya kitaalamu kama toka "US Secret Service" au the New Scotland Yard kufanya uchunguzi wa Benki Kuu kuanzia juu hadi chini na kupanua wigo wao hadi nje ya mipaka yetu ili kuona na kutafuta wahalifu waliokwapua fedha za Watanzania?

g. Kwa upande wa Balali, ripoti inasema uteuzi "umetenguliwa" lakini haisemi kama amefukuzwa kazi au kuondolewa katika utumishi wa serikali ya Muungano. Je, Gavana Balali bado ni mwajiriwa wa serikali ya Muungano? Kama anatuhumiwa kufanya uhalifu je serikali ya Tanzania ina mkataba wowote wa kutumiana watuhumiwa na Marekani (extradition treaty) au Balali akiomba political asylum Marekani ndio itakuwa imetoka hiyo?

h. Rais ameagiza kuwa vyombo vya usalama licha ya kuchukua hatua dhidi ya watu na makampuni (hata kama hayapo tena na yamefilisiwa) pia wahakikishe fedha zilizolipwa bila uhalali zinarudishwa. Je hili halitukumbushi mawazo yake kuhusu suala la Rada kuwa "tutaidai serikali ya Uingereza waturudishie fedha zetu kama tutakuwa tumelipa zaidi kwani BAE ni kampuni ya serikali"? Kama makampuni haya hayapo na yamejitangaza kufilisiwa ni kwa kiasi gani atarudisha fedha hizo?

Nikiendelea kutafuta majibu ya maswali hayo najikuta sina jinsi ila kukaa chini na kuacha kushangiia goli tulilofungwa na Kapteni wetu! Naweza kuwa nimekosea mahali fulani lakini siko mbali sana na ukweli.

Hata hivyo hatua moja ya alizozichukua haina budi kupongezwa nayo ni kusitisha malipo kwenye akaunti hiyo. Lakini Rais angeweza kwenda mbele zaidi kwa kuvunja kitengo kizima cha EPA na kukiweka chini ya uangalizi maalumu na kuomba msaada toka IMF au WB kukiendesha kwa muda.

Nitaendelea kuandika kwa kadiri mawazo yangu yanavyotiririka!
 
Ahsante MKJJ,

Ninaipitia over lunch.Naona hot off the press.

Congrats on the new site.
 
Mimi nilishasema wabongo tumepigwa tena changa la macho halafu watu wengine wanamshangilia Tapeli na Msanii Mkuu Kikwete. Huyu jamaa hafai hata kuwa Katibu Kata.
 
Kudos! good analysis keep it up!
Mosi, Nami nashangaa kama Raisi ameweza kumwondoa Papa(Gavana, iweje ashindwe kuwawajibisha dagaa(BOT staff)?
Pili, Kamwondoa Balalli baada kuona ana hatia ya kuwa mshiriki au mtuhumiwa katika sakata hili. Kwa nini asiamuru watuhumiwa wakamatwe na kushitakiwa? Ushahidi gani wa ziada unahitajika?
Tatu, Je vyombo kama Polisi na PCCB havina self motivation ya kufanya uchunguzi mpaka viwe prompted na Raisi? Miezi sita nayo mingi kukamilisha kazi hii.
Nne: Kwanini full report haitolewi hadharani?

Hitimisho: Ngonjera as predicted
 
Amen!! i wonderin abt the same thing...how do companies that no longer exist pay back...and how the same directors who were there for over 10 yrs solve the problem they have harbouring all that time?? the carpet has been pulled from under us KENYAN style...ha ah ahhah aha
 
Mkijiji we ni kichwa! unaona hatua mia mbele yatulio wengi,Yaani umenionyesha upande wa pili wa shilingi. good job bro, tunahitaji vichwa kama hivi ilikutoka tulipo!
 
maskini wee wanadhubutu kumtoa sadaka mtu ambaye walishirikiana naye kwenye madili yoote machafu au it might b walikubaliana hebu niasaidieni mlioko bongo family ya BAlali iko bongoo??usije kuta nayo iko USA yamuuguza immaginary "mgonjwa"
 
Mwanakijiji hii kitu kama unaweza itoe kwenye Magazeti ya Bongo itakuwa makini sana. Maana najua waandishi wa Bongo walivyokuwa wapambe wakuu wa Msanii JK, Kesho headings zao zitakuwa Kikwete Kiboko, Kikwete Mwisho, Kikwete Afanya Kweli.

Asilimia kubwa ya waandishi wetu hawakai chini kutathmini na kuzichambua taarifa kwa ufanisi na umakini wa hali ya juu. Wao huishia kutoa pongezi tu pasipo kukwaruza bongo zao na kufanya uchambuzi wa kina. Hongera sana Mwanakijiji kwa kufanya hilo.
 
Kudos! good analysis keep it up!
Mosi, Nami nashangaa kama Raisi ameweza kumwondoa Papa(Gavana, iweje ashindwe kuwawajibisha dagaa(BOT staff)?
Pili, Kamwondoa Balalli baada kuona ana hatia ya kuwa mshiriki au mtuhumiwa katika sakata hili. Kwa nini asiamuru watuhumiwa wakamatwe na kushitakiwa? Ushahidi gani wa ziada unahitajika?Tatu, Je vyombo kama Polisi na PCCB havina self motivation ya kufanya uchunguzi mpaka viwe prompted na Raisi? Miezi sita nayo mingi kukamilisha kazi hii.
Nne: Kwanini full report haitolewi hadharani?

Hitimisho: Ngonjera as predicted

Niseme tu kuwa hiii Ni Point Kamili sina budi kuirudia::::pili, Kamwondoa Balalli baada kuona ana hatia ya kuwa mshiriki au mtuhumiwa katika sakata hili. Kwa nini asiamuru watuhumiwa wakamatwe na kushitakiwa? Ushahidi gani wa ziada unahitajika?
 
kwa akili yangu ndooogoo ni kuwa hata Jk ni mmojawapo ya watuhumiwa wa scandal hili zima..na baadhi ya mawazir wake...
 
Burying Bad News at convenient times.....Hivi Kenya mambo vipi?? Baraka Ockbamer niaje?
 
Kuna mambo mengine nafuatilia kutokana na hili na hatimaye nitafanyia marekebisho ya hapa na pale. Your inputs and critique is highly appreciated. Nataka nihakikishe yanatoka kwenye magazeti ya nyumbani kabla ya mwisho wa juma.
 
Kuna mambo mengine nafuatilia kutokana na hili na hatimaye nitafanyia marekebisho ya hapa na pale. Your inputs and critique is highly appreciated. Nataka nihakikishe yanatoka kwenye magazeti ya nyumbani kabla ya mwisho wa juma.

Yap. Itoe wakata suala lenyewe likiwa bado moto. Najua makanjaja wetu kesho kwenye magazeti mengi itakuwa JK kafanya kweli, kafanya kufuru, kasi mpya, ari mpya...and blah...blah...blah.
 
Yeah nimeshapata preview ya baadhi ya magazeti mengine yanasema "JK Amng'oa Balali"...
 
Kuwa involve US Secret Service, Scotland Yard, WB na IMF central bank kunaweza kuwa counter productive katika mambo ya national security.

Tumekwisha, ndani hatuna mtetezi, nje nako utata kibao!

Naona Tanzania tumejipatia "Goldenberg Affair" yetu.Natafuta habari zaidi jinsi Kenya walivyo wa involve Scotland Yard kwenye hii issue bila kukwaza na possibility ya economic espionage katika kuchunguza ufisadi.
 
Pundit, ripoti yenyewe imetokana kutokana pressure ya hao wakubwa kwa sababu walikuwa wanajua mambo mengi yanayosemwa na ni wao ndio wanatrack large movement of cash.. si unajua mambo ya "funding terrorists".

Pasipo wao kudokeza yawezekana hata tusingejua.. na wanajua mengi zaidi...
 
MKJJ: ile nchi tuna njaa na kiu kali sana ya mafanikio; hatujayaona siku nyingi, sasa ikitokea hata kuachuro kidogo inabidi tushangilie. Waliosoma Zoology wanajua kuwa kama minyoo imekosa chakula siku nyingi, siku ikikipata inabidi ile hata michanga wakidhani nayo ni chakula. Ndio CCM ilipotufikisha hapo, kushangilia mafanikio hewa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom