Kikwete awaachia huru Polisi waliomuua Jenerali Kombe

Rais Jakaya Kikwete amewaachia huru askari polisi wawili Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe. Wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais ambaye alipunguza adhabu hiyo ya kifo, kuwa kifungo cha miaka miwili jela.

Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol mali ya W. Ladwa, kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.

::Mwananchi::
Kwa maelezo yako Hao askari wawili hawakumuuwa huyo Jenerali kombe kwa Makusudi kama ni hivyo Rais J.K . Ana haki ya kuwaachia huru ingawa Mahakama kuu ilitoa Adhabu ya kifo. Je Tuangalie Sheria yetu inasemaje je mtu akiuwa kwa bahati mbaya anaweza kuhukumiwa Adhabu ya Kifo? Na hata kama atahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kifo mwamuzi wa mwisho ni Rais ,Rais akitia saini ndipo anaweza huyo mtu kuuwawa Natanguliza hivyo asanteni...
 
Kwa maelezo yako Hao askari wawili hawakumuuwa huyo Jenerali kombe kwa Makusudi kama ni hivyo Rais J.K . Ana haki ya kuwaachia huru ingawa Mahakama kuu ilitoa Adhabu ya kifo. Je Tuangalie Sheria yetu inasemaje je mtu akiuwa kwa bahati mbaya anaweza kuhukumiwa Adhabu ya Kifo? Na hata kama atahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kifo mwamuzi wa mwisho ni Rais ,Rais akitia saini ndipo anaweza huyo mtu kuuwawa Natanguliza hivyo asanteni...
Ulijuaje walimwuua kwa bahati mbaya? Unawezaje kumpiga risasi "mhalifu au mtuhumiwa" ambaye kishaweka juu mikono yake? It was cold blooded murder ordered by someone. Otherwise kwa nini wapewe msamaha sasa na hela za kuanzishia biashara?
 
Ni shinikizo toka kwa kikosi cha mauaji, ni kama vile hakikuwa active na sasa kimeibukia kwa akina Mwakyembe baada ya ya shinikizo lao la kutaka wenzao waachiwe kutimizwa......sasa chizi kapewa rungu tutashuhudia mengi....
 
waliohukumiwa kifo ni hawo tuu mbona kuna wengine wamekaa zaidi ya miaka 30 hawo vip????
 
Mimi nasema hivi Kikwete anataka tulipize visasi.SASA BASI UWEZO WA VISASI TUNAO,NIA TUNAYO NA SABABU TUNAYO.
 
Awezi JK kwa sababu shida ni kwamba BABu Seya amekula na demu wake ndio nooma yote hiyo. Ukweli ndio hiyo na upo wazi ssa nauliza yeye JK atakua na wanawake wagapi ?? Mbona Rais mzima anatotia aibu ??? Malaya kama mbuzi Shame unto him. Afai kwa rais kabisa. Kwa nini tusiingie barabarani kupinga atolewe IKULU.... Tunasubiri lini jamani

una ushahidi kuwa babu seya alimkazia jk mke wake?.
 
Ndugu! Hoja hapa si kwamba kifo cha kombe kiliumiza ama la. Hoja iliyopo hapa ni kuwa je, katiba inampa rais uwezo wa kusamehe? Kama ukisoma ibar ya 45 wala huwez kuwa na jazba za ajabu. Kifo chake kilituumiza ndiyo, lakini na katiba yetu ndo imempa uwezo rais.

Nadhani sasa unapotoka.. kwani kwa kuwa umepewa madaraka ndio huyatumie bila busara? Hapa kwa kweli raisi amechemka na anaonekana kabisa amefanya uamuzi kwa shinikizo fulani kitu ambacho kinazidi onyesha udhaifu wake kuwaogopa wasio na madaraka. Nadhani kuna mauaji mengine yanapangwa ila ukweli utakuja tuu kujionyesha.
 
Wakati mwingine haya mambo yangekuwa yanawekwa wazi umma usingekuwa unawatwisha lawama mtu ingekuwa inajenga baada ya kubomoa.Ni vyema kuwa dunia tunayokwenda kutakuwa na siri za maana na siri zisizo na msingi zitakuwa hazina nafasi.Dunia tunnayokwenda ni dunia ambayo mwasisis wake Nelson Mandera ameianzisha ya ukweli [Trutha and reconciliation].Haya mabo ya babu Sya wakati mwingine yeye na familia yake kukaa ndani ni salama yake zaidi kuliko kuwepo huku nje.

Babau Seya he has never been a national , regional wala street threat to the secuirty mkuu .Kama amewahi thibitisha hapa ni kivipi .
 
Tusinhangaike bure hiyo ni system ya nchi yetu ndivyo wanavyojiendeshea mambo,walishauwawa wengi sana tu.Wakati mwingine tuweke chuki pembeni, hao jamaa waliua mwaka 1996 akiwepo Mkapa....leo 2011 JK anawasemehe manake kazi iliyoanza katika serekali iliyopita JK kafanya kuimalizia tu.Pia inaonekana anaujua ukweli kwamba hawa jamaa waliua na si kwa makusudi kwa mantiki kwamba walitumwa na watu wenye mamlaka nafikiri mna idea na mambo ya Jeshi yalivyo amri kwanza matokeo baadaye.Jifikirie wewe ndio ungekuwa askari hao waliopelekwa kwenye hilo zoezi ukaambia ukauwe watakukinga ..... jaribu kufikiria ungetaaa kingetokea nini?

Cha msingi hapa ni waliotoa hiyo amri ya hayo mauaji ndio wa wakutafutwa...ndio maana mnasikia watu wanapelekwa huko the HAGUE mnafikiri wao ndio walishika bunduki wakamwaga damu?Tafakari..
 
Hiyo si kweli kabisaaaaaaaaaaa ni uwongo uliotukuka.

Hoa polisi walihukumiwa kunyongwa sio kifungo cha maisha na rais hakusaini hukmu hiyo hivyo wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 16 na kama wameachiwa basi watakuwa wamemaliza kifungo chao.

Hiyo ni kama alivyoachiwa mama Liundi au Asha mkwizu baada ya rais kukataa kusaini adhabu zao za kifo.

usimsingizie JK bureeeeee. Mkapa ndio wa kulaumiwa kwa kukataa kusaini hukmu hiyo.

Kama wasema Mkapa hakusaini karatasi hiyo na hukumu ilisha pita JK alikuwa na mamlaka gani ya kuingilia hukumu iliyo pita na kuwa toa? kama wewe wakataa sisi tusimlaumu kwanini asiache nayeye kuingilia jambo hilo. Maana kama JK ame sign watoke basi wamekinzana na hukumu ya mahakama kumbuka mwenzio alipo kuwa kwenye urais haku sign wewe umekuja ukasign watoke mbona hapo mwatukanganya zaidi.

My Take;

Jk ni wakulaumiwa tuuu period
 
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri. Si kila kitu ni siasa, mengine ni sheria zaidi. Ni bora usichangie kuliko kuchangia pumba. Hapa mzembe si Jk bali ni wewe nngu007. Katiba inampa uwezo rais kufuta au kupunguza adhabu yoyote. Rudi darasani!!!

Hili li f a l a nilishabiki la kijinga. Utaona ujinga wa mtu pale mapenz yake yanapozidi na anashabikia hata upuuzi.
Kwani si tunajua uwezo wa kiongozi wako.
 


Kama wasema Mkapa hakusaini karatasi hiyo na hukumu ilisha pita JK alikuwa na mamlaka gani ya kuingilia hukumu iliyo pita na kuwa toa? kama wewe wakataa sisi tusimlaumu kwanini asiache nayeye kuingilia jambo hilo. Maana kama JK ame sign watoke basi wamekinzana na hukumu ya mahakama kumbuka mwenzio alipo kuwa kwenye urais haku sign wewe umekuja ukasign watoke mbona hapo mwatukanganya zaidi.

My Take;

Jk ni wakulaumiwa tuuu period

sasa wewe ulitaka tu wakae gerezani bila kujua hatima yao. Je huoni huo ni kuvunja haki za binadamu kwa kumuweka mtu gerezani bila kumuhukumu?

Kosa la mkapa kwanini alikataa kusaini wakti hukumu hiyo bado ipo katika sheria za nchi yenu.
 
Mauaji ya Kombe hayakuwa ya bahati mbaya; yalikusudiwa. Nakumbuka magazeti mengi yalivyoripoti wakati ule:
Kwamba askari walikuwa wanamfukuza mwizi wa magari
Kombe alikuwa na mkewe nadani ya gari
Kombe baada ya kuona akikimbizwa alisimamisha gari na kutoka nje ya gari
Alinyosha mikono juu ya kujitambulisha, ndyo maana risasi ziliingia kifuani si mgongoni
Askari walimjua vyema kwani alikuwa bosi wao katika masual ya usalama wa Taifa
Kome alikuwa ametoa taarifa rasmi kuwa atasafiri kwa gari hilo kwenda Kilimanjaro,
Mkewe aliyashuhudia yote hayo, na kama askari wangekuwa wanamfuatilia mwizi magari, huyu mama wangemu-arrest baada ya kumuua huyo "mwizi wa magari' ili asaidie upelelezi; lakini huyu mama aliachwa hapo hapo.
Kombe alituhumiwa kumpa Mrema Lyatonga habari za kijasusi za mipango ya kumdhuru na ndiyo maana mitego mingi waliyoweka ilijulikana mapema kwa Mrema na kuweza kuikwepa. Nadhani mtu akienda maktaba anaweza kupata baadhi ya magazeti.
Katika hali hiyo, hawa askari wawili walikuwa wakitekeleza agizo la wakuu ndiyo maana JK kawaachia. Msishangae kuona wanalipwa kinyemela mafao yao!
 
Mie naona yafuatayo:
1. Katiba inayompa Rais madaraka ya kusamehe KOSA LOLOTE, itamke wazi kuwa adhabu ya kifo tunayoipigia kelele, IONDOLEWE KIKATIBA! Hii itaondoa manung'uniko ya Rais kusamehe pale anapojisikia kuna maslahi yake binafsi.
2. Serikali iILIPE familia ya Kombe hayo madai yaliyokubaliwa na Mahakama zetu! Tunaomba Rais alisimamie hili.
3. Maslahi ya Rais hapa, nionavyo mimi, ni kuwagawa wanaharakati wanaounga mkono kuondolewa adhabu ya kifo, ili waone kosa la kuwasamehe askari hawa 2 halikustahili.
4. Tunahitaji KATIBA MPYA SASA!
 
Jamani hii inazidi ku-strength argument ya kuwa na katiba mpya. Haiwezekani muuaji anahukumia kunyongwa,
Rais badala ya kusaini hati ya kunyonga anampunguzia adhabu ya kifo kuwa kifungo cha miaka miwili? Uko wapi
hapa uhuru wa mahakama. Katiba mpya lazima ieleze makosa ambayo rais anaweza kusamehe na yale ambayo
hawezi kusamehe.

Huko Marekani Rais Obama hawezi kabisa kumsamehe mtu aliyehukumiwa kunyongwa. Tatizo letu katiba yetu imempa
madaraka makubwa rais na tunapopata rais kihiyo kama JK ndiyo tunaona ubovu wa katiba. From kifo to two years
imprisonment. Anything is possible in Tanzania. Sasa kwanini watanzania tusiamini kwamba kweli aliuwawa na serikali na CCM?!


Hapo kwenye bold vipi kuhusu Govenor Of state?? Usilinganishe mataifa mawili tofauti yenye Judicial systems tofauti
 
@barubaru
vipi kazi ya kumuondoa gadaffi mmekamilisha? ukimaliza utaenda syria? huku kwetu pia kazi zako za kijasusi zinahitajika
 
JK kaichoka ccm,
anaamua kufanya vituko makusudi ili watanzania muiondoshe ccm madarakani lakini hamtaki
,
ni msaada gani mnaoutaka kutoka kwa JK zaidi ya haya madudu anayoyafanya?
au mnataka aseme wazi kuwa ccm haifai kuongoza nchi?
Kati ya JK na watanzania anaowaongoza nani mjinga hapa sasa?

Mkuu katika watu wote waliochangia hapa wewe ndio umenena maneno ya ukweli ukweli kabisa, maana naona wote hapa wanazunguka tu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom