JK awa kinara wa kuvunja Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi ya mwaka 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK awa kinara wa kuvunja Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi ya mwaka 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mchokonozi, Aug 26, 2010.

 1. M

  Mchokonozi Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliposaini Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi ya mwaka 2010, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Mrisho Kikwete, hakutambua kwamba sheria hiyo ingerudi na kumhukumu kwa kuwa kinara wa kuivunja.

  Akiwa kwenye kampeni zake alizoanzia Kanda ya Ziwa, kwenye mikoa ya Geita, Kagera na Mwanza, JK ametoa ahadi kede kede ambazo zilijenga mazingira kuwashawishi wapiga kura kumchagua. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, toleo Agosti 26, 2010, imeripotiwa kwamba alipokuwa mjini Katoro, Kikwete alilazimika kumtumia Waziri wa Nishati, William Ngeleja, kuwaelezea hatua ya Serikali iliyofikiwa kuhusu umeme kupelekwa kwenye mji huo, jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni "rushwa", kwani Ngeleja alilazimika kutoa ahadi kwamba umeme utaanza kuletwa mjini hapo kuanzia Januari 2011. Hili lilifanyika kwa lengo la kuwashawishi wananchi wa mji huo kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi, jambo ambalo limebainishwa kwenye Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi ya 2010 kuwa ni kosa, kwa mujibu wa sheria hiyo.

  Ina maana kwamba, Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi ya 2010 INAKATAZA wagombea wa nafasi za kuchaguliwa, udiwani, ubunge na urais, kutoa ahadi kwa lengo la kuwashawishi wananchi kuwapigia kura. Kikwete amemtumia Ngeleja kutoa ahadi kwamba iwapo wananchi wataipigia kura, basi, miundombinu ya umeme itaanza kuwekwa mjini hapo na kwingineko karibu na hapo, kuanzia Januari 2011. HII NI RUSHWA!

  Wewe mwananchi unayejiheshimu, unayeipenda nchi yako, una wajibu wa kutoipigia kura CCM kwa kuwa inatoa ahadi kushawishi kuchaguliwa. Haya tayari yamebainishwa kuwa ni makosa kisheria, na Tendwa anapaswa kumuengua mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kwa kuwa tayari ameivunja sheria aliyoisaini kwa mkono wake mwenyewe, akiwa Rais.

  Iweje "rais", kiongozi wa nchi, awe wa kwanza kabisa kuvunja sheria aliyoiridhia mwenyewwe, tena kwa mbwembwe zote, kule Ikulu? Kumbe ulikuwa unafiki?

  Atakayesema ya Ngoswe aachiwe Ngoswe ana lake jambo!

  Tusitarajie utawala bora kwa mwendendo huu. Hakutakuwa na mabadiliko yoyote yale katika Awamu ya Tano!

  Uongo uendelee!

  --> Mchokonozi <--

  Kura kwa Dk. Slaa TU!
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kikwete might have never done anything to be trusted so far, je hivi slaa angekua kwenye serikali kama presiding president, angekwepa ktumia rasilimali anazotumia JK?
   
 3. M

  Mchokonozi Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpe nafasi uone kama atafanya au hatafanya!
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Hata akivunja sheria Chief Justice kamteua yeye, IGP kamteua yeye, Magereza, PCCB nk. Tukubali tu tumepigwa mchanga wa macho
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Suala ni whether ni sahihi au sio sahihi kutumia raslimali za walipakodi (majority of whom sio wana-CCM) kwa minajili ya kura.Naelewa logic ya swali lako lakini put it this way: as part of defence, mwizi amuulize hakimu angefanya nini if he were in their shoes!
   
 6. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  Sheria ya uchaguzi ni mahususi kwa wapinzani na wasio kwenye mtandao tu
   
 7. b

  bobishimkali Member

  #7
  Aug 27, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jakaya kikwete hakutoa ahadi ili kuwashawishi wananchi wamchague tena, ila alikuwa anawaelezea wananchi mipango aliyokuwanayo ambayo anakusudia kuitekeleza endapo atapata tena fulsa ya kuongoza nchi. Hata nchi zilizoendelea kama USA, UK nk.wakati wa kampeni wagombea huelezea mikakati na mipango waliyonayo ambayo watatekeleza endapo watachaguliwa.Hivyo KIKWETE hajavunja sheria
   
 8. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wewe mbona unarukia jambo bila kulielewa...soma na huelewe kwanza kabla ya kuanza kuchangia...unaambiwa sheria aliyoiridhia mwenyewe yaani Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi ya mwaka 2010 inakataza vitendo vya kutoa ahadi na kujinadi kwa mtindo huo...wewe unaanza kuelezea habari za USA.Kwani wamarekani wakifanya lazima na Tanzania tufanye?Yaani mfano mzuri wa Demokrasia ndo huko Marekani?
   
 9. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Huo ndiyo ukweli wenyewe na ambaye alitarajia kuwa Sheria ya Uchaguzi itawabana CCM ni kipofu. Kwa upande mwingine mimi naona kama CHADEMA wako passive sana. Kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na CCM au vyombo vya dola kwa maslahi ya CCM ambavyo yanaweza kuwa-challenged mahakamani lakini hatuoni hatua yoyote inayochukuliwa. Kwa mfano pingamizi za CCM dhidi ya wagombea wa upinzani. Inaonekana kana kwamba pingamizi za CCM zikishakubaliwa inakuwa basi ndiyo mwisho. Matokeo yake CCM tayari ina magoli kibao hata kabla ya mechi kuanza. Kwani CHADEMA na vyama vingine hawana wanasheria wa ku-challenge pingamizi hizo? Wapi Tundu Lissu? Kuamini kuwa sheria hizi zinatungwa kwa ajili ya kutenda haki ni kujidanganya. Na kama CHADEMA wako tayari kucheza mchezo ambao wanajua matokeo yake toka mwanzo wanawakatisha tamaa watu wengi sana.
   
Loading...