JK AUZA NCHI KWENYE MNADA!

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Ndugu zangu wana bodi,
Ebu tubadilishane mawazo kwenye hii issue! Je, mwaionaje?..
1. Tupo tayari kuukabiri Ubepari? au ndio tumeisha yavulia maji nguo!
2. Wakati nchi za magharibi wanajaribu kila njia kuziba nguvu za mashirika makubwa sisi ndio kwanza tumefungua tena mnadani...
3. Ikiwa wahindi matajiri Uchwara na hao Wa shona weupe wameweza kushika nchi kiuchumi na kuleta madhara kwa wafanya biashara wadogo, je tunaweza kushindana na haya makapuni?

Kuna faida zake tena nyingi, Sii muda Dar itakuwa NY ya Africa kama ilivyokuwa Kenya kabla na baada ya Uhuru. Mashirika yote haya yamekuwepo hapo zaidi ya karne na sijaona maendeleo kwa Wakenya.
Ajira kwa wasomi kibao zitakuwepo lakini ni asilimia ngapi TZ wamesoma hadi leo!... chini ya 20%. Je, kuna sheria gani zimewekwa na serikali kuwalinda wananchi kibiashara kabla ya hayo mashirika hayajaanza kuingia?
Kazi kwenu wanabodi nipeni mawazo yenu!
 
Mzee Bob,

Hili suala halijadiliki, maana hata BM huko aliko in private nasikia hucheka sana anapowasikia kina JK na EL wanapopiga piga kelele, na yeye huwaita marais wawili kwani yeye anasema anelewa kuwa hawatafanya kitu zaidi ya kelele tu zamlango,

Tunafuata siasa gani sidhani kuna kiomgozi hata mmoja wa bongo anayeweza kusema ukweli kuwa kwenye hili hatuna lolote ila tupo tu!

Binafsi ninasema sasa ni Mungu tu nisaidie, serikali yetu leo imejaa who knows who! Sio tena Who knows what! As much as I have a problem na siasa za Mwalimu, lakini angalau chini ya mzee tulikuwa tunajua tunasimamia wapi, na mimi binafsi nilisoma bureee, na warrant ya shule ile ya treni na basi niliikwaa sana, basi tu sometimes sina shukrani na Mwalimu, unajua Biblia inasema kuongeza knowledge ni kujiongezea sorrow, Watanzania ndugu zangu we are stuck!

Haya mambo ya mashirika makubwa sisi we have absolutely no idea nini kinaendelea, Bob na wengine nafikiri mmesoma kile kitabu cha Economic hit Man, now yale ni mambo ya 1950s na 1960s! Sasa niambie leo 2006 hao kina hit man wanafanya nini? Na sisi tunafanya nini?

Sasa hivi tuna viongozi wezi tu na siasa hatuna kabisaa, tena sasa nimeshaanza kukata tamaa na mzee JK, kuwa hakuna lolote kama anvyosema mzee BM, as much as I hate him lakini ana point "......hawa MARAIS wawili kazi yao kelele tu unafikiri wataweza?......"
 
Mkandara, Mzee ES
Mimi pia sina tatizo na ubepari as such. Lakini ukiona nchi zote zilizoendelea zilikuwa na mfumo wa kuretain capital. Sisi capital yetu inavuja left and right.
There is more money leaving Tanzania than that is coming in. Nimewahi kusema elsewhere kuwa jiji la Johannesburg lilijengwa kwa dhahabu. Skyscrapers, highways, driveways, what have you. Je sisi at the end of the day, ile dhababu ikishamalizika kule Bulyankulu, miji ya Kahama, Geita itaweza kufanana na Jo'burg? Wenzetu ulaya wamejenga miji yao kwa kukomba nchi za nje: Africa, Latin America. Sisi hatuna mahali pa kukomba na kile kidogo tulicho nacho tunawaachia wakombe. Tunahitaji ubepari ambao utatuwezesha ku-retain our capital na si kwenda kuwatajirisha wenye hisa mijini Toronto, Washington na Houston. Je, tunao uongozi unaoweza kutupeleka huko?
 
Mzee Es,

Umesema kweli sana tu isipokuwa dhana za Mkapa siwezi kuzisikiliza. Kwa sababu mkosa hawezi kumtoa makosa mtu.. Ikiwa kweli mtu anaamini 2+2 ni 22 na mbishi kukubali jibu la 4 kwani haoni uhusiano kati ya 2 na 4, huyu mtu hawezi kabisa kutoa ushauri wa maana. Mkapa bado anaamini jibu ni 22 na anachotegemea JK kufanya ni kuleta hilo jawabu ambalo kwa eli yake Mkapa haliwezekani na mtu isipokuwa yeye mwenyewe.
Tukirudi kwa JK mimi hofu yangu kubwa ni hawa jamaa wa mnadani ambao hawana sheria zaidi ya utajiri na hasa one way traffic ya biashara!..Hii ni kamali ya biashara inayotuhusiwa, utalishwa zako kwanzaaa kisha watafumua na tutarudi watupuuu!

Jasusi,
Mshikaji umesema yote!... Hii ndio hofu yangu kubwa na wala sio sisi hata mabepari wenyewe wanayaogopa mashika haya ya Mnadani tena toka nchi za nje, kwa sababu kazi yao kubwa ni kuvunja nguvu vijikampuni vyote vidogo nchini humo na kuushika uchumi wa nchi. Kazi yao kununua makampuni dhaifu hali makao makuu yapo US na soko lao lipo Nasdac - Marekani. JK aulize Canada wanavyolia, leo hii hawana hata sauti na hata serikali yao sasa hivi hawana budi kumsikia Marekani.
Sasa hiyo Dar stock exchange itakuwa na kitu gani? maanake nina hakika kitu cha kwanza kabisa watu hawa watayapigia speed mashirika yanayozalisha na yenye faida kubwa. Mafahari wengi watageuza TZ uwanja wa mapambano na sisi nyasi sijui kama tutabaki salama...

Naukubali sana ubepari iwapo sisi wenyewe tupo tayari na hasa ikiwa sisi ndio tutakao endesha mfumo huo yaani kuwepo na two way traffic ya kibiashara na nchi za nje. Na hii mikakati ya kuinua miradi midogo midogo (small business) ina mwisho mbaya sana kwa wananchi, tumewashindwa wahindi ambao ukifungua kitu tu wao wanajaza duka... Ebu angalia biashara ndogo ya muziki tu ambavyo wanawanyanyasa vijana. Master tape inanunuliwa kwa elfu 20 lakini hao wahindi wanatengeneza faida mara 1000 hali Bamuta wanao mtambo mzima wa ku - record na kufyatua toka enzi ya Mwalimu. Wamehakikisha haufanyi kazi za biashara zaidi ya mazoezi kwa Twanga pepeta.
Labda Jk kaona dawa ya moto ni moto!... ili kuwaondoa hawa wahindi na vitu vyao feki bora kumleta mnyonyaji na mwizi mwingine ambaye ataiba sawa na mhindi lakini tumebakiwa na majumba kama Maputo huko Msumbiji.
 
Mkandara,
Kama Unayosema ni kweli, watanzania tutakuwa tumewekwa pabaya sana!

Maana mabepari hawana huruma. wanachotaka ni monopoly na kupata faida kubwa!

Kama JK hakulifirikia hilo la ushindani inabidi aangalie sana, He has to think twice! na kama ni mikataba ianadaliwe kwa makini zaidi.

Maana hao matajiri wanaweza kumharibia mipango yake yote ya kutuletea mafanikio. Na hapo huyo mjuaji BMW hana haya atapata pa kusemea zaidi.

Kama ni kweli BWM naye anasema sema huko, tunamshauri aache kabisa.

BWM anaamini kuwa watz wote hawajui kitu ila ni yeye tu na akina K!

ni kweli yeye 2+2 =22, akae kimya vinginevyo anaendelea kutuudhi zaidi. Anaweza kuitwa mahakamani siku za baadaye. Labda madhara ya mikataba yake yadumu kwa muda wa miaka 10 tu!

Ninashauri, madhara ya hiyo biashara ya mnadani yawekwe wazi na wachumi wamshauri JK ili akikataa, anaweza naye anaweza kuwa na kesi ya kujibu hapo baadaye. Lakini wahindi nao na vitu vyao visivyo na standard na tabia yao ya kutopenda kulipa kodi itakuwa imepatiwa dawa.
 
Hebu tujiulize kidogo hapa:

Hivi mafuta yanasaidia vipi serikali za Kuwait, Saudi Arabia, Bahrain, na UAE kuwahudumia wananchi wao? Wenzetu chanzo chao kikubwa cha fedha za kigeni ni hayo mafuta.. je wabongo chanzo chetu kikubwa ni nini? Bila ya shaka tuna Utalii, na Madini! je hivi viwili vinasaidia vipi katika kuinua maisha ya kawaida ya wananchi? Maoni yangu ni haya:

a. Makampuni yote yanayochimba madini, badala ya kutoa msaada wa maji, umeme, shule, na hospitali peke yake... waanze kujenga nyumba nzuri za vijiji vya karibu!! au sehemu ya mapato yao yaende ili kuborosha makazi. Ina maana gani kuwa na kampuni yenye mabilioni ya dola halafu upande wa pili kuna watu wanaishi kwenye vibanda vya makuti na kutumia visima vya kuchimbwa?

b. Serikali ianzishe mfuko or something like that... ambayo itakusanya fedha angalau bilioni tano kila mwezi na kuziweka katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu kama wanavyofanya kwenye barabara. Hizo ziwe ni fedha zetu siyo za misaada. Je hilo linawezekana? Ni nyumba ngapi zinaweza kujengwa Mbeya, Mtwara, Kigoma etc kwa kiasi hicho kila mwezi?
 
Mwanakijiji,
Kuna njia mbili kuu za kuifanya serikali na wananch wafaidike na na hii miradi (Kwa kuongezea tu na ile ya community development):
1. Mineral Benefication - Serikali ingepigania sana mineral benefication. Hili hata Mkapa alisisitiza sana. Sijui hiyo mikataba ina sisitiza nini. Katika migodi hii ya dhahabu imefahamika kuna copper nying sana inauzwa through agent wa barick gold Australia as mineral concentrate, na hawa wazungu wanasema hawana facilities za kuchambua Tanzania. Na wataalamu wetu feki hawa waki-Tz wanaona tu.

2. Tangu mwanzo zingewekwa clauses kwenye mikataba kuwa baada ya muda fulani Serikali husika inunue shares au wananchi/communities/ indigenious companies wanunue shares.

Kwa kuwa hatujui mikataba imeandikwa nini, hapa ni pa-gumu.

Hata huko uarabuni (nci ulizotaja)ni hawa hawa westerners ndiyo waliowekeza, lakini refineries katika nchi hizo zimeshikiliwa pamoja na aidha wenyeji au serikali au watawala, kampuni kama Aramco, Kuwaiti Oil, etc. Hawa jamaa kutokana na mapato yao hayo wameweza hata ku-control Citibank (the largest bank in the world).

Suala hapa siyo ubaya wa ubepari, ni mikataba yetu, upimbi wetu, it happens only in Africa. Usilaumu dobi, kaniki ndiyo rangi yake!!
 
Mengi sana yamesemwa nami natia kaneno kadogo tu .Jibu la mambo yote haya ni pale Wazalendo watakapo amua kuweka uzalendo na kusema I am Tanzanian and will remain Tanzanian piga ua .Hapo tutaona mabadailiko ya kweli na hawa watu wa mnadani wataambiwa kwamba hapa ni Tanzania na kila kitu kiwe nusu kwa nusu na Watanzania kuliko ilivyo.We need to drop politica opportunities.Baki kiongozi wa Watanzania pata heshima kwa Watanzania na si wazungu.Hapa ndipo ilipo shida .

Wawekezaji wengi wanashirikiana na akina Malecela, Msekwa , Kigoda , Lowassa, Rostam ,Sitta nk hapa kazi iko kubwa hatutapata kitu na watabakia matajiri wakubwa na watu wenye nguvu na influential kwenye siasa na Serikali hapo tumeisha .Jamani sisi tunayaona haya je wao unadhani hawajajiuliza maswali kama haya kabla ya kuwaita watu wa mnadani ????????????
 
Ndugu zangu
Sisi watanzania ni malimbukeni......hatujiamini wenyewe kwamba tunaweza kuleta mabadiliko. Wanasiasa wanahubiri lakini hawaamini hayo wanayohubiri. Basi mambo tu.

Ubepari kama mfumo, sidhani kama ni tatizo. Nchi nyingi zimefanikiwa katika mfumo huo. Kama nchi ina sheria zinazofanya kazi, hayo mashirika au makampuni makubwa ambayo bajeti yake kwa kampuni moja tu kama Microsoft au HSBC au Chevron ni kubwa kuliko bajeti ya nchi kadhaa za kiafrika kwa pamoja, yanaweza kufanya kazi na kuleta manufaa kwa nchi husika.

Biashara au uzalishaji ambao nina uhakika nchi kama Tanzania ingenufaika nao ni partnership. Suala la kuwauzia wageni biashara nzima ni somo tulilokwisha jifunza.
 
Mkandara said:
Mzee Es,
....Labda Jk kaona dawa ya moto ni moto!... ili kuwaondoa hawa wahindi na vitu vyao feki bora kumleta mnyonyaji na mwizi mwingine ambaye ataiba sawa na mhindi lakini tumebakiwa na majumba kama Maputo huko Msumbiji.

Mkandara,

Sidhani kama atakuja bepari (eti jina zuri ni muwekezaji) kutoka nchi nyengine halafu aanze kuijenga bongo kama Cape Town au Maputo, Harare nk, karne ile ilishapita. KIlichofanya wakajenga ni kuwa kipindi kile walikuwa wanajaribu fuhamishia luxury za makwao (ulaya) katika makazi yao mapya (africa) kwa sababu moja kubwa ilikuwa haiwezekani kuendesha kiwanda au machimbo kwa "remote control", sikuhizi inawezekana. Yaani safari kipindi hicho zilikuwa zinachukua wiki au miezi kwa meli hivyo ikabidi makazi yao mapya ya afrika wajaribu kuyajenga yawe kwenye standard, miaka hii hilo si tatizo, wanaweza wakawa wanaishi Washington, Jo'burg au London na wakawa wanaona kila linaloendelea kwenye machimbo au viwanda vyao, sasa je kwanini waje hapa bongo waumwe na mbu? Mifano ya karibu na kama wanavyosafirisha containers za michanga/ madini ili wakachambulie kwao.

Pia wawekezaji wengi weshajanjaruka, mambo ya kuweka mayai yao kwenye tenga moja hawawezi kurudia tena, kwani mambo kama azimio la arusha, mugabe na hao "war veterans", au enzi za Idd Amini alivyotimua watu uganda pia imechangia wawekezaji kutojiingiza africa kichwakichwa...Si mnaona mwenyewe africa kusini wazungu wanavyoondoka? je mnadhani watarudia kujenga nchi nyingine?

Kitu kikubwa kinachonifurahisha kwenye huu mjadala ni uzalendo wa wachangiaji, ila swala ni kuwa wangapi tukipata au kupewa ulaji uzalendo wetu utakuwa na msimamo huu huu?? Wengi wetu tunalalamika kwani tupo kama watazamaji tu upande wa pili, tunapopata huo uongozi basi tunahama kambi.

Tukisoma magazeti yetu mengi mtu akipandishwa cheo wanamwandika "....FULANI KAULA...." hii ni kasumba ya kupenda kula au kudhania ukubwa na ulaji tu na sio utendaji au uwajibikaji na kwa sababu hii ndo maana mtu akipanda cheo tu watu wanategemea atakuwa ma pesa nyingi, magari na nyumba nzuri, kwa akina yakhe pia ni kuwa na ma binti wengi tu nje ya ndoa (nyumba ndogo)!! Nimeshangaa eti hadi leo hii watu wanatoa rushwa ili wepewe vyeo na wala hakuna anayeshtuka je mtu anayetaka cheo kwa udi na uvumbi ana nia njema kwa taifa lake??

Tukirudi kwenye topiki yetu ni kuwa matatizo ambao tunayapata watanzania na waafrika ni ule ujinga na ushamba uliokithiri ambao ndo unaotufanya tutapeliwe na kila tunaeyekutana naye alimradi tu awe na rangi tofauti ya ngozi.

Tanzania na Afrika itajengwa na wa tanzania na waafrika wenyewe, hao mabepari tunaowaita wawekezaji au wafadhili watakuja kuchuma na kurudi kujenga kwao tu. Na tusipoyafungua macho yetu basi tutaendelea na kutaabika kwetu tukitegemea eti mtu baki asiyetufahamu atafika atusaidie na kutotoa kwenye shida zetu na kwa hilo tutasubiri hadi siku ya maisha yetu (kiama).

choveki.
 
Ndg Mkandara na wachangiaji wengine,

Ubepari upo na unaendele kuimarika kwa nguvu zote, na hayo ni mafuriko yanakuja, wengi wetu tutabaki kuwa maskini, na wachache watapeta, na huo ndio mwelekeo wa serikali yetu "fukutu" (maana sio "tukufu" tena).
nina maoni yafuatayo on the way forward

1.Tupige kampeni za kutosha ili mikataba ijayo iwe WAZI na kwa manufaa ya waTZ

2.Mikataba tuliyonayo (ambayo hatufaidiki nayo), naishauri serikali ya JK, ifanye negotiation upya kwa malengo wote tufaidike

3.Kwa kuwa wengi wa wafanya kazi kwenye site nyingi za rasilimali zetu ni waTZ, basi serikali ichukue/iweke mikakakti inayotekelezeka kwa kuwawezesha waTZ. (tuige mfano wa China na India wanavyowawezesha wananchi wao mpaka westerners wanawapiga makelele, ila hahao westerners wamesahau "banzi" lao la kutoa subsidy kwa wakulima wao).

4.kuna areas ambazo ni critical kwa kukuza uchumi wetu especially kwenye production iwe viwandani, migodini, na mashambani na pia kwenye tourist industry. Nakumbuka enzi zile za JKN akisaidiwa na Elinawinga waliweka mikakati mizuri ya kuwawezesha wananchi kielimu ili kupata wataalamu wetu wazalendo, wengi walienda Urusi (udaktari), India (wahandisi) huko India ilibidi serikali yetu ijenge hostel kwa ajili ya waTZ, hiyo ni mifano michache tu ya kuwawezesha wananchi kiutaalamu ili waje kuongoza uchumi wetu. Sasa hivi eti tunasikia tunaleta wawekezaji kuja eti kuendesha TANESCO!!!!!!, eti hatuna uwezo wa kusafisha madini yetu hapa nchini!!!!! (wakati wa JKN "atleast" alijenga kiwanda hapa hapa TZ cha diamond)

JK weka mikataba WAZI iliijadiliwe kwa kina, pili WEZESHA wananchi ili tujenge uchumi wetu
 
Ogah, umesema ukweli,

JK aweke mikataba wazi! kwa nini hawataki wanachi waijue mikataba na ni wanachi hao hao wanaothirika au kunufaika na mikataba?!!!

Kuna wakati fulani Mramba alisema mikataba ni siri kati ya serikali na wawekezaji!!

Kama hakuna ulaji mikataba itwekwa wazi lakini ulaji ukiwamo wajinga ndio waliwao!

Nchi kama Botswana ilitumia Ford Foundation na wamefanikiwa sana maana Ford Foundation huwashirikikisha wananchi katika ngazi zote!! kwa hiyo unapofika wakati wa utekelelezaji wa miradi au mikataba kila mtu anakuwa anaelewa kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa! Lakini hawa IMF and World Bank!
Na wana maisha mazuri kwa kutumia raslimali zao vizuri.
Lakini wa kulaumu ni viongozi wetu wanaweka mbele kwanza matumbo yao, wakati masilahi ya taifa hakuna kabisa! hata sisi tunapiga kelele tukipewa huo unaoitwa ulaji basi!!! kelele zinaisha. VIONGOZI BADILIKENI YATAWATOKEA PUANI SIKU ZA BAADAYE!

Cha ajabu wanaosema mikataba ni siri wao wanaonekana kuwa matajiri kupita kawaida! mafano NBC iliuzwa karibu na bure!! lakini baada ya muda mfupi ABSA walitengeneza faida kubwa sana kama mara tatu ya gharama walizonunulia. Mramba alipohojiwa na BBC kuwa kwa nini hawa jamaa wameuza asilimia 15% tu ya share zao na kupata faida kubwa kiasi hicho!!!


Jibu lake lilikuwa NINI CHA AJABU HII BIASHARA HURIA BWANA!!!

TUMEKWISHA TUAMKE BEFORE IT IS TOO LATE, TUWAPELEKE AKINA MRAMBA MAHAKAMANI ILI WAJIBU HAYO MAJIBU. NA TUWAULIZE KWA NINI MIKATABA HAIKUWA YA WAZI!! LABDA MNGELIUZA KWA BEI NZURI!
 
Wazee wote wachangiaji,

(1). Mimi ninasema kuwa ni vigumu kuwa on top ya mikataba ambayo hata wewe kiongozi you have no idea faida na hasara zake, na that is the case na viongozi wetu ni lazima tukubali kuwa hawaelewi kinachoendelea, kuanzia kwenye uchumi, Afya, mikataba, wao wanachojua ni kampeni za siasa tu!

(2). Mabepari ni binadamu ambao wanajali masilahi yao na wala sio ya nchi zao, na serikali kama za West zina sheria kabisa katika vitabu zinazoisukuma serikali kuwa involved katikia kuyasaidia mashirika binafsi ya biashara, yanapokwama nje ya nchi kama zetu, lakini hawa wafanya biashara binafsi ni lazima tujiulize kinachowakimbizia kwetu ni nini? Ni kwa sababu kwetu huku hakuna sheria! Hivi majuzi kampuni moja ya US ilienda kuutupa uchafu wao wa mafuta huko Guinea kwa kuilipa seriakli dola 600,000 tu! Kule kwao kwa sheria za environment ingewacost kama millioni dola 3, waziri wa Guinea alipoulizwa alijibu kuwa we needed the money, alipoulizwa kuhusu madhara ya afya ya ule uchafu akasema tusipokufa kwa uchafu huu wa US, tutakufa kwa njaa ni afadhali tufe tukiwa tumeshiba! Unafikiri kuna tofauti ya hao wa Guinea na bongo? Mara ngapi unga na mchele mbovu unauzwa tu mitaani kwa kuruhusiwa na serikali? Viongozi wetu hawana idea na mambo mengi wanayoyapitisha kwa kushinikizwa na mashirika ya biashara!

(3). Sasa hivi mashirika ya nje ya biashara yamekuwa na ujanja sana, kwani yote yanapitia South Africa, kule yanapata mashirika mengine ya kuwa front na kuja bongo kwa niaba yao, haya ya south Africa yanatujua sisi waafrika nje ndani kwa yanapata deal kiurahisi, maana yanajua kuwa hatujui lolote na tuna njaaa, jamani niambieni ATC tumeshuhudia mara ngapi ikibadili mikataba na hakuna lolote? Sasa hivi Tanzania tuna viwanda viwili tu ambavyo angalau vinaendeshwa na mashirika ya nje lakini yanatuletea faida kidogo nayo ni Bia na Sigara, lakini hata hayo mawili utashangaa kusikia hayo mashirika yanavyotengeneza hela, na hakuna kitu chochote cha ajabu yanachofanya kuendesha hivi viwanda,

sisi tulishindwa, sasa kama Guntram Itatiro walikirun hichi kiwanda cha bia to the ground wakaenda mapak kuwa mawaziri ili wafanya nini tofauti? Mwapachu ATC ilimshinda kabisaa sio siri leo ni waziri, Mungai ATC neye imemshinda kabisaa leo ni waziri ili afanye nini tofauti, yaani mifano ya kwa nini tunamatatizo tunayo kibao ni kwamba viongozi wetu hawafai na hawaelewi hii mikataba faida na hasara zake, hata kuwashauri ni kazi ya bure je kuna wataalamu wangapi hapa bongo? Ukiwakuta hawa wataalamu bungeni utafikiri kuwa nikweli kumbe ni uozo tu!

Kiongozi safi ni watu kama Kaduma ambaye ninajua kuwa aliendesha NMB kwa kiutaalamu na ana uwezo, kina Sumaye Kigoda na wenziwe wezi na mashirika toka South Afria, wakamshabikia kwa Mkapa ili afukuzwe kazi na wauze NMB kwa makaburu, mpaka siku Kaduma alipoitwa pale bungeni kueleza ukweli ndio viongozi kushituka kuwa hawa kina Sumaye ni wahuni, sasa ulitegemea mtu kama Kaduma awe nafasi kubwa katika serikali yetu katika kuangalia hii mikataba, NO! hata hiyo NMB alifukuzwa na Mkapa,

Ubepari hauna tatizo lolote kwa sababu unajali faida tu, sasa na serikali ni lazima iipiganie nfasi yake katika ubepari nayo ni kukusanya kodi na ajira kwa wananchi, leo kule US majengo kama Rockfeller Center yanamilikiwa na shirika toka Japan, lakini seriakli ya US inahakikisha kuwa hakuna hata senti moja wanaikosa kuitoza kodi, na kuna sheria za nchi kuwa only CEO ndiye atatoka Japan otherwise wote watakuwa wananchi wa US, Tanzania ni lazima ufike mahali tuwaheshimu na kwainua wataalamu wetu wa kweli kwani wapo ila hawapewi nafasi kwa sababu political system yetu imejengwa kwa ajli ya mkao wa kula. Mzee JK kabla ya kuingia alikuwa na mipango mingi kabambe lakini na yeye ameshaingia kwenye ile ile system ya kukaa na kusubiri a miracle, baraza la mawaziri ni bovu mno ni afadhali makatibu wa wizara wangebadilishana na mawaziri, otherwise tunaelekea shimoni tu!
 
Great Mzee ES! let me call you kijana ES!

tukipata watano kama wewe ndani ya chama nina imani hatimaye ndoto za watanzania zinaweza kutimia tu bora uzima. Hakuna haja ya kusarenda. Kwa kweli kama JK akishindwa kutatua matumaini ya watanzania angalau kwa asilimia 50% itakuwa mbaya zaidi!

(1) bila aibu akubali kupitia mikataba YA MADINI UPYA.
(2)nyumba zote walizouziwa hao wenye uwezo wa kujenga zirudi maana si zake ni za watanzania. Unaona kutangaza tu kuwa hatauza wananchi wamefurahi sasa akiamua zirudi itakuwaje? Furaha itakuwa mara 50.

(3)Waliohusika na IPTL wafikishwe mahakamani au angalau amufukuze Mary Ndosi toka ofisi ya mwana sheria mkuu..

(4) Angalau apangue upya PCB. Kamazima akae nje.


(5) Amalize au kupunguza kwa asilimia 70 tatizo la umeme kwa kutumia hiyo Gas na grid ya Zambia. Na tatizo la maji sijui hapa atafanyaje?

(6) Asikubali kupeleka jeshi letu Darfur labda DRC! vita ya Darfur haitafanikiwa maana serkali ya Sudan yenyewe inhusika moja kwa moja! ya nini afikirie kupeleka jeshi eti kama UN italipia Gharama. Ni upuuzi maana Maana Serilali ya Sunani ni wapuuzi tu! Ya nini apeleke ndugu zetu kwenda kuuawa na Serkali ya Sudan! katu asikubali.

(7) wasikubali upuuzi wa Mseveni wa makasudi wa kutumia maji ya ziwa victoria zaidi ya kiwango chake kwa makusudi tu! UGanda ni tatizo EAC! Lakini hii si topic yake hapa!
 
Ndg Mkandara na Wachangiaji

Nimeona hapa kuna watu wana mawazo mazuri sana kuhusu nchi yetu, itakuwa ni vyema hawa viongozi wetu wakawa wanapewa hivi vipande/vidonge.

Nini maana ya tatizo??, inaelekea kama sikosei watu wengi hatujui maana ya tatizo. nijuavyo mimi ...........tatizo linakuwepo pale ambapo malengo yako ni kupata maksi angalau X BUT unapata < X (i.e less than X). kama kuna mwingine mwenye definition nzuri na aiweke.

Kuna waTZ wana mawazo mazuri sana ili kuijenga nchi yetu, BUT viongozi wetu either ni kiburi au hawajui kama kuna mawazo mazuri na ya neema kwa nchi yetu.........therefore, tunahitaji ku-bridge hiyo gap, na kwa kuanza napenda kusema yafuatayo. Ubepari ndio huo na hatuna budi na sisi kuweka mikakati ili tufaidike nao

1.WaTZ walioko nje, kwa kifupi huijenga nchi yetu kwa saana tu, wengi wao hutuma pesa nyingi sana nyumbani ambazo kama wengekuwa TZ wasingeweza ku-raise hizo pesa, kwa hiyo nawapongeza sana waTZ walio nje wanaorudi kuleta maendeleo huku nyumbani... keep it up.

2.waTZ walio nje na tulioko nyumbani tuwe aggresive zaidi tufikie kwenye level ya kuwa investors/wafanyabiashara makini. Kwa mfano. mTZ unayeishi kihalali nchi Y, fanyeni utafiti na mufungue ofisi ya biashara/soko ya mazao yetu kama lets say chai/pamba/korosho nk mkishirikiana na wenzenu huku TZ.

3.serikali yetu iwe mstari wa mbele kuwasaidia ktk kufungua ofisi kama hizo waTZ(kuwezesha), hii itaepusha mazao yetu yasiharibikie mashambani bali yauzike nje. “Here good proposals are eminent”

4.Wakulima wa kawaida nao wawezeshwe kununua share za makampuni hayo ya kibiashara (yawe ya wazawa au ya wageni), in a simple terms za kibiashara.

5.Ziundwe district investment councils kwa ajili ya kuhamasisha wakulima kuingia ubiya kwenye biashara. Mkulima wa kawaida mfugaji, ukimwambia ukitoa ng’ombe wako wawili utapata ng’ombe eg wanne zaidi mwisho wa mwaka, hiyo ni language ambayo wataelewa kirahisi, badala ya kuwapelekea language za akina stock exchange

6. Kama kweli Shell wanakuja, na kukiwepo na hayo mafuta, hatutaki kujutia yanayotokea Nigeria sasa hivi. Tunataka share nzuri kwa faida ya wananchi wa TZ.

Viongozi wetu, please, kama mnavyo wawezesha watoto wenu nyumbani kuingia ubiya na investors wanaokuja wawezesheni na waTZ wengine wanaowania kufungua ofisi kw ajili ya uwekezaji TZ kama hao wazungu wanavyokuja!!
 
Wanabodi hii,
Kwanza nawashukuru sana kwani darasa hili kubwa sanaaaa. Limenufumbua sana tu na labda niseme Watanzania wote kwa ujumla wana wasiwasi kubwa na Sheria za nchi ikifuatiwa na viongozi..

Nimesoma mahala fulani kama sio maoni-org kuwa JK kaweza ku-raise mabillioni ya dollar nchi za nje kuja saidia TZ. Sijui kuna kati yetu anayefahamu mikataba iliyowekwa ktk upatikanaji wa hizo fedha?... ikiwa hakuna basi hilo moja kukamilisha hofu kubwa ya pili ya ndugu yetu Interested Observer. Hapa kilichobaki ni kuomba Mungu JK atumie mikopo hiyo sehemu ambazo tunapenda ama niseme tunafikiri atakuwa kazipa kipaumbele. Lakini tukumbuke ndio kesha saini mikataba na hao jamaa nasi hatufahamu kilichoambatanishwa na hiyo mikataba wala wapi fedha hizo zimekusudiwa kutumika ktk hayo makubaliano.

Nadhani sote tumekubaliana kwamba Ubepari hauwezi kuepukwa isipokuwa ni jukumu letu kuweka sheria ambazo hazipindiki na zenye malengo ya kuiendeleza nchi. Nd. Mkira Ford foundation wanayo NGO yao hapo kwetu inaitwa Economic and Social Research Foundation kwa kifupi ESRFTZ na site yao ni hii esrftz.org. lakini Botswana hawakuweza kupata mikataba bora kutokana na hawa jamaa ila kuna mshenzi mmoja nimesahau jina lake. Huyu jamaa ni mstaafu alikuwa benki kuu ya dunia. Huyu jamaa aliandaa mkataba mpya na kuiweka kona IMF na benki kuu hadi Botswana wakapata hiyo 50% kwa kila deal la Almasi. Mshirika kama huyu sio rahisi kumpata labda hatua inayotakiwa ni kutafuta watu kama hawa..
Pili, Hadi hapo itakapo fikia kwamba mikataba inawekwa kati ya serikali yetu na wageni badala ya wageni na Lowassa ama JK itakuwa kazi kwetu kuweza kupata mkataba wa maana. Nikitazama kwa uharaka maoni yetu sote humu ndani inaonyesha wazi kwamba mikataba yote nchini inawekwa na viongozi kwa faida ya Uongozi ama viongozi hao, kisha swala la nchi linafuatia bila hakika ya mafanikio. Kila mtu anapopigania kupata nafasi ya uongozi serikalini sio kwa sababu anataka kuongoza ila uhakika wa KULA yake, hayo matatizo ya nchi yameshindikana toka JKN.
Hii inatisha sana na kama sheria haitaweza kusimama na kutatua tatizo hili sidhani kama ukaribishaji wa wawekeshaji kwa njia yeyote ile unaweza kutusaidia. Na mbaya zaidi ni kwamba hao tunaowakaribisha sasa hivi ndio mapenzi yao makubwa. Fungueni vijikampuni vyenu kwa misaada ya serikali na kadhalika lakini siku watakayo ingia jamani mmekwisha!...Oneway business traffic hata siku moja haiwezi kuwa na mafanikio kwa nyasi...Kwa sababu Microsoft wanawekesha China sio kwa sababu China inayo maliasili ya kutengeneza chips ila cheap manpower. Kwa wachina wao ni faida tupu hawana technology wala mchanga isipokuwa labour!.. na chips zote zinasafirishwa kama mali ya China..exports! Haya ukiangalia waarabu mafuta ni export na serikali zao (hao masultan) wana asilimia kubwa tu ndani ya mashirika ya nje! Tena basi haohao waarabu wamewekesha ktk makampuni ya ugawaji mafuta hata nchi za magharibi.
Lakini tazama Bongo basi, nguvu yetu inaishia ktk ajira na ruzuku. Pamba, Kahawa, dhahabu, Almasi vyote vinaondoka kama malighafi na kurudi kwetu kuuziwa baada ya kutengenezwa kitu. Pamba tuliyouza nje kwa milioni nne hurudi kama nguo za pamba yetu na sisi hutughalimu millioni kumi...
India, China, Russia na nchi nyingine zote zimeweza kupiga hatua kwa sababu sheria imewafunga viongozi na hata wawekeshaji.

Mzee Es nakusikia baba..... Invincible, Choveki eeeh bwana karibuni tena. Points nzito hazibebeki!
 
Sasa milango ndio imefunguliwa na wageni na mashirika yao makubwa ndio wanaingiza wafanyakazi wengi kutoka India na SA kwa kusema ati hatuna wataalam wa kutosha. Hivi kweli kwa kipindi chote hiki cha miaka 46 ya uhuru ni kweli hatuna wasomi? Huko uhamiaji wanawadekeza sana hawa wageni kwa sababu gani? Pamoja na JK kusema kwamba kazi ambazo zinaweza kufanywa na WTZ wageni wasiajiriwe inaonekana kama Idara ya uhamiaji na wizara ya kazi na ustawi wa jamii hawana mpango kama huo. Je kwa mwendo huu tutafika?
 
Maendeleo ya kweli yataletwa na Mtanzania. Kitu kikubwa ni kufuata the Basic law za kila field, ukiwa mwl, kuwa mwalimu kweli, ukiwa Daktari hivyo hivyo, mfamasia, muhasibu, mkaguzi, mkulima, mjasiriamali, kiongozi , ukienda kinyume, mguu upinde kosema sukuta ( Sheria ichukue mkondo wake iwe sheria za nchi au za Profession yako)
Eg Vilabu vya mpira vinatakiwa kuwa na Mikutano ya Mwaka na Chaguzi kila baada ya Miaka Mitatu, lakini hilo halifanyiki unategemea kutakuwa na maendeleo ya mpira ?
 
Wachangiaji, nami naomba kuchangia machache:

Mimi naona kupata mgawo mkubwa wa fedha toka hayo madini si tatizo kwa sasa, tatizo la sasa ni namna tunavyotumia hicho kidogo tupatacho ili kiweze kuzalisha zaidi ama kilete faida zaidi.

Kwa ninavyoielewa serikali ya CCM NA WABUNGE WAKE hata tungepewa asilimia 80 ya mapato bado isingesaidia. Maana CCM ni serikali ya anasa na wezi wabinafsi. Kibaya zaidi ni kua CCM pia imefanikiwa sana kuwafanya wengi wa waTZ si wafanisi ama wawajibikaji wa fani na kazi zao serikalini. Kwa mfano, tungepewa 80&#37; ya mapato ya madini, serikali ingefikia kuamua kwa kutumia wabunge wake kua kila mfanyakazi wa serikali atibiwe nje, ama mbunge atumie lita million za mafuta. Hiyo ndio TZ ya CCM ninayoielewa.

Hizo millions chache tulizopata tungejua namna ya kuzitumia vizuri mpaka sasa tungeweza hata kujenga migodi mingine miwili yetu wenyewe. Vilevile tungewadai investors na kupewa hizo 80% kwa sababu tungekua na akili na sababu ya kufanikisha hilo.

Chukua mfano toka China, kwenye foreign company factory, mfanyakazi mchina anapewa pay USDOLLARS 60 (AVERAGE) na labda factory inatengeneza DVD players na ku export @ kwa USD 20 (China price) baada ya kufunga kiwanda huko kwao (eg. USA)ambako mfanyakazi alikua na PAY 1600 (AVERAGE) pamoja na benefits zingine. Baada ya kuziexport USA zinauzwa kwa faida mara tano ya bei ya China lakini China kama nchi inaambulia USDOLLAR 1 in taxes @ KWA KILA MOJA na makato kidogo toka kwenye mishahara. Lakini China hizo pesa chache wana zi re-invest locally kiasi cha kwamba zinazaa viwanda vingine vya kwao wenyewe na haijalishi kama ni vya serikali. Na kwa kuwa serikali inafanya kweli basi na maendeleo yanaonekana.

TZ ya CCM haiwezi jua namna ya kutumia pesa labda IJE TZ YA CHAMA KINGINE, maana hao CCM walishaharibika hata wao wenyewe hawaelewi cha kufanya. Nilidhani JK anajua, nae kasema wazi hajui. Hata hajui tunaenda wapi maake njia kisha ipoteza, kisha tuingiza maporini tunahaha pakutokea. Sasa tunataka pesa nyingi za nini.

Kwanza ije serikali ya kweli haraka iwezekanavyo kabla madini yote hayajaibiwa, na ndio irekebishe mambo na pesa ije. Kibaya CCM wameshaonyesha hawawezi kuongoza kuzalisha ama kutumia pesa. Ni mabilioni kibao ya msaada yamepotezwa bure na serikali ya CCM. Wakipewa za madini wataziweza, hawataziweza, watazifuja tu.

Ubepari ni safi tu, ila CCM hawajui wafanyacho.
 
Clauses kwenye mikataba zilitakiwa kuwekwa! Wana JF mmeshagundua lakini kuwa kila tatizo manalojaribu kulijadili sasa hivi linakuwa na ngeli ya "INGE" halafu "AWAMU TA TATU"? Matatizo yote tuliyonayo leo "HAVE THEIR ROOTS DEEP INTO AWAMU YA TATU" Sasa sijui hapa tufanyeje? Maskin mimi huwa wakati mwingine nalia kwa uchungu, nipeleke hata mbinguni bado nitakwenda kulia huko na Mungu anaweza hata akanifukuza akidhani mi LUCIFER wa pili!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom