JK atua Dar apokewa na Maandamano ya wana CCM

Sidhani kama alipokelewa na wanaccm bali watanzania ambao wamefurahishwa na heshima tuliopewa ya rais wetu kuwa mwenyekiti wa AU.JK nikama nabii ambaye wachache wenye akili ya mgando wanawaza kwa nini amepewa uchair lakini wenzetu wanatambua ubora wake.

Mtoto Fisadi

Nadhani ukitaka kuweka msisitizo labda utuambie alipokelewa na watanzania waliokuwa wamevaa mavazi ya chama tawala ambao si wanaccm.....
 
OAU, AU old wine in new bottle. Wanaojua wanaweza kukucheka wewe.

unataka kunambia gongo na chibuku ni moja ?

wacha masihara yako haya

kikwete ni kiongozi wa AU ambayo ina hazi zaidi kuliko OAU

kikwwete anaongoza umoja wenya akili na unaosimamia maendeleo ya waafrika sio OAU ambao ulikuwa ukiangalia ujirani mwema
 
Unaweza kunitajia hizo akili na maendeleo tangia wamekuwa AU ? Akili zipi za kuacha Sudan watu wafe ? Akili za kushindwa kusimama kati katika Mgogoro wa Kenya wanakuja weupe kusema ?Maendeleo yapi ?Maendeleo leo kungalikuwa na coup na ufisadi ? Maendeleo ya kuacha kumweleza Mugabe ukweli Zimbabwe ni ya wote hivyo aheshimu haki za binadamu ? Hebu niweke sawa
 
(Samahani kama hii tayari iko kwenye threads zingine)

salamu za lipumba kwa jk

Taarifa ya Mhe Profesa Lipumba juu ya Uteuzi wa Mhe Jakaya Kikwete kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa AU

Directorate of Information and Policy Dissemination

The Civic United Front (CUF)

Party Headquarters

P.O. Box 3637

Zanzibar

Tanzania

Tel. (+)255 (0)747 414100

(+)255 (0)741 257 665

E-mail:
cufhabari@yahoo.com

Website: www.cuftz.org

Kufuatia kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Lipumba, ametoa taarifa ifuatayo:

"Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Jakaya Kikwete kwa heshima kubwa aliyopewa na viongozi wenzake wa nchi za Afrika waliyomchagua kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa mwaka huu wa 2008.

Chama Cha Wananchi (CUF) kimezipokea habari hizo kwa furaha kubwa na kinaiona heshima hiyo ni ya Tanzania na Watanzania wote kama Taifa bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa. Hapana shaka kwamba kuchaguliwa kwa Rais Kikwete kuuongoza Umoja huo kutasaidia kuzidi kuipandisha chati Tanzania na kuitangaza kimataifa.

Pamoja na kuwa ni heshima kubwa kwa Rais wetu na kwa nchi yetu, hatua hii inatupa changamoto zaidi kuzidi kuling'arisha jina la Tanzania katika bara la Afrika na ulimwengu wa kimataifa kupitia nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Natoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa mfano katika ujenzi wa demokrasia ya kweli kwa kujenga taasisi imara zitakazohakikisha sauti ya wananchi inasikika, maamuzi yao yanaheshimiwa na uwajibikaji unaimarika.

Katika uchumi, Tanzania iwe mfano katika kuhakikisha tunatumia rasilimali zetu nyingi na za kutosha kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake kwa kujenga uchumi imara wa soko huria linalotoa ajira, tija na neema kwa wananchi wote. Na katika masuala ya kijamii, Tanzania iwe mfano katika kufikia malengo ya milenia.

Hii pia ni nafasi adhimu ya kukamilisha mazungumzo ya CCM na CUF ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili kumpa nafasi Rais Kikwete ya kushughulikia vyema migogoro mingine ya kisiasa barani Afrika, ambalo litakuwa sehemu muhimu ya majukumu yake akiwa Mwenyekiti wa AU.

Namhakikishia Rais kuwa mimi binafsi na Chama cha CUF tutampa kila ushirikiano na msaada anaouhitaji katika kutimiza matumaini ya Waafrika wenzetu waliotuamini kuuongoza Umoja wa Afrika. Kwa mara nyengine tena, tunasema hongera Rais Kikwete.

DAR ES SALAAM
1 Februari, 2008
 
Well sii lazima kila kitu anachofanya JK basi jamani tulaumu- sasa ni uwongo kuwa amechaguliwa kuongoza AU? Kwa hiyo asipokelewe kwa masham sham?

Mimi nampongeza kupata hii nafasi -walikuwepo wengi- ikaonekana Tz!

Hongera JK- hongereni Watanzania!
 
Lunyungu im sorry kwa ile statement..ilikaa sipo...pale nilikusudia kumwambia Ushirombo kuwa hata wewe unaekaa Kijichi umefika Airport ktk harakati zako za kusaka Taarifa.

Ushirombo kimsingi ile kauli yako ya kuwa CCM waliwachukua wa vingunguti, na kipawa, then unakuja tia rangi eti waliwachukua watu wa karibu....then unasema walipewa 2000 or whatever inaonesha bado hujarekebisha kauli yako. Kimsingi weka Hoja Juu ya Ujio wa JK na Kupokewa kwa Shangwe. na si kutaja maeneo watu wanayotoka. Statement yako mtu anaweza kuifasiri waliwachukua watu wa karibu na kuwapa pesa tzs 2000 watu wa Vingunguti na Kipawa...so hao ndio easily kurubuniwa...

Nakuomba radhi kwa kukuambia unakaa masaki na Kula Kulala...
 
Wananchi wa Tanzania, walimpokea Lipumba na ni wananchi hao hao walimpokea Muungwana, sio kila ishu ni ya kuwa politicalization,

Kikwete kuwa mwenyekiti wa AU, ni heshima kubwa kwa Tanzania kama taifa, kama vile Lipumba kuwa UN, ni heshima kwa taifa letu pia,

Kama sisi JF hatuelewi hizi simple political facts, basi huko mtaaani hatuwezi kumsaidia mwananchi yoyote kama ambavyo lilivyo lengo letu hapa JF.
 
Mzalendo ni kweli..muhim kupongezwa then ashauriwe nini afanye...ikiwa watu wa Big Brother, Ma-mamiss JF members mliwapa Hongera...hao walikwenda kufanya nini Huko?

Kwa status ya JK, kupewa hio Post ni Haki yake, whether ata perfom au la? Je hao viongozi waliopita huko AU wali perfom au ku-deliver anything?tupe mifano..Rais wa Ghana kachemsha Kenya.

Siasa za Migogoro ya Nchi za Africa zinachochewa na Mataifa makubwa US,France IMF, WB etc. wao wanafanya hivyo on purpose ya kuuza silaha. Then waje ktk sura ya Human right watch, UN's agencies waonekane wema. as JK sijui kitu gani anafikiri juu ya AKILi yake juu ya migogoro.

Ushauri wangu amalize issue za TZ, then Aje Kenya then aaangalie huko kwingine. Ahakikishe kuwa Migogoro inakwisha au kupungua kasi yake.
 
Wananchi wa Tanzania, walimpokea Lipumba na ni wananchi hao hao walimpokea Muungwana, sio kila ishu ni ya kuwa politicalization,

Kikwete kuwa mwenyekiti wa AU, ni heshima kubwa kwa Tanzania kama taifa, kama vile Lipumba kuwa UN, ni heshima kwa taifa letu pia,

Kama sisi JF hatuelewi hizi simple political facts, basi huko mtaaani hatuwezi kumsaidia mwananchi yoyote kama ambavyo lilivyo lengo letu hapa JF.

Hizi ni simple ABC za politics wanasiasa wanatafuta platform wakilipata wanalitumia vilivyo ndio mtaji wao huo.

Mwalimu aliwahi kusema wakati wa kufungua kampeni za Mkapa pale Jangwani kuhusu Mrema anavyobebwa na wananchi alisema hivi

"Ushauri wangu kwa serikali ni kuwa, kama kuna mtu anapenda saaana kubebwa, na watu wa kum-beba wapo, tena wakipokezana hivi kama jenezi mwacheni"

Sasa kama waandamanaji wapo tena kwa hiari yao wanaandamana waacheni ndio siasa hizo. Hawana kazi sawa hizo Tshirt na 2000 walizopata ni bora kuliko kukaa majumbani tu...
 
makao makuu ya CUF yako kilima tindi Mtendeni Zanzibar

au unamaanisha nn?

ni chama pekee cha upinzani kinachojulikana kina makao makuu zanzibar na hili pia ndio inaloifanya CUF ivipite vyama vyengine
 
Thanks Lunyungu... unajua nini walio wengi huenda walichukuliwa kule vingunguti na Kipawa kisha kupewa Shs 2000 na nguo za kijani ilikuonyesha mapokezi ya kishindo......ukiwaambia hao hata Idd Amin aliishawahi kuwa mwenyekiti wa OAU hawawezi kuelewa ...kazi kweli kweli

WaTanzania haya matusi haya sio mazuri kwenye jamii yetu... unless you are sure off... please don't utter these kind of words...

Kwetu Mwanakwerekwe watu wana hali kama ya pale Kipawa... kwa hiyo naona unatutukana...

Yakhee... tutatoana mijino humu...
 
makao makuu ya CUF yako kilima tindi Mtendeni Zanzibar

au unamaanisha nn?

ni chama pekee cha upinzani kinachojulikana kina makao makuu zanzibar na hili pia ndio inaloifanya CUF ivipite vyama vyengine

MTU wa Pwani,

Hizi ofisi za Buguruni ni CUF ofisi ndogo bara? au CUF mkoa wa Dar?

Chama chochote chaweza kuwa na makao makuu popote- hata Ngara au Chanjaani- Pemba!

Mbona Makao Makuu CCM yako Dodoma?
 
(Samahani kama hii tayari iko kwenye threads zingine)

salamu za lipumba kwa jk

Taarifa ya Mhe Profesa Lipumba juu ya Uteuzi wa Mhe Jakaya Kikwete kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa AU

Directorate of Information and Policy Dissemination

The Civic United Front (CUF)

Party Headquarters

P.O. Box 3637

Zanzibar

Tanzania

Tel. (+)255 (0)747 414100

(+)255 (0)741 257 665

E-mail:
cufhabari@yahoo.com

Website: www.cuftz.org

Kufuatia kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Lipumba, ametoa taarifa ifuatayo:

“Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Jakaya Kikwete kwa heshima kubwa aliyopewa na viongozi wenzake wa nchi za Afrika waliyomchagua kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa mwaka huu wa 2008.

Chama Cha Wananchi (CUF) kimezipokea habari hizo kwa furaha kubwa na kinaiona heshima hiyo ni ya Tanzania na Watanzania wote kama Taifa bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa. Hapana shaka kwamba kuchaguliwa kwa Rais Kikwete kuuongoza Umoja huo kutasaidia kuzidi kuipandisha chati Tanzania na kuitangaza kimataifa.

Pamoja na kuwa ni heshima kubwa kwa Rais wetu na kwa nchi yetu, hatua hii inatupa changamoto zaidi kuzidi kuling’arisha jina la Tanzania katika bara la Afrika na ulimwengu wa kimataifa kupitia nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Natoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa mfano katika ujenzi wa demokrasia ya kweli kwa kujenga taasisi imara zitakazohakikisha sauti ya wananchi inasikika, maamuzi yao yanaheshimiwa na uwajibikaji unaimarika.

Katika uchumi, Tanzania iwe mfano katika kuhakikisha tunatumia rasilimali zetu nyingi na za kutosha kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake kwa kujenga uchumi imara wa soko huria linalotoa ajira, tija na neema kwa wananchi wote. Na katika masuala ya kijamii, Tanzania iwe mfano katika kufikia malengo ya milenia.

Hii pia ni nafasi adhimu ya kukamilisha mazungumzo ya CCM na CUF ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar ili kumpa nafasi Rais Kikwete ya kushughulikia vyema migogoro mingine ya kisiasa barani Afrika, ambalo litakuwa sehemu muhimu ya majukumu yake akiwa Mwenyekiti wa AU.

Namhakikishia Rais kuwa mimi binafsi na Chama cha CUF tutampa kila ushirikiano na msaada anaouhitaji katika kutimiza matumaini ya Waafrika wenzetu waliotuamini kuuongoza Umoja wa Afrika. Kwa mara nyengine tena, tunasema hongera Rais Kikwete.

DAR ES SALAAM
1 Februari, 2008

Lipumba hapa ametumia hekima!!! kufanya haya... ninalotofautiana na Lipumba ni uwezo wake mdogo wa ku-delegate na kufanya kazi ki-team...

Lipumba alivyokuwa hayupo... CUF ilionekana kama imeenda likizo... tunashukuru sasa karibu CUF iko hewani.. watu wazima munaelewa namaanisha nini...

Anyway jiulizeni... hivi... Lipumba na Seif wasipokuwa CUF... CUF ikuwa vipi... usiku mwema.
 
CUF nadhani inakuwa kama Bunge la Jamhuri kwamba Sitta akiwa kaenda kula nalo linakuwa nje ya kazi .
 
sasa chizi kapewa rungu,ataanza kutembea dunia nzima kujitambulisha kuwa yeye sasa ni raisi wa AO,hatakapokuja kuamka muda umekwisha.Sasa jk jaribu kufukia soo ya mama yetu mongela maana jamaa wamemshika pabaya.
 
Mwambieni basi mheshimiwa akazane kujifunza kiingereza hasa grammar na pronounciation. Nimemsikiliza leo CNN ana problem sana na haya maeneo. Itabidi amuombe Mkapa ampige msasa kidogo.
 
JK kuongea Kiingereza kwa public address sii mzuri- hutabasam tabasam tu- saa ingine haonyeshi seriousness!

Naona pia ana tatizo la little/limited concentration!
 
Yaani kuchapia kote kule na maneno ya Kiingereza kumbe lugha ya watu inampa shida hata kumwaga aibu leo kwenye CNN.Alikuwa kwenye kipindi gani kama naweza ku catch up na mimi jamani hebu semeni kama ni news nitege masikio na macho
 
Back
Top Bottom