JK Atoa mwaliko kwa wadau wa maoni ya katiba

tembeleh2

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
765
165
Source:blogu ya michuzi.

Taarifa ya ikulu kwa vyombo vya habari inasema kwamba, Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania jana (29/2/2012) ametoa mwaliko kwa wadau mbali mbali kuwasilisha majina ya watu ambao wadau hao wanawapendekeza kuwamo katika tume ya kuratibu na kukusanya maoni kuhusu katiba mpya.

Wadau waliopatiwa mwaliko huo kupitia gazeti la serikali no.66 la ijumaa iliyopita (24/2/2012) ni pamoja na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, jumuia za kidini, asasi za kiraia na pamoja na jumuiya,taasisi pamoja na makundi mengine yenye malengo yanayofanana.Mwaliko huo vile vile utatangazwa kwenye magazeti ya kawaida. Mwisho wa kupokea majina hayo ni machi 16,2012.
 
Kama JF tutajikusanya vizuri na sisi tunaweza kupata majina yetu matatu tukayawasilisha huko kwa Rais. Tuchangamkie fursa hii badala kubaki kulumbana wenyewe kwa wenyewe tu kila siku. Naanza kupendekeza:
-Mzee Mwanakijiji. Ufahamu na uelewa wake mpana wa mambo ya nchi utatusaidia kupata KATIBA nzuri.
-Mag3. Ujengaji wake wa hoja zenye mantiki na mashiko ni hitaji kubwa la KATIBA mpya.
-Nguruvi. Huyu anasimamia zaidi mambo yenye maslahi kwa Taifa. KATIBA mpya itayasimamia haya.
Tutoe mapendekezo yetu ya majina tunayoona yanafaa.
 
Naunga mkono pia mwanakijiji kama yupo ndani ya nchi au ataaamua kuja kushiriki katika suala hili.
 
Wazazi mnapoteza muda bure JK ni sanaa tupu na anawajua wa awabongo mataanza kugombania hizo nafasi kwa kutaka mpunga mpaka mtavunja vyama na mwisho wa siku utaona vichekesho kwa hao watako teuliwa jiulizeni JK amewahi kufanikisha jambo gani? taifa stars ilimshinda ndio katiba! wazazi yangu macho.
 
Back
Top Bottom