JK atishia kuwahamisha watu kwa nguvuTarime. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK atishia kuwahamisha watu kwa nguvuTarime.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Oct 14, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,206
  Likes Received: 3,621
  Trophy Points: 280
  Source:Gazeti la habari leo.

  "RAIS Jakaya Kikwete, amewataka wakazi wa Tarime mkoani Mara waache kupigana, kama wataendelea hatasita kuwahamishia mikoa mingine.

  Ametoa msimamo huo jana wakati anazungumza na wakazi wa Tarime katika maeneo ya Nyamongo na Ntagacha.

  Rais Kikwete amesema, taarifa zilizoenea kuwa Tarime kuna mapigano yasiyokwisha hazifurahishi . “Punguze ugomvi , hivi ndugu zangu mkikosana jawabu lenu ni kupigana.”

  “Mwalimu Nyerere aliwahi kuwahamisha katika mikoa tofauti wapo waliokwenda Tunduru na kwingineko, kama hapana budi kuwahamisha mikoa tutafanya hivyo ingawa hatupendi kuwaondoa katika maisha yenu mliyozoea.”amesema Rais.

  Amewashukuru kwa kuwa hawajapigana kwa miezi miwili, na amewataka wanapokuwa na matatizo waende kwa viongozi wao na si kupigana"

  Kwa maoni yangu.Tatizo kubwa la huo ugomvi ni uhaba wa ardhi na wala sio eti ugomvi wa makabila kama serikali ya CCM inavyotaka tuamini!Kiuchumi,idadi ya watu ikiongezeka hufanya ardhi iwe most valuable natural resource,

  lkn sidhani kama suluhisho la ugomvi w ardhi wa wana Tarime ni kutishia kuwahamisha kutoka kwenye makazi yao ya kudumu na kuwapeleka makazi mapya kama JK alivyosema jana!

  Uzoefu unaonyesha kuwa hivi sasa sehemu nyingi za TZ kuna mzozo wa kugombea ardhi kati ya wafugaji na wakulima toka kule Kilosa,Loliondo na sehemu zingine nyingi,je ina maana nao hao wote watahamishiwa sehemu zingine wakianza kupigana?Kumbuka Kilosa walipigana hadi makumi ya watu walikufa!JK tafuta ufumbuzi wa kudumu sio huu wa zima moto
   
 2. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,206
  Likes Received: 3,621
  Trophy Points: 280
  Kazi tunayo haki ya nani naapia!
   
Loading...