JK atangaza kuanza utekelezaji ahadi ya vyandarua Lindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK atangaza kuanza utekelezaji ahadi ya vyandarua Lindi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Kikwete jana aliendelea kumwaga ahadi kwenye kampeni zake mkoani Lindi, huku akibainisha kuwa tayari ameanza kutekeleza ahadi ya kugawa vyandarua viwili kila kaya aliyoitoa hivi karibuni.

  Akizungumza kwenye uwanja wa Nyangao Jimbo la Mtama, Kikwete alisema ahadi ya kugawa vyandarua hivyo, imeanza kutekelezwa mkoani Lindi.

  “Hivi karibuni niliahidi kugawa vyandarua viwili kila kaya, ahadi hiyo tumeanza kuitekeleza kwa wakazi wa Mkoa wa Lindi ambako tumepeleka vyandarua 145,968,”alisema na kuendelea:

  “ Watu wanasema sana kwamba rais anatembea sana na mimi nasema, kama ningekaa Dar es Salaam na kuangalia uzuri wa mke wangu, Watanzania wangekufa.”

  “Nisingetembea ningefahamiana wapi na Bushi hata anipe vyandarua bilioni 5.2 ? alihoji.

  Kikwete alitaja faida zingine za ziara zake nje ya nchi kuwa ni pamoja na kufahamiana na serikali ya Marekani ambayo imeahidi kuipa Tanzania msaada wa vitabu vya sayansi.

  “Vitabu 800,000 ya masomo ya sayansi wameshatupatia na mwakani wataendelea kutupa vitabu vingine milioni 2.4,” alisema.

  Alieleza kuwa mbali na msaada wa vitabu, serikali yake ijayo ina mpango maalumu wa miaka mitano kujenga nyumba za walimu ili kuwawekea mazingira mazuri ya kazi.

  “Tunapanga pia kuajiri walimu 19,000 ambao tutawagawanya watano kila shule za sekondari za kata,” alisema Kikwete na kuongeza kwamba serikali yake pia ina mpango wa kuboresha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kujenga hospitali nyingine ili kusaidiana kukabiliana na changamoto za kuuwahudumia Watanzania.

  “Pia tuna mpango wa kuhamisha Chuo Kikuu cha Muhimbili kutoka mahala kilipo n kukipeleka Mlonganzila ambako pia tutajenga hospitali nyingine kubwa itakayoshirikiana na Muhimbili. Lengo letu ni kupunguza tatizo la kupeleka wagongwa nje ya nchi na kuwaleta wagonjwa kutoka nje kuja kutibiwa hapa,” alisema Kikwete.

  Akizungumzia suala la afya kwa wakazi wa Jimbo la Mtama, Kikwete alisema ana mpango wa kuipandisha hadhi Hospitali ya Nyangao ili iwe na hadhi ya Hospitali Teule na Hospitali ya Mandawa iliyoko Lindi vijijini kuwa hospitali ya wilaya.

  Awali Kikwete aliwataka wananchi kuichagua CCM akieleza mambo matatu aliyosema ndio kigezo cha chama hicho kuendelea kutawala.

  “Nawaombeni Watanzani tuichague CCM kwa sababu tatu muhimu:Moja hakuna chama bora kuliko CCM kwa muundo, sera na mipango. Vipo vyama 18 lakini wengine ni ‘photocopy’, vinajaribu kutuiga na hii ni haki yao kwani ukichelewa kuzaliwa unapaswa kuwaiga waliokutangulia,” alisema na kuendelea:

  “Sababu ya pili ya kuwatakeni muichagua CCM ni kwamba imeongoza nchi hii vizuri. Nchi imetulia ndiyo ni maskini lakini mambo yamebadilika sana ikilinganishwa na wakati wa uhuru.”

  “Pia sisi ni waaminifu.Tukiahidi tunatekeleza. Mwaka 2005 tuliahidi amani na utulivu natumefanya.”

  chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hili zee kweli jinga ..mke mzuri yuko wapi?na tungekufa kwa nini?kwa ukimwi au?mbona alishasema kupata ukimwi ni kiherehere?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kigogo Usimwite mkuu wa nchi yako (jinga) unakosea hivyo amesema ukweli kuwa kupata ukimwi ni kiherehere chako mwenyewe kwa nini mtu mmoja unakuwa na wapenzi

  wengi? Kupata ukimwi ukiangalia kwa undani ni kujitakia mwenyewe itabidi tuache kufanya mambo ya ukahaba kila mtu awe na Mke wake mmoja Au mpenzi mmoja kama hakutoshi Mtu kuwa na Mke mmoja? Kama ni hivyo bora uowe Mke mwengine sio kuweka kimada Mkuu wa nchi hapo mimi ninamuunga mkono kwa maneno yake aliyoyasema.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ujinga sio tusi MRI mjinga anahitaji kuelimishwa ili aelewe...mpumbavu haelimikishiki hat a iweje!kwa level yake Kama mkuu wa nchi aongee mambo ya maaana Kama Hana akae any we kahawa ila sio kuongea matapishi...eti nikae kumuangalia mke wangu uzuri wake?..sio ujinga huu
   
 5. m

  mubi JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  when will tanzanians make their own mosquito nets? For how long the usa will be suppling free nets to tz?...how much did the president spent for trips abroad compared to the mosquito given, think abt if the total money spent for travelling abroad were spent to assemble small industries for mosquito in nyanza area where there are abundant production of cotton......tell me what how many dealth would have happened there.
   
 6. m

  mubi JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  alizungumzia hayo akiwa tabora pia. Tunafundishwa kutegemea kuletewa tu. Ndugu wapenzi mosquito net haihitaji teknolojia ya ajabu kutengeneza. Jua kali inaweza tengeneza net hizo. Nipe mimi pesa anayopanga kusa**** nje, ninunue mashine za kutengeza net na nifundishe vijiji viwil viwe vinaproduce, tutauza africa nzima na amerika ya kusini yote na pato la wanakijiji litaongezeka maradufu ya pesa anazotumia raisi kwenda kuomba vyandarua usa,
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Dr. Slaa alisema JK anatumia mipango iliyo tayari kutoa ahadi na ni kinyume na sheria ya gharama ya uchaguzi. JK amekuwa akitoa ahadi kuwa akichaguliwa tena atatufanyia wananchi, sasa iweje hata kabla ya kuchaguliwa anatimiza ahadi? Sio kwamba anamalizia kutimiza ahadi za 2005 - 2010? Kwa maneno mengine hiyo ni rushwa kwa wapiga kura. Poor JK!!!!!!

  Kumbe ahadi hizi ni moja ya maombi yaliyoko kwenye hayo makaratasi aliyoshika kwenye picha hii.
  [​IMG]
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Technically hiyo ahadi sio yake kwa sababu pesa inatolewa na mtu mwengine..credit iweje ajinadi nayo yeye?

  Pathetic..
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  So desperate. Begging.

  JK pumzika tu ndugu yangu. Kazi ya urais huiwezi.
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Safi sana jk na dawa ya umbu pia umalizie malaria ni tatizo mojawapo kubwa tanzania
   
 11. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nyumba za Lindi na Vyandarua? Hivi hawa wanajua nyumba zilizoko lindi? au nini hiki?
   
 12. l

  lembeni Member

  #12
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  faida ya kutembea kwako ni ndogo kuliko hasara
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Tunagawa vyandarua lakini hatuweki nguvu zozote za kuondoa tatizo la mazalia ya mbu! Kazi tu kuomba misaada hata sehemu ya kutumia akili kidogo.
   
Loading...