JK atakiwa kuomba radhi

wewe unataka kunizungumza mimi. Miye najonga hoja na kutoa maoni, ni haki yangu kutoa maoni hiyo na hakuna mtu anayeweza kuniambia niyatoe namna gani. Unayo haki ya kutoa maoni yako kuhusu nchi yako jinsi wewe unataka kutoa na hakuna mtu mwenye haki ya kuuliza kama unatoa maoni vizuri au vibaya au kusema jinsi gani maoni yako yatolewe.

Kama maoni yangu hayapendezi mbele zako mheshimiwa au hayatoshi kwenye sanduku lako la maoni unayo haki ya kuyachambua na kuyaonesha hayafai ili maoni yenye nguvu yashinde.

and to answer your question, yes I'm serious. Hakuna hoja isiyotaka kufikiwa kikomo. Sisi kama Taifa tutaendelea kulizungumza suala hili kwa muda gani? Mawazo kama ya kwako ndiyo yamesabibisha na viongozi wanaozoea na kuvumilia uzembe kwa sabab hawataki kuhitikisha mijadala ya maana na badala yake wanaivuta miaka nenda miaka rudi.

Suala la mikataba mibovu lingemalizwa zamani lakini hadi leo they are still dragging it out, bodi ya mikopo is the same thing, michezo is the same thing. Ni lazima tujifunze kuhitimisha mijadala na huu wa Kadhi ni mmoja wao. Wao waislamu wafikie mahali wapate majibu ya uhakika, Serikali ifikie mahali itoe maelezo ya uhakika n.k

Sijui kwa nini wewe unataka huu mjadala uendelee bila kukoma, kwa faida ya nani na kwa hasara ya nani?
 
Yeyote anaye support mahakama ya kadhi ni MHAINI, anapaswa aadhibiwe kama watu wa aina hiyo.

Mahakama ya Kadhi itatumia SHARIA, na hapo ndo kiama kitaandama
 
CCM na JK they made a terrible mistake . Walisema na wanasema wana hoja na sera imara lakini waliishia ku copy kwa uroho wa kupata kura na madaraka . Maneno haya yalianzwa na Mrema na baadaye baada ya kuona CUF they are powerful pamoja na kuwaita wadini wakaamua ku copy kwao na sasa inawatokea puani. JK ni msanii lakini sasa kanasa . Hatuwezi kuruhusu vita kisa kuwapa watu furaha . Not under my name with my tax hapana .Waislam lazima mjiulize kweli mnaweza kupokea funds ambazo zina source toka kwa makafiri ? Maana kuna hata makahaba wanalipa kodi na kuwa na Kadhi kupitia Bungeni means mpate pesa zetu . Hebu nendeni mkajibu hoja za Mtikila kwanza then mje hapa tuongee .
 
Naamini Mh. JK atatumia busara zake katika kuilinda katiba ya Jamhuri Ya Muungano wa Wadanganyika kama alivyoahidi siku ile alipokula kiapo alipolamba dume. Hali kadhalika kwa Afande Mwema, katiba ya Tanzania ni ile ile. Hairuhusu nchi kuendeshwa kwa misingi ya dini. Sasa nyie mliopewa dhamana na mkala kiapo cha kuilinda inabidi muilinde kweli. Na kama hii habari ya kupelekwa jambo hili bungeni kwa mlango wa nyuma ni ya kweli, basi hapo kutakuwa na danger ya hatari.
 
Mimi nafikiri tungefuata formula iliyopendezwa na Mtikila hili jambo ni rahisi kabisa: Waislamu wana haki ya kuanzisha mahakama ya kadhi na hata mahakama zingine, lakini kamwe hawana haki ya kutaka hili jambo liwe sehemu ya Katiba yetu. Kwa hiyo hakuna hoja ya serikali kuhangaika na hili jambo. Ni kutoa tamka tu, waislamu endeleeni na shughuli zenu ikiwemo kuanzisha mahakama ya kadhi na zingine, lakini sio kutaka serikali iwasaidie, au kutunga mswada, hiyo ni No. Basi mjadala unakuwa umeisha.

Ahadi nyingi alizotoa JK alitoa kwa ajili ya kujipendekeza kwa wapiga kura bila hata kujua kama zinaweza kutekelezeka au la. Sasa awe jasiri kama alivyofanya Mkapa 1996, apime ukweli wa ahadi alizotoa, kisha asimame kwa zile ambazo anaona haiwezekani, awatangazie watanzania kwamba hili halitekezeki, basi. Mwenzake Mkapa alifanya hivi 1996 na aliendelea kuwa Rais wa nchi tena kipindi cha pili akapata kura nyingi zaidi kuliko alizopata 1995. Watanzania hawana maneno, huwa wanakubali tu chochote wanachoambiwa na viongozi wao, sijui JK anaogpa nini kuwaambia ukweli kuhusu hili!
 
Mwanabodi,
Nimejaribu kwa muda mrefu kuvumilia haya nayoyasoma hapa lakini imefikia wakati inabidi nizitoe hizi pamba masikioni kuyapokea yote kisha kusema yangu machache kwa haki hiyo hiyo mnayoitangaza wengine.
Ni lazima katiba iwe na vifungu vinavyoruhusu baadhi ya sheria kutambua uhuru wa watu fulani ili kutimiza haki mnayozungumzia. Mnaposema Fedha na kodi za Watanzania wote mna maana gani?.... maanake hili swala sasa hivi linaanza kujenga hoja za Udini zaidi na watu mnajibu mengi kwa kutazama rangi zenu za dini.
Sasa ikiwa serikali haitambui mafundisho ya Kikristu inawezaje jenga kinga ya dini hii kuweza kuendesha shughuli zake nchini?..Kila sheria nchini inajengwa kwa kutazama vipengele vyote (Objective) ktk kujenga na sio ktk kubomoa (Negative) manner. Katiba inajengwa kulingana na mazingira yetu, watu wake na mambo yote yanayohusu jamii nzima kwa mtazamo wa kujenga na kuimarisha jamii hiyo. Hata mikataba inayotiwa sahihi ina sheria zake ktk Katiba kwa kuwatazama wawekeshaji, miradi na kadhalika kwa manufaa yetu sote hata kama ni kundi dogo la hawa watu wanaopewa sheria hiyo. Kuna sheria za Kikatiba zinazowapa nguvu na haki wanawake, watoto na hata wageni tofauti na kundi la watu wengine kwa sababu hizi Sheria zipo kwa ajili ya kuweka usawa ama kuleta maendeleo kwa jamii nzima.
Wanabodi, rais wetu alitoa ahadi ya kuwepo kwa korti ya Kadhi na zipo sababu ambazo zilifanya yeye kuafiki ama kutoa ahadi swala ambalo sisi kama raia wake inabidi tujenge hoja zinazolinda maslahi ya Taifa na sio kubomoa. Tatizo kubwa linalojitokeza hapa yaonyesha wazi sio korti hizi ila ni hofu yenu kwa Uislaam. Hofu ambayo Mtikila kama kiongozi wenu wa dini kainjenga ktk mioyo yenu na sasa mnaanza kuamini kabisa kuwa korti za kadhi ni mbinu ya waislaam kuutokomeza Ukristu. Hoja zenu zinajieleza wazi kabisa na hata hizo kodi mnazozungumzia ni sababu finyu zilizotanguliwa na hofu yenu kuhusu Uislaam.
Kitu cha maana hapa ni kutoa mapendekezo yetu ktk swala hili kisha tujenge hoja inayolingana na kuprotect maslahi ya nchi na sio kuzungumzia maswala ya fedha na kodi wakati ni fedha na kodi hizo hizo zinazoendesha serikali yetu ktk kila taasisi. Ni sawa na mtu kusema sheria za Uhalifu kuwepo kwa Polisi ama Jela ni upotozaji wa kodi za wananchi kwani mimi sio mhalifu na wala sintakuwa. Ukitazama kujitenga wewe na hao wahalifu kisha ukajenga hoja. Ikiwa kriti za kadhi ni too much kwenu jengeni hoja inayohusu korti hizi na waislaam sio kutazama nje ya waislaam kama tunavyozitazama korti zetu, Polisi na jela zetu tukitazama na kuzingatia Uhalifu (crime).
As a Muslim sioni sababu ya muhimu kwa Kikwete kwenda Vatican na naweza jenga hoja za kipuuzi lakini kama naelewa nini mahusiano ya jamiii ktk mawasiliano siwezi kuweka visingizio na kudai kwa nini kodi za waislaam zimelipia ziara hiyo ya rais huko Vatican!. Huu ni ufinyu wa kutazama swala zima linalohusiana na ziara za rais na kama nita raise swali kwa njia hiyo nitakuwa nachekesha. Zipo sababu nyingi za kuhoji ziara za rais lakini sio kwa mtazamo wa dini.

Rais Mwinyi alitoa ahadi ya kurudisha shule na mahospital kwa madhehebu ya dini hasa wakatoliki mbona hamkupiga makelele na kuuliza kulikoni kwa mtazamo huu mnaoutumia hapa. Naelewa kwa uhakika kuna walimu waislaam kibao walifukuzwa kazi zao kwa sababu tu ni waislaam lakini sijasikia mkisema yote haya isipokuwa leo Mtikila mshenzi mmoja kajenga mioyo yetu kuamini kuwa Waislaam ni Magaidi basi nanyi mnadakia na kuanza kumwita rais wenu GAIDI just because ni Muislaam aliyetoa ahadi kwa waislaam. Mbona Nyerere alitoa ahadi nyingi tu kwa Vatican na hakuna muislaam aliyejenga hoja za kipuuzi kuulizia kodi za waislaam.. ahadi ambazo alikuja zitimiza lakini bila kuathiri maisha ya waislaam.
Guys sisi tumesoma ktk shule za katoliki na tumelazimika kutumia majina ya kikristu kuweza kupata nafasi ya kusoma. Tazama huko Tanga kuna watu kibao wenye majina mchanganyiko utasikia mtu akiitwa Gregory Hamid, wote hawa wamebadilisha majina yao kwa sababu ya kutafuta elimu chini ya himaya ya kikristu leo sheria zinabadilika kidogo mnaanza kutazama ni kwa faida ya waislaam.
Pleeease kluna tatizo na korti ya kadhi toeni hoja zenu zikizungumzia korti hiyo na sio waislaam kuwa heading ya mada kwani wapo waislaam wasiokubaliana na korti hizo.

KUWAITA WAISLAAM MAGAIDI ni ushenzi, Upumbavu na Ufisadi mkubwa unaotokana na utumwa wa imani ya dini..
 
na nimeona kitu kibaya sana anataka kukidhi mahitaji yake kwa kufikia conclusion ya jambo muhimu na ambalo limepamba moto na linahitaji muda mwingi kulifikiria, lakini kilichonishangaza ni yeye kusema kwamba vyovyote itakavyokuwa lakini linatakiwa lifikie kikomo ! is he serious ??

Mzee hili suala halihitaji ujue sheria saaaana hili kulitupa kapuni.

Ni suala ambalo halihitaji mjadala kabisa.

Ni suala ambalo watu wenye busara kama wewe ungeshauri watawala waachane nalo kabisa.

Hii siyo politics hila ni mchezo utakaotumaliza mkuu.Lakini mara nyingi watu watawala wengi wenye uwezo mdogo wakishindwa kutawala huwa wanatafuta mahala pa kushika.

Suala hili naona ni mbinu ya watawala(wenye kukosa dira) kutaka kupata watu wa kuwaunga mkono.
 
Serikali ya Tanzania haina dini. Pamoja na kuwa nataka sana kuona mabadiliko makubwa ya Katiba yetu ambayo ina mapungufu mengi sana, lakini siungi mkono kuingiza mambo ya Kadhi katika katiba hiyo, kufanya hivyo itakuwa ni makosa makubwa sana.
 
Kuna bwana mmoja hapo juu ametoa maelezo marefu.Huyu bwana anatakiwa apepewe kidogo kwani inaonekana amechemsha.Amekuwa na michango constuctive sometimes, lakini hapo naona amevuruga kabisa.Ila nachoelewa ni kwamba udini ni suala lenye nguvu sana katika jamii kwani moja ya research zilizofanyika hapo nyuma zilionyesha kwamba watu wanasilikiza zaidi na kuwa na imani kubwa kwa viongozi wa dini kuliko wanasiasa.Sijui sisiemu hawakulipima hili kabla ya kuliingiza suala la kadhi kama sera, au waliasema potelea mbali mambo yote ni mbele kwa mbele.Sasa hivi hawana namna inabidi watoke na majibu ya kuwaridhisha waislamu otherwise watakuwa wanahatarisha amani makusudi.
 
Mfuatiliaji,
najua unaye mtaja hapa ni mimi lakini nakuomba kitu kimoja tu - Hoja hujibiwa na Hoja ktk uwanja huu. Jibu hoja zangu kwa hoja na sio kunyoosha vidole vitupu. Maneno ya kusema fulani kachemsha kisha usiseme nilichochemsha na kueleza hoja yako inakuwa Upuuzi mtupu.
Kwanza unaposema wananchi husikiliza viongozi wa dini kuliko wanasiasa ndio hapo hoja nzima inapokuwa na uzito. Hili ni swala la Kisiasa ambapo dini inatazamwa kama jumuiya inahitaji haki fulani na wahusika wa swala hili ni dini inayokusudiwa sio jinsi wewe unavyofikiria ama mchungaji wako.
Korti ya kadhi ina matatizo mengi ktk mtazamo tofauti na kama nilivyosema inapingwa na waislaam pia kwa hiyo sio swala la Udini hata kidogo. Kisha nitakwambia kitu kimoja ambacho wengi wenu hapa mnajaribu kupotosha topic nzima. Maswala yote ya ndoa, mirathi na kadhlika yametungiwa sheria toka mwanzo kwa kutazama imani za DINI. Sio Uingereza, Marekani Arabuni, Kenya, Tanganyika ama Vatican wote wameweza kutazama imani za dini na sio mila zetu, na vifungu maalum vipo ktk KATIBA zote za nchi zinazotoa Uhuru wa imani za dini.Uurusi na China walikuwa hawana vifungu hivi ktk katiba zao na ndio maana tunasema wananchi wake hawana uhuru ktk maswala ya dini..Lakini kuwepo kwa sheria hizi kunahakikisha kwamba hakuwezi kuponza uhuru wa waumini wa dini nyinginezo.
Haihitaji degree kufahamu nini Mtikila amezungumza na kwa malengo gani na kama wewe unamsikiliza yeye kutokana na imani yako fanya hivyo bila kuingilia imani za wengine. Mtikila kamwita rais wetu GAID na hili neno pamoja na kuwa lina tafsiri nyingi limetumika kwa malengo ya kumwita rais wetu as a TERRORIST.. Hiii neno limeundwa na Wamerekani kuwa lebel Waislaam wenye siasa kali na tafsiri yake ktk kiswahili tumekuwa tukitumia GAIDI. Kwa hiyo ktk Kiswahili kwanza hutazamwa neno limetumika wapi ili upate maana halisi ya malengo ya message nzima. Mtikila was wrong pamoja na haki yake ya maoni pia kama kiongozi wa dini na siasa ni mpotoshaji na hatari kwa usalama wa Taifa...

Mnachojaribu kujenga hapa ni upotoshaji kwani huwezi kumwita Mwanamke ***** kutokana na hulka zake kisha ukasema haukuwa na maana ya Umalaya bali huyu mwanamke anasema sana, filimbi nyingi. Ama mtu akuulize why unawaita Wanawake ***** ukasema Noo sikuwa na maana hiyo kwani hata wananume wanaweza kuwa Malaya. These a just excuses na hatuwezi kuzipokea ati kwa sababu alosema ni Mchungaji!
Hell Nooo!
 
Wasee,
Mie nilisha wahi kuuliza siku za nyuma, je ni nani amefanya study au poll ya kujua kwamba ni nini hasa opinions za waislam wa Tanganyika juu ya kadhi courts??........mie nasikia hasira na donge moyoni kwasababu watu wanatumia issue hii, waislam na uislam wao for cheap political gains!!! Wallah, huu ni ufisadi kushinda ufisadi...... hii issue ni ya kuiacha, yeyote atakae taka kuifufua basi mmuogope kwasababu si rafiki yenu.
Mie nimeishi Tanzania mpaka nafika 21yo, kwenye familia ya kiislam hasaaaa Dar na Tanga.....sikuwahi kusikia hata siku moja watu(ndani ya familia) wakizungumzia jinsi uislamu wao ulivyopungufu ati kwasababu hamna kadhi courts!!!........sasa leo ghafla bin vuu, haya yanatoka wapi??. Acheni kuwa na "blackboard mentality" meaning, watu wanawajaza ujinga, wanafuta, wanaweka mwingine nyie mmebung'aa tu kama jiubao kwenye ukuta darasani.
Wake up people.....hii ni "political IED," mnatumika, hawa jamaa ni opportunistics, wanataka ku-divide ili watawale/kushinda chaguzi kwa ku-avoid really issues........maisha na matatizo ya TZ ni bigger than Kadhi courts, get real pple.!!
 
YournameisMINe,
Mjomba kwanza hongera umesema neno la maana sana kwani hakuna mtu alofanya study yoyote ile na kama nilivyokwisha sema kuwa wapo waislaam wanaopinga, mimi mmoja wao. Sasa inapofikia kuweka kifungu fulani ktk Katiba yetu mnaanza tena kujenga hoja za kidini inashangaza sana kwani Katiba yetu ya kwanza ilijengwa kwa kutazama dini hizi hizi. How can you solve this probl;em ikiwa kila kitu mnapinga tuuu maadam hili swala ni la dini nyingine sio yako!
Katiba yetu ilikwisha rekebishwa huko nyuma kwa kuwahusisha waislaam na wanasheria na kwa bahati nzuri umesema mwenyewe kuwa ktk maisha yako hukuona matatizo kabisa. Then sheria tayari kulikuwepo na vifungu vya dini why now imekuwa problem kurekebisha katiba hiyo hiyo...
iProblem tulokuwa nayo leo ni kuanzisha kwa korti hii sio kufungu cha sheria ambacho kinaweza ku deal na ndoa, mirathi ya waislaam. Kama kuna utata pia ni vizuri tuseme utata wenyewe kwa kuwatazama wahusika na sio imani zetu sisi nje wakati hazituhusu kabisa. Nipo against korti za kadhi kwa sababu zinazolingana na mazingira yetu yaani Watanzania wana ruksa ya kuoa mke wamtakaye bila kujali dini yake. Pili, waislaam wengi wameoa wake nje ya ruksa ya mke wa kwanza wakifuata tamaduni zaidi ya dini, Watoto wengi wamezaliwa nje ya ndoa za kiislaam kwa hiyo swala la korti linaweza bomoa familia hizi badala ya Kujenga. Korti za kadhi hazitambui haki za watoto waliozaliwa nje ya ndoa pia wanawake wengi wamekuwa wakifukuzwa toka ktk nyumba ama mirathi ya mume kinyume cha sheria ya dini. Hivyo basi kama kutakuwepo na mabadiliko ktk sheria zetu basi inabidi kwanza waislaam wenyewe wakubali kufuata sheria zote za dini yao jambo ambalo haliwezekani kabisa Tanzania.
Kifupi sisi wote ni waumini wa kuchagua kilicho bora kwetu, tunafuata dini kwa sababu ya Identity tu sijaona jamii fulani kuwa muumini wa kweli zaidi ya mila zetu kwa hiyo sheria pekee inayoweza kwenda na sisi ni ya kimila zaidi tukizingatia ndoa na mirathi zinalinda maslahi ya wanyonge wahusika.
Hivi sasa pamoja na kwamba Katiba yetu ilifanyiwa marekebisho zamani kutazama maslahi ya waislaam kuna vipengele ktk ndoa na mirathi havikutazamwa kiasi kwamba watu wanatumia nafasi hizo kuwanyanyasa wanawake na watoto, Je, tuweke sheria gani ambayo itakuwa Universe ktk imani zote za dini nchini?...sidhani kama ipo na kama ipo twambieni ili hao waislaam wanawake na watoto wanaozaliwa nje ya wapate haki yao na nafasi ktk jamii hii.
 
Mkandara,
Tupo pamoja, kwenye ile thread ya Mtikira na mahakama za kazi nilisema kama ulivyosema hapo juu!! Mie pia ni mslamu(lakini si-practice kihivyoo...najua nitapigwa dogo,lakini poa tu) ambae kutokana na facts kama zilivyo napinga kuwepo kwa mahakama ya kadhi, napinga mjadala huu kuendelea na naona suala hili limejaa siasa(viongozi wa vyama na serikali), a $$$ sign kwa masheikh uchwara wasio na la maana la kufanya na muda wao. Issue hii ni kwasababu za binafsi na sio maslahi ya waislam kwa ujumla!!.
 
Hivi watu wanaopinga Mahakama ya Kadhi kuwa ni kinyume cha Katiba, mbona Mahakama hiyo ipo tayari Zanzibar kwa zaidi ya miaka mia moja sasa, na hakuna mtu aliyepinga kuwa Mahakama hiyo inapingana na Katiba ya Muungano ambayo ndiyo sheria kuu ya Jamhuri yetu? Wengi wanaopinga uwepo wa mahakama hiyo ni kutokana na uelewa wao kuwa Mahakama hiyo itakuwa hivi au vile bila kukaa na kuuliza itakuwaje.

Leo hii kuna mahakama za kadhi Israeli (nchi ya wayahudi) lakini hakuna mahakama ya Kadhi Uturuki (nchi ya Waislamu). Leo hii kuna Mahakama ya Kadhi Uganda (ambapo wengi ni wakristu) na Kenya (ambako wengi ni wakristu) lakini hakuna mahakama ya Kadhi Indonesia ambayo ni nchi yenye Waislamu wengi. Leo hii kuna Mahakama za Kadhi kule India na zinafanya kazi zake lakini Sheria ya India hazitambui rasmi lakini maamuzi yake yanachukuliwa kuwa ni maoni tu yasiyo na nguvu za kisheria na wale wahusika wakiridhika basi maoni hayo yanasimama kama uamuzi.

Jamani hakuna modeli moja ya uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi duniani. Kila jamii ya Waislamu inayo haki ya kukaa chini na kuona katika mazingira yao na historia yao Mahakama ya Kadhi inaweza kufanya kazi vipi. Binafsi ningependa kuona Waislamu wanatengeneza proposal ya jinsi Mahakama hiyo itakavyokuwa na itakavyoendeshwa ili utupe angalau wazo la kuona tunapopinga au tunapounga mkono tunafanya hivyo kwa misingi gani.

Kupinga tu alimradi kupinga kutokana na kutojua ni kupinga kwa waoga! Mbona kama nilivyosema hapo juu Kanisa Katoliki na Kanisa la Anglikana wana Mahakama zao za Kanisa? Mbona hatujasikia watu kusema kuwa sheria ya Mke mmoja na Mume mmoja italazimishwa kwa watu wote? Kama Mahakama za Kanisa zimekuwa zikifanya kazi nchini kwa muda wote huu kwanini tuogope uwepo wa Mahakama za Kadhi ambazo zitawahusu Waislamu?

Tusipinge alimradi tunapinga ili tuonekane tunapinga. Hoja za Mtikila zina msingi mkubwa. Hata hivyo hoja hizo zisichukuliwe kama Neno la Bwana na haziwakilishi mawazo ya wakristu wote nchini.
 
Wanaforum
Watu tunapochangia inabidi tuwe na data nzuri na si zakufikirika.
Hili la Vatican.
Vaticani ni nchi huru na bahati nzuri kwa au mbaya kwa ,kulingana na katiba ya nchi hii Rais wake huwa ni PAPA ,sasa ukiona papa anaudhuru ktk nchi huwa anaenda kama Rais wa nchi ya vatican.Haitwi Rais Papa wa Vaticani kutokana na ugumu wa matamushi kama ilivyokuwa vigumu kutamuka Mwalimu RAis Julius Nyerere wa TZ.
Hii ni sawa kabisa na nchi za Falme za kiarabu utakuta shehe pia ni mfalme ama Rais wa nchi hizi zipo nyingi sana nchi za namna hii na ubalozi wa TZ upo pia huko sasa ikitokea muislam akasema haoni sababu ya kikwete kwenda Vaticani ama hakuna sababu yakuwa na ubalozi huko huyu mie nafikiri hana data kamili au uelewa finyu ama ana jadili akiwa amejikita ktk udini na kuzifungia mipaka fikra zake .
KADHI ni jambo Muafaka kwa waislamu lakini kwa nini wanalifanya kuwa GUMU??? kwanini lihitaji kutungiwa sheria wakati DINI ni imani yani YES au NO.
KADHI waislamu ianzisheni lakini kwanini mnahitaji itungiwe sheria na iwe ndani ya katiba???
Lazima watu tukubali mtindo wa kukubali ukweli watu tunapinga hii mahakama kupewa sheria kikatiba maana kwa kufanya hivo kila kitu kitakacho aanishwa ktk mahakama hiyo itabidi kila mtanzania akikubali mfano mie leo ni muislam kesho nahasi lakini wenda ktk sheria za kadhi zasema mtu atakaye hama uislamu anyanganywe mali zote maana wa islamu ndio walimsaidia kupata mali hizo.
ama kama baba ni muislam mtoto akahamia dini nyingine basi mtoto yule hana haki ya kupata urithi kutoka kwa baba yake
Jamani sasa hiki kitakuwa ni utendaji wa haki kweli??

KADHI ni sehemu ya Ibadaa sawa ianzisheni basi kwa mtindo wa ibadaa yani IMANI na si kuilazimisha hadi ipewe mamlaka kisheria na ipewe Fungu kutoka serikalini LESS SENSE!!!!
Ktk tarafa yangu hakuna mahakama ya serikali na mharifu lazima apelekwe wilayani miaka ya nyuma ilikuwepo serikali ikaivunja kutokana na hali ya uchumi, sasa hawa wanaokuja na KADHI kuishinikiza serikali IIDHAMINI KADHI ni ukosefu wa uzalendo(patriotism) na nchi yenu nchi masikini ya MWISHO AMA YA PILI KUTOKA MWISHO DUNIANI KWA UMASIKINI bado mnatka kuitwika jizigo jingine.
Utaweza kuabudu kama una njaa wewe acheni hizo yani watanzania tuko KUMUBABAISHA RAIS leo KADHI kesho kile sasa unafikiri atafanya kazi ya kuleta maisha bora saa ngapi????
Mngekuwa mnapigana hivo kuleta maendeleo ya nchi kama mnavopigania KADHI si mambo yangekuwa mswano maana nahisi UKISHIBA NDIO UTAABUDU KIKWELI KWELI lakini kama una njaa baada ya kupiga sala utakuwa unawaza du mbona hii swala ndefuu
WANGWANA TUWE NA PATRIOTISM yani love of patriotism is to volunteer to protect your country
 
Nadhani Raisi wetu anastahili kupata washauri zaidi!

kwa mtazamo wangu kutaka kurusha so hili la KADHI kwa Mrema ni kujidhalilisha!

Ni yeye mwenyewe kwa 'akili zake timamu bila kulazimishwa na mtu yeyote' alipita mitaani na mabonde kuinama ya Tanznaia akiipigia debe na kuiombea kura, Ina maana hakuwa anatumia ubongo wake, alikuwa ame cut na kupaste toka kwa Mrema??

Anapaswa atoke na sababu utetezi ama uungwana wa kukubali sehemu yake na si kutafuta mchawi!
 
Mwana kijiji
Mahakam za katoliki na aglikana ndivyo vivyo tunataka na Kadhi iwe,
yani hakuna bajeti ya serikali kuiendesha mahakam hiyo.
wala haipo kikatiba ama sheria inayofahamika kikatiba kwamba ikikuadhibu hivi lazima adhabu itekelezeke lakini sisi tunacho hoji kuwepo kadhi kikatiba lazima Adhabu zake zitekelezeke.

Pili Serikali yetu ni masikini kupindukia hata mahakama zake hazitosherezi kutokana na bajeti yake kutegemea kwa zaidi ya 40% wadhamini hiyo haitoshi bado tunataka mahakama ya Mtindo tofauti ianzishwe nchi muzima EBWANA WEE UZALENDO WETU UKO WAPI?????????

TAtu lazima waislamu wakubali ukweli huu Nchi NYINGI zinazochangia BAJETI YA TZ Haziko tayari kuona pesa wanazotoa zinahudumia KADHI tena hawa wako tayari kuona MFISADI anaharamia Na kuzikwanyuwa pesa zao kuliko kuona pesa zao zina HUDUMIA KADHI
KADHI ianzishwe na mfuko wa waislamu na waendeshe bila kuingilia katiba ya nchi, hapo atakaye wawangia basi huyo naye anajambo
ngoja niulize swali hivi mtu akitaka kuanzisha msikiti anahitaji mpaka ukajadiliwe na BUNGE???
Hizo zote si hoja, hoja ni UZALENDO TZ NI masikini mno umasiki unatisha waislamu wakristu ishinikizeni jamii ianzishe mambo yanayoikwamua jamii kutoka ktk umasikini.HIZO NDOA MTAZIAMUA NDOA ZIPI ?WAKATI WATU HATUOI NI OA NITAIIRISHA NINI FAMILIA ,HIZO MIRATHI NANI ATAENDA GOMBEA SURUALI YENYE VIRAKA RUKUKI HAIJAFURIWA MIAKA KADHAA NYUMBA MBAVU YA UMBWA YA MATEMBE NA NYASI
WE AFRICAN WHO BE WITCHED US?? nashawishika kukubalina YULE MTAALAMU WA DNA aliyesema african are less intelengent THIS MIGHT BE TRUE
 
Mwankijiji,
Nakuunga mkono na mguu ktk hili isipokuwa ktk kura za No, kupinga kuundwa kwa korti hizi mimi nipo isipokuwa naunga mkono tu kuwepo kwa kipengle cha sheria yetu (KIKATIBA) kinacho deal na maswala ya ndoa, mirathi kwa waislaam wale wanaotaka kuitumia. Kama vile kutumia wataalam wa dini ktk maswala haya.
Kama vile sheria za madini na kadhalika yapo kwa wenye kutaka kuwekesha.
nachowaomba watu hapa ni kujaribu kuondoa UBINAFSI kwani hata swala la pasi na uraia wa nchi mbili limekuwa na Utata mkubwa kwa sababu tu wapo wananchi wasiokuwa na uraia wa nchi mbili hivyo wanaona why sheria itolewe kwa baadhi ya watu waliokwenda Ulaya nje tena wamejengewa na jina WAKIMBIZI wapewe nafuu hii badala ya kuwa ni haki ya hawa watu kimsingi. watu wajaribu ule msemo wa:- What about me?
korti ya kadhi haitufai pamoja na kuwepo nchi nyinginezo kwani hapa kinachotazama ni sisi Watanzania na mazingira yetu.
 
Haya Mzee amelizungumza hilo suala Kadhi kwenye hiyo Shere ya Walutheri, sasa sijui ndio kuomba radhi kwa Mkubwa ni hivyo au kalitolea Ufafanuzi.
Sasa Turudi kwenye suala la Mafisadi.
Maana hapa naona sera ya Devide and Rule ina taka kutumika.
Tusiwe that much cheap
 
Mkamap,
WE AFRICAN WHO BE WITCHED US?? nashawishika kukubalina YULE MTAALAMU WA DNA aliyesema african are less intelengent THIS MIGHT BE TRUE!

It might be true 'cause hatuna sheria inayowalinda wanyonge na wananchi wanapinga kuwepo kwa sheria hiyo kwa sababu ya dini zao.
Unajua mjomba nchi yoyote inayopiga vita ama kutotambua sheria fulani za dini ya wananchi wake kikatiba ina maana wanakataa haki za kimsingi za dini hiyo. Ndivyo wanavyofanya China na urusi enzi zile za Ukommunist!
Hakuna haki yeyote ya kidini inayoweza kukubalika bila kipengele ktk katiba na ndio maana tunawachagua Wabunge ktk kutunga Sheria.
sasa basi yawezekana hawa wazungu wakasema sisi ni less intellegent kwa sababu tunapinga hata vitu vya msingi wakati wao hakuna kitu kinachoweza kupita bila kulindwa na sheria (katiba)!..iwe haki ya watoto, wanawake , vilema ama wanyama. Wanasema kipofu mpe fimbo yake! Sio sisi kila kitu tunatazama wazungu wanasema nini kisha ndio tuna apply kama wao.
Hata kama nchi yetu ni joto basi hutumia Pamba kupamba miti ya Christmas kuiga snow badala ya kufikiria kitu ambacho kinaendana na mazingira yetu..tena basi wengi hushangaa nguo tunazovaa ktk joto lile (Suit kubwa za wool) watakosa kweli kutuita sisi Kabuntas!
 
Back
Top Bottom