JK Atakapokuwa Hana "cha Kupoteza!" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Atakapokuwa Hana "cha Kupoteza!"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Apr 14, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikitafakari jinsi Marais wanapokuwa madarakani katika ungwe ya awamu ya miaka mitano ya mwisho ya uongozi wao, mara kadhaa Marais hao kwa kuwa hawana tena cha kupoteza hubadilika sana. Labda nianze na awamu ya pili ya Mzee Ruksa. Huyu alitaka kuiuza Nchi kwa Waarabu kwa kuitumbukiza kwenye Jumuiya ya OIC kinyemela bila hata ya Bunge kuwa na habari, kisa mafuta na udini! Ameshiriki sana kuuza utajiri wetu kwa Waarabu kupitia kashfa ya Loliondo. Mambo yote haya yalitokea kwenye kipindi cha Pili cha uongozi wake!

  Mzee Mkapa alijulikana sana kama Mr "Clean" kwenye awamu ya kwanza ya uongozi wake, lakini mambo yalibadilika sana katika awamu ya pili. Aligeuka kuwa fisadi la kutisha!

  Mambo haya labda yanafanyika kipindi hiki kwa sababu hawa waheshimiwa hawakuwa na cha kupoteza katika ungwe ya pili ya uongozi wao.

  Kwa upande wa JK alianza vizuri sana na wengi walimpa sifa mbalimbali km: "Tumaini lililorejea, chaguo la Mungu, nk" Mimi kwa upande wangu hata hivyo, kusema ukweli toka moyoni, sijaona matunda ya JK ya kuwaletea maisha bora kwa kila m-TZ kama alivyoahidi. Wala sikutegemea kama angeleta maisha bora kwa kila m-TZ! Amekuwa mtu wa safari nyingi za Marekani, sijui ya sasa ni ya ngapi na sijui ameteketeza mabilioni mangapi kwa safari hizo! Sijui vile vile kama atafuata nyayo za akina Mzee Ruksa na Mzee Ben za kutokujali zaidi katika ungwe ya pili ya uongozi! Let's wait n c!

  Nakaribisha mjadala!
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sehemu iliyopigwa msitari ni "Utumbo na Upupu"

  Uchambuzi wako umejaa dini hadi unakosa akili na busara

  Pole sana.
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Tumain, nahoji busara yako hapo. Unasema sehemu uliyopigia mstari ni utumbo mtu, hilo ni sawa kuwa hukubaliani nalo lakini hiotmisho lako lnasema uchambuzi wake umejaa dini hadi anakosa akili na busara!

  Nadhani wewe ndo umekosa busara kwa kuwa ni sehemu ndogo tu ya uchambuzi (ambayo umeipigia mstari ndo umeituhumu kwa udini sasa iweje unajenga hoja kuwa ni Uchambuzi wote umejaa dini? Huo ni upofu ndugu, hoja kuu ni JK hana cha kupoteza, au kwa kuwa naye ni dini yetu?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hata wewe unajua moyoni mwako kwamba umekosa nukta za kuongea!
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Buchanan umesema kweli. Hata wale wanaompenda JK wana hofu kubwa kuwa akiingia kipindi cha mwisho ataharibu zaidi kwa sababu hana cha kupoteza. Yanayohofiwa kuwa atayafanya bila hofu kipindi hicho, baadhi yake ni:

  -Kuwarejesha rafiki zake aliolazimika kuwatosa ili kuokoa urais wake,
  -Kufuta kesi zinazowakabili baadhi ya wachangiaji wazuri wa chama walio na kesi,
  -Kuchuma hela ya kutosha na kuwekeza ndani na nje,
  -Kuhakikisha anaboresha sheria ya kinga ya marais wakiishastaafu
  -Hataigusa katiba, tume ya uchaguzi, wala ofisi ya msajiri wa vyama
  -Taifa litaingia OIC na mahakama ya kadhi itaruhusiwa ili kutufuta machozi waislam,
  -Atatoa fedha za kutosha kwa mahospitali ya kanisa na mashule ili kuwapoza wakristo,

  Mengine Tumaini aongezee..
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Apr 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sijui this time amekuja na style gani, naona sasa ameanza na sms kuomba TSh 300 kwa wa-TZ ili wachangie CCM! TShs 40bn/- za kampeni! Sijui anahofia nini huyu bwana hata kama amedai kuwa hatazitumia fedha hizi peke yake, still atakazotumia yeye ni nyingi vile vile!
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ndipo atakapofanya kweli ! Kaeni chonnjo mnaojifanya mnachanganya mambo ya siasa na shughuli nyengine.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Atakuwa na cha kupoteza kama hatokuwa makini makosa yale yale ya nyuma yakaendelea kutokea. Kuna siku watanzania watawawajibisha wakuu hawa
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Apr 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nchi hii hajapatikana Kiongozi mwenye uchungu nayo kama alivyokuwa Nyerere ndugu yangu!
   
 10. m

  mtemi Member

  #10
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  atajivunia CHUO KIKUU CHA DODOMA.....aka UDOM
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Apr 16, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280

  ameshawahi kujivunia yeye mwenyewe au unamsemea?
   
 12. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kinachokatisha tamaa ni kwamba hao wenzake awamu zao za kwanza walipiga kazi na sio blaa blaa sasa mkubwa wetu ameanza kutuumiza kuanzia mwanzo nadhani awamu ya mwisho ni kilio tu wala hakuna wema anaoweza kuutenda
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kikubwa atakachofanya ni kuhakikisha utawala unaofuata ni watu wanaomlamba miguu hivi sasa, na ni watiifu kuliko hata kwa wazazi wao waliowazaa.
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Buchanan amechambua vizuri tabia za hawa Marais waliopita na vimbwanga vyao; kama amekukwaza ni shauri yako, lakini ukweli ni huo uliounderline; Mzee Ruksa awamu ya pili alikuwa anaiuza nchi kwa wakwe zake waarabu!!

  Dalili na ishara zinazoonekana sasa ni kwamba Jakaya asipothibitiwa atafanya madudu mabaya zaidi ya hayo waliofanya waliomtangulia [ hasa baada ya ugunduzi wa URANIUM]; salama yetu ni kama tutapata wagombea binafsi bungeni watakaoweza kuyaweka hadharani madudu yake!! Wanajanvi hivi karibuni niliwahi kuwatahadhalisha kuwa alipoitisha kikao cha dharula cha Nec alikuwa anawaweka sawa jamaa kwa safari ya ughaibuni; wengi hawakuamini!!

  Sasa mnajua muungwana yuko wapi?? New York!! Jama hasikii wala haoni vilio vya wadanganyika!!
   
 15. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  No Comment, Niko ndani ya Red Tshirt
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wewe ndio kilaza huwezi kuchambua jambo lolote lile la kitaifa bila kuwataja waislamu na waarabu kwasababu za chuki zako za kidini..inaonyesha uwezo wako mdogo wa kufikiri..pole sana
   
 17. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama ambavyo Kambarage alivyouza kwa wakatoliki?

  Kama ambavyo Mkapa alivyouza kwa Wazungu/makaburu?

  Acheni maongezi ya kijiweni leteni data kwamba mwinyi aliuza nchi kwa waarabu? Wapi? Kiasi gani? Blah blah udini chuki ni ujinga wake Buchanan usijiingize na wewe, kila mwenye akili anajua busara ndogo zake
   
 18. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Alikuwa na uchungu lakini alikuwa "MBAGUZI" wa kufa mtu...hana lolote afadhali anakandamizwa na ardhi kama alivyowakandamiza wengine shit!
   
 19. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jk hana cha kupoteza kwani hata term yake ya kwanza sioni kipi anacho cha kujivunia. Uwezoo wake pia umekuwa kikwazoo cha usimamizi na utekelezaji wa majukukumu ya umma. Yupo New York Kwa mwaliko wa NGOs huku nchii ikiendeleaa kudidimia katika lindi la umaskini.
   
 20. h

  housta Senior Member

  #20
  Apr 16, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima yako mkubwa!

  Kila binadamu ana mapungufu yake na hakuna anayeweza kusimama leo na kusema yeye yupo kamili na Mungu amemuumba na kumpa kila kitu.Kinachotofautisha haya mapungufu ni kiwango.Kuna wenye mapungufu mengi na machache.Buchanan amewasilisha hoja yake.Cha msingi ni kuchangia hoja yake - kuna supporting ideas na critics.Mtu ukiichukulia hoja kama personal attack ndio mwanzo wa kuanza kurushiana maneno machafu.Ninavyoelewa kila mtu ana haki ya kuongea chochote ili mradi tu asivunje sheria.Kwa nini tusiwape haki kila mtu aseme atakalo?

  The only positive thing tunachoweza kufanya ni kuendeleza thread na siyo kutukanana.Kila mtu ana akili - kinachotofautisha ni utimamu au vinginevyo.LAKINI zote ni akili.

  Nawasilisha.
   
Loading...