JK ataka wasomi waandike vitabu.....yeye kaandika vingapi?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
JK awataka wasomi kuandika vitabu

Thursday, 09 December 2010 20:07 newsroom

Na Yassin Kayombo
RAIS Jakaya Kikwete, ametoa mwito kwa wasomi kuandika vitabu vya historia ya maisha ya viongozi wa kitaifa ili kuhifadhi historia ya nchi. Alitoa mwito huo jana, Ikulu, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha yake kilichoandikwa na Profesa Julius Nyangíoro. Kitabu hicho chenye wasifu wa Rais ni cha pili kuandikwa nchini, cha kwanza kiliandikwa mwaka 1971 kuhusu maisha ya Rais wa Kwanza, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere. Kwa mujibu wa Profesa Nyangíoro, msambazaji pekee wa kitabu hicho atakuwa duka la vitabu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
kku.jpg

Katika kitabu hicho, mwandishi Profesa Nyangíoro ameelezea maisha ya Rais Kikwete akiwa mtoto mdogo, elimu, mwanajeshi, mwanasiasa, Waziri na hatimaye rais. Rais alisema wasomi wanapaswa kulisaidia taifa kwa kuandika vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wa kitaifa kwa ajili ya historia ya kizazi kilichopo na kijacho. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, maprofesa na waandishi wa habari, Rais aliwahimiza wananchi kujenga mazoea ya kusoma vitabu vikiwemo vya maisha ya viongozi. Rais alisema viongozi wengi wakiwemo marais wastaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa hawajaandikiwa vitabu kuhusu maisha yao. ìKutoandikwa vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wetu wa kitaifa ni kuua historia ya viongozi hao na ya taifa kwa jumla, hivyo wenye uwezo wa kuandika andikeni,î alisisitiza Rais
 
Nafikiri hii sentensi "RAIS Jakaya Kikwete, ametoa mwito kwa wasomi kuandika vitabu vya historia ya maisha ya viongozi wa kitaifa ili kuhifadhi historia ya nchi." ilitakiwa igusie nyanja zote, kwani tuna vitabu vichache sana vilivyo andikwa na wasomi wetu katika mambo mbali mbali.
 
Tatizo kitakuwa hakiongelei uhalisia wa Jk mwenyewe yaani kitakuwa kinampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Hao waliokwisha toka madarakani itachukua muda kuandikwa historia zao, maana itahitaji waandishi wa kujitoa tofauti na hii ya kuandika aliye madarakani ambapo kazi inaweza kuwa sponsored kwa njia moja au nyingine au mwandishi anaweza kuwa rewarded mbali na mauzo ya kitabu. Naamini nakala za hicho kitabu zitakazouzwa/somwa (perception yangu) zitakuwa chache sana , heri mwandishi angeruhusu kiuzwe hata mitaani. Hata hivyo njia mijawapo ya ku boost sales za kitabu cha maisha ya rais wetu ni kutumia mbinu zinazotumiwa kuuza gazeti la Uhuru
 
Jaman ata yeye amesoma eti, si anaitwa Dk?ana mashada mengi!
 
Kitabu cha maisha ya JK chaandikwa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 9th December 2010 @ 23:50

ATAKUWA Rais wa pili wa Tanzania kuandikiwa wasifu wa maisha yake baada ya wasifu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuandikwa mwaka 1971 na Mzungu William Smith.

Julius Nyang'oro ambaye ni Mkuu wa Idara ya Taaluma za Afrika za Wamarekani Weusi kwenye Chuo Kikuu cha North Carolina – Chapel Hill, ameandika kitabu cha wasifu wa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao wasifu huo ni wa maisha yake ya kisiasa.

Katika uzinduzi uliofanyika Ikulu Dar es Salaam jana, Profesa Nyang'oro alisema amesukumwa na sababu nyingi kuandika wasifu huo, lakini mojawapo ni kuwa marais wawili wa Tanzania, wameondoka madarakani bila ya wasifu wao kuandikwa, hivyo kupoteza kumbukumbu muhimu kwa Taifa.

Anawataja marais hao kuwa ni Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, ambao waliiongoza Tanzania kwa nyakati tofauti kuanza mwaka 1985.

Profesa Nyang'oro alisema ni Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyeiongoza Tanzania kwa miaka 23, ndiye pekee aliyeandikiwa wasifu wake mwaka 1971 na William Smith, hivyo akaona haja ya kuandika wasifu wa Rais Kikwete kwa kuamini kuwa ni vyema wasifu huo
ukaandikwa na Watanzania wenyewe.

"Lakini sababu nyingine ni ya binafsi….kisaikolojia yapo mambo ambayo mimi na Rais Kikwete tumepitia vipindi vinavyofanana.

Na pia mafanikio yake katika kuiongoza Tanzania yamenisukuma kuandika wasifu huu," alisema mtunzi huyo wa kitabu hicho chenye kurasa 308 na sura 11.

"Ushindi wake wa asilimia zaidi ya 80 katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, ni tukio la nadra ulimwenguni hasa kwa chama tawala.

Lakini amefanya mambo mengi akiwa madarakani na amekuwa na changamoto nyingi kuliko marais wengi waliomtangulia, ukiacha changamoto ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa," alisema.

"Suala la ajira kwa vijana ni mojawapo ya changamoto hizo, na katika hili, rais ameonesha maslahi makubwa kwao.

Lakini kumekuwapo na mabadiliko ya kiteknolojia, kwa maana watu wanayajua yanayoendelea kila mahali, hivyo utendaji wake wa kazi unapimwa kwa
kuwalinganisha na marais wengine duniani.

"Lakini pia zipo changamoto ya mazingira ya kila siku, na hasa sasa suala la uchumi. Hii ni changamoto mojawapo, ingawa rais amefanya kazi kubwa katika masuala ya ajira kwa vijana, elimu na mengine," alieleza Profesa Nyang'oro katika uzinduzi huo uliowashirikisha pia Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mama Salma Kikwete, familia ya Rais, mawaziri na wageni mbalimbali waalikwa.

Alisema kazi ya kuandika kitabu hicho kilichoandikwa kwa Kiswahili na Kiingereza, ilimchukua miaka mitatu, na alimshukuru Rais Kikwete kwa kukubali kiandikwe pamoja na watu wengine waliomsaidia kuandaa kitabu hicho ambacho juzuu ya pili itakuwa ni baada ya
Rais kumaliza muda wake Ikulu.

Akifanya uchambuzi wa kitabu hicho, Profesa Severine Rugumamu wa Taasisi ya Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema wasifu huo umeandikwa vizuri kwenye mazingira ya historia, taasisi za siasa na jamii za Tanzania pamoja na mahusiano ya kisiasa na
kiuchumi ya nchi na dunia nzima.

Naye Rais Kikwete alimshukuru mtunzi wa kitabu hicho ambacho kitauzwa katika duka la vitabu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pekee, na kueleza kuwa kama yupo ambaye ataona mapungufu katika kitabu hicho ni bora akaandika cha kwanza, badala ya kumlaumu
mtunzi.

Alisisitiza umuhimu wa kuandikwa kwa historia za viongozi nchini kwa sababu zinasaidia katika kuweka kumbukumbu muhimu za historia ya nchi, maamuzi, sera na hatua mbalimbali alizochukua kiongozi husika.

Alirudia mwito wake wa kuwataka Watanzania wasome vitabu, lakini pia wanataaluma kuandika vitabu kwa nia ya kuhifadhi kumbukumbu za nchi.

Tatizo la JK ni kujaribu kujilinganisha na J.K. Nyerere ambaye kwenye uhai wake aliandika yeye mwenyewe vitabu vingi.............................angalia eneo nililoweka alama nyekundu kwa ufafanuzi zaidi..................
 
Ningekuwa mimi JK, ningegusia dongo alilopigwa mwandishi wa kitabu na mhariri wa kitabu hicho kuwa uandishi wake wa hicho kitabu umegusia upande mmoja tu wa 'mema' na mazuri ya JK na kuacha kabisa mapungufu yake na changamoto za wazi zinazomkabili.

Hakuna umuhimu wa kuandika vitabu ambavyo haviko objective, huko ni sawa na kuwalisha matapishi wasomaji, huku vizazi vyetu vikitushangaa kwa kusifiana bila msingi wowote!!
 
Yes mkuu, nilimsikia Prof. Rugumamu aki-criticise kitabu hicho jana!!.. akisema kimelenga mazuru yake tu bila kugusia mapungufu yake..... Tehe teh... tatizo la viongozi wa Africa tunapenda kupewa misifa tu hata ambayo hatuna!!!! Bado tuna safari ndefu kwelikweli..... No objectivity at all..
Ningekuwa mimi JK, ningegusia dongo alilopigwa mwandishi wa kitabu na mhariri wa kitabu hicho kuwa uandishi wake wa hicho kitabu umegusia upande mmoja tu wa 'mema' na mazuri ya JK na kuacha kabisa mapungufu yake na changamoto za wazi zinazomkabili.

Hakuna umuhimu wa kuandika vitabu ambavyo haviko objective, huko ni sawa na kuwalisha matapishi wasomaji, huku vizazi vyetu vikitushangaa kwa kusifiana bila msingi wowote!!
 
kitabu cha maisha ya jk chaandikwa
imeandikwa na mwandishi wetu; tarehe: 9th december 2010 @ 23:50

atakuwa rais wa pili wa tanzania kuandikiwa wasifu wa maisha yake baada ya wasifu wa baba wa taifa, mwalimu nyerere kuandikwa mwaka 1971 na mzungu william smith.

julius nyang'oro ambaye ni mkuu wa idara ya taaluma za afrika za wamarekani weusi kwenye chuo kikuu cha north carolina – chapel hill, ameandika kitabu cha wasifu wa jakaya mrisho kikwete, rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, ambao wasifu huo ni wa maisha yake ya kisiasa.

Katika uzinduzi uliofanyika ikulu dar es salaam jana, profesa nyang'oro alisema amesukumwa na sababu nyingi kuandika wasifu huo, lakini mojawapo ni kuwa marais wawili wa tanzania, wameondoka madarakani bila ya wasifu wao kuandikwa, hivyo kupoteza kumbukumbu muhimu kwa taifa.

Anawataja marais hao kuwa ni alhaj ali hassan mwinyi na benjamin mkapa, ambao waliiongoza tanzania kwa nyakati tofauti kuanza mwaka 1985.

Profesa nyang'oro alisema ni baba wa taifa mwalimu nyerere aliyeiongoza tanzania kwa miaka 23, ndiye pekee aliyeandikiwa wasifu wake mwaka 1971 na william smith, hivyo akaona haja ya kuandika wasifu wa rais kikwete kwa kuamini kuwa ni vyema wasifu huo
ukaandikwa na watanzania wenyewe.

"lakini sababu nyingine ni ya binafsi….kisaikolojia yapo mambo ambayo mimi na rais kikwete tumepitia vipindi vinavyofanana.

Na pia mafanikio yake katika kuiongoza tanzania yamenisukuma kuandika wasifu huu," alisema mtunzi huyo wa kitabu hicho chenye kurasa 308 na sura 11.

"ushindi wake wa asilimia zaidi ya 80 katika uchaguzi mkuu wa 2005, ni tukio la nadra ulimwenguni hasa kwa chama tawala.

Lakini amefanya mambo mengi akiwa madarakani na amekuwa na changamoto nyingi kuliko marais wengi waliomtangulia, ukiacha changamoto ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa," alisema.

"suala la ajira kwa vijana ni mojawapo ya changamoto hizo, na katika hili, rais ameonesha maslahi makubwa kwao.

Lakini kumekuwapo na mabadiliko ya kiteknolojia, kwa maana watu wanayajua yanayoendelea kila mahali, hivyo utendaji wake wa kazi unapimwa kwa
kuwalinganisha na marais wengine duniani.

"lakini pia zipo changamoto ya mazingira ya kila siku, na hasa sasa suala la uchumi. Hii ni changamoto mojawapo, ingawa rais amefanya kazi kubwa katika masuala ya ajira kwa vijana, elimu na mengine," alieleza profesa nyang'oro katika uzinduzi huo uliowashirikisha pia makamu wa rais, dk. Mohamed gharib bilal, waziri mkuu mizengo pinda, mama salma kikwete, familia ya rais, mawaziri na wageni mbalimbali waalikwa.

Alisema kazi ya kuandika kitabu hicho kilichoandikwa kwa kiswahili na kiingereza, ilimchukua miaka mitatu, na alimshukuru rais kikwete kwa kukubali kiandikwe pamoja na watu wengine waliomsaidia kuandaa kitabu hicho ambacho juzuu ya pili itakuwa ni baada ya
rais kumaliza muda wake ikulu.

Akifanya uchambuzi wa kitabu hicho, profesa severine rugumamu wa taasisi ya maendeleo ya chuo kikuu cha dar es salaam, alisema wasifu huo umeandikwa vizuri kwenye mazingira ya historia, taasisi za siasa na jamii za tanzania pamoja na mahusiano ya kisiasa na
kiuchumi ya nchi na dunia nzima.

Naye rais kikwete alimshukuru mtunzi wa kitabu hicho ambacho kitauzwa katika duka la vitabu la chuo kikuu cha dar es salaam (udsm) pekee, na kueleza kuwa kama yupo ambaye ataona mapungufu katika kitabu hicho ni bora akaandika cha kwanza, badala ya kumlaumu
mtunzi.

Alisisitiza umuhimu wa kuandikwa kwa historia za viongozi nchini kwa sababu zinasaidia katika kuweka kumbukumbu muhimu za historia ya nchi, maamuzi, sera na hatua mbalimbali alizochukua kiongozi husika.

Alirudia mwito wake wa kuwataka watanzania wasome vitabu, lakini pia wanataaluma kuandika vitabu kwa nia ya kuhifadhi kumbukumbu za nchi.

tatizo la jk ni kujaribu kujilinganisha na j.k. Nyerere ambaye kwenye uhai wake aliandika yeye mwenyewe vitabu vingi.............................angalia eneo nililoweka alama nyekundu kwa ufafanuzi zaidi..................

lets talk some business people ok! First thanks brother ruda. You good bro. I realized most of are not econ or business major, thats ok, we all the same. Here the thing, do you know what kikwete said in economic terms. I know you know it. Can you say this in english, watanzania uchumi wenu mmeukalia, alafu nambie kabla sijakukomfyuzi sana. You worryinng too much about kikwete, he is president ok be it. For on positive not negative, you guys like to say that.
 
JK awataka wasomi kuandika vitabu

Thursday, 09 December 2010 20:07 newsroom

Na Yassin Kayombo
RAIS Jakaya Kikwete, ametoa mwito kwa wasomi kuandika vitabu vya historia ya maisha ya viongozi wa kitaifa ili kuhifadhi historia ya nchi. Alitoa mwito huo jana, Ikulu, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha yake kilichoandikwa na Profesa Julius Nyangíoro. Kitabu hicho chenye wasifu wa Rais ni cha pili kuandikwa nchini, cha kwanza kiliandikwa mwaka 1971 kuhusu maisha ya Rais wa Kwanza, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere. Kwa mujibu wa Profesa Nyangíoro, msambazaji pekee wa kitabu hicho atakuwa duka la vitabu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
kku.jpg

Katika kitabu hicho, mwandishi Profesa Nyangíoro ameelezea maisha ya Rais Kikwete akiwa mtoto mdogo, elimu, mwanajeshi, mwanasiasa, Waziri na hatimaye rais. Rais alisema wasomi wanapaswa kulisaidia taifa kwa kuandika vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wa kitaifa kwa ajili ya historia ya kizazi kilichopo na kijacho. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, maprofesa na waandishi wa habari, Rais aliwahimiza wananchi kujenga mazoea ya kusoma vitabu vikiwemo vya maisha ya viongozi. Rais alisema viongozi wengi wakiwemo marais wastaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa hawajaandikiwa vitabu kuhusu maisha yao. ìKutoandikwa vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wetu wa kitaifa ni kuua historia ya viongozi hao na ya taifa kwa jumla, hivyo wenye uwezo wa kuandika andikeni,î alisisitiza Rais

I think we could analyze this and figured out the specific beneficiaries such as youths and business make a scalable move upward from this rukhsa ya kutunga vitabu, please keep us posted, I think Orgainization Wabunifu USA may support development project on public financial leterary. i think most people would like to learn how to swim before jumping into the water., Lets not be wapinga maendeleo and let kikwete have all the attentions, let the people benefits, and also to learn how to be financially sustable based on their income, at how to balance a check book if any. including open a real bank account for a business. bank account for wajasirimali etc. just like mwalim said if you wanna help the poor educate their children. These its like if wanna help the poor give them a monster scums microloans without telling what are they getting into. its quite interesting world myfriend. I think its time for a villegers man to make a change in economic terms. this innitiative is awesome, but still he needs to do more on education especially, we need more colleges and university and maktabas. and lastly, if possible lets design a program to support a highschool drop outs, so that it will be easier for them to enter the workforce and some computer slkils. Brother Ruda, can you actually follow these things. well ukijaaliwa!
 
jk awataka wasomi kuandika vitabu

thursday, 09 december 2010 20:07 newsroom

na yassin kayombo
rais jakaya kikwete, ametoa mwito kwa wasomi kuandika vitabu vya historia ya maisha ya viongozi wa kitaifa ili kuhifadhi historia ya nchi. Alitoa mwito huo jana, ikulu, dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha yake kilichoandikwa na profesa julius nyangíoro. Kitabu hicho chenye wasifu wa rais ni cha pili kuandikwa nchini, cha kwanza kiliandikwa mwaka 1971 kuhusu maisha ya rais wa kwanza, baba wa taifa hayati mwalimu nyerere. Kwa mujibu wa profesa nyangíoro, msambazaji pekee wa kitabu hicho atakuwa duka la vitabu la chuo kikuu cha dar es salaam.
kku.jpg

katika kitabu hicho, mwandishi profesa nyangíoro ameelezea maisha ya rais kikwete akiwa mtoto mdogo, elimu, mwanajeshi, mwanasiasa, waziri na hatimaye rais. rais alisema wasomi wanapaswa kulisaidia taifa kwa kuandika vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wa kitaifa kwa ajili ya historia ya kizazi kilichopo na kijacho. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na makamu wa rais, dk. Mohammed gharib bilal, waziri mkuu mizengo pinda, waziri mkuu mstaafu, joseph warioba, maprofesa na waandishi wa habari, rais aliwahimiza wananchi kujenga mazoea ya kusoma vitabu vikiwemo vya maisha ya viongozi. Rais alisema viongozi wengi wakiwemo marais wastaafu wa awamu ya pili, ali hassan mwinyi na rais mstaafu wa awamu ya tatu, benjamin mkapa hawajaandikiwa vitabu kuhusu maisha yao. ìkutoandikwa vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wetu wa kitaifa ni kuua historia ya viongozi hao na ya taifa kwa jumla, hivyo wenye uwezo wa kuandika andikeni,î alisisitiza rais

kumbeee ndio maana
 
Back
Top Bottom