Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,172
JK awataka wasomi kuandika vitabu
Thursday, 09 December 2010 20:07 newsroom
Na Yassin Kayombo
RAIS Jakaya Kikwete, ametoa mwito kwa wasomi kuandika vitabu vya historia ya maisha ya viongozi wa kitaifa ili kuhifadhi historia ya nchi. Alitoa mwito huo jana, Ikulu, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha yake kilichoandikwa na Profesa Julius Nyangíoro. Kitabu hicho chenye wasifu wa Rais ni cha pili kuandikwa nchini, cha kwanza kiliandikwa mwaka 1971 kuhusu maisha ya Rais wa Kwanza, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere. Kwa mujibu wa Profesa Nyangíoro, msambazaji pekee wa kitabu hicho atakuwa duka la vitabu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika kitabu hicho, mwandishi Profesa Nyangíoro ameelezea maisha ya Rais Kikwete akiwa mtoto mdogo, elimu, mwanajeshi, mwanasiasa, Waziri na hatimaye rais. Rais alisema wasomi wanapaswa kulisaidia taifa kwa kuandika vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wa kitaifa kwa ajili ya historia ya kizazi kilichopo na kijacho. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, maprofesa na waandishi wa habari, Rais aliwahimiza wananchi kujenga mazoea ya kusoma vitabu vikiwemo vya maisha ya viongozi. Rais alisema viongozi wengi wakiwemo marais wastaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa hawajaandikiwa vitabu kuhusu maisha yao. ìKutoandikwa vitabu vinavyozungumzia maisha ya viongozi wetu wa kitaifa ni kuua historia ya viongozi hao na ya taifa kwa jumla, hivyo wenye uwezo wa kuandika andikeni,î alisisitiza Rais