JK ataka tena urais wa kuendela kuwalea mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ataka tena urais wa kuendela kuwalea mafisadi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Aug 11, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kila nikiangalia, naona JK anashindwa, au anawaonea haya viongozi wanaotuhumiwa na ufisadi. Kwa maana nyingine, anaonekana anawalea. Swali ninalojiuliza ni jee, anaomba kura ili aendelee kuwalea hawa mafisadi?
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana yake, kwani aliingia madarakani kwa fedha ya kifisadi, kwa lugha nyingine ni kuwa ufisadi hapa tz ni mfumo dola, na yeye JK ni sehemu ya mfumo huo , hawezi kujitafuna mwenyewe, kwani akianza kuwagusa na yeye hatapona.CHAGUA CHADEMA KUONDOA UFISADI
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ki hulka!!!

  Jk si mtu wa kuweza wala kudhubutu Kusimama dhidi ya tuseme, TYRANTS AND DICTATORS. Hakuumbwa au hakujengeka hivyo! He is too sweet and pleasing!! Anaweza kufanya mambo mengi mazuri sana na kiukweli amayefanya .... LAKINI si kuwa wajibisha mafisadi wajeuri, wakatili na wakaidi!! Na hasa wengi kama marafiki na washiriki wa karibu!!! Anaishiwa nguvu na kusikia kuwaunga mkono kila anapotaka kuchukua hautua yoyote dhidi yao!!

  Jambo la mshangao!

  Kwa hali aliyonayo bado ameweza kuindesha nchi kwa miaka mitano hadi ilipo sasa! Tuseme ana kipaji kizuri cha uongozi wa jamii iliyo lala!!!? Au siri ya mafanikio yake ni nini?
   
 4. n

  njori Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wachangiaji mnaelewa maana ya urais?kagombeeni urais muone!
  kama huoni alichofanya nenda kijijini kwako kama mnajua hata njia,mmezoea Dar mnafikiri ndio kwenu!!mmechina nyie!
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Swala hapa sio Jk hajafanya kitu bali mtoa mada ameuliza "Anaomba kura ili aendelee kuwalea mafisadi?"
  Jibu hoja ya kuwalea mafisadi kwanza.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwenye rangi: Ndiyo hasa -- na kwa maana hiyo kama urais ni hivyo anavyuchukulia muungwana, basi mtu yeyote anaweza kuwa rais wa hapa Bongo!
   
 7. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mwonja asali haonji mara moja.
   
 8. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni wazi kwamba JK hapaswi kuchaguliwa tena kuongoza nchi hii kwa sababu kazi ra urais imemshinda. Huwezi kuwa rais halafu ukawa rafiki mkubwa wa mafisadi wanaoiangamiza nchi. Tatizo kubwa la nchi yetu ni umaskini unaosababishwa na kukosekana kwa utawala bora (good governance) na rule of law. Watu wanakwiba raslimali za nchi na kuachiwa hivi hivi. Miongoni mwa vituko alivyofanya JK ni pale alipowataka wezi wa fedha za EPA kuzirejesha (sijui kama walizirejesha kweli!) halafu akawaachia huru na kuanzisha sinema ya kuwashitaki wale walioshindwa kuzirejesha. This is ridiculous! Sidhani kama hii imewahi kutokea nchi yoyote duniani. Mwizi yeyote hufikishwa kwanza mahakamani na kuiachia sheria ichukue mkondo wake.
   
Loading...