JK ataka Afrika iandikwe vizuri

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
JK ataka Afrika iandikwe vizuri
Claud Gwandu, Arusha
Daily News; Tuesday,May 20, 2008 @00:03

Rais Jakaya Kikwete amevitaka vyombo vya habari vya nchi za Magharibi kuacha kuandika habari mbaya tu za nchi za Afrika na badala yake waandike mazuri yatakayovutia watalii.

Akifungua mkutano wa 33 wa chama kinachoshughulika na huduma kwa watalii Afrika (ATA) mjini hapa jana, Rais Kikwete alisema bara la Afrika lina mambo mengi mazuri ya kuandika.

“Kila mara kukitokea Darfur kuna tatizo wanaandika Afrika, kama pale Mogadishu kuna mapambano wanasema Afrika. Hii siyo sahihi kuna mengi mazuri ya kuandika juu ya bara letu,” alisema Kikwete.

Alisema Bara la Afrika leo ni tofauti sana na ilivyokuwa miongo mitatu, miwili au miaka kadhaa iliyopita kwa kuwa sasa kuna demokrasia zaidi kuliko huko nyuma. Bara hili ambalo lina vivutio vingi vya utali halifaidiki na biashara kubwa ya utalii ya kimataifa kutokana na kuwa na miundombinu hafifu ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea, alisema.

Akitoa takwimu, Rais Kikwete alisema inakadiriwa kuwa Afrika itapokea watalii milioni 47 ifikapo mwaka 2010 na watalii milioni 77.3 mwaka 2020, ukuaji wa kiwango cha asilimia 5.5 kwa mwaka.

Hata hivyo, alisema kwa dunia nzima inakadiriwa kuwa kutakuwa na watalii bilioni moja ifikapo mwaka 2010 na bilioni 1.6 mwaka 2020, jambo linaloonyesha Afrika ipo nyuma ingawa ina rasilimali nyingi.

“Bara letu limejaliwa kuwa na vivutio vingi vya asili, lakini kiasi linachopata katika biashara ya utalii ni kidogo hivyo ni wakati wa kuiongezea uwezo Afrika ili iweze kupambana na umasikini kwa kutumia rasilimali hizo,” alisisitiza Rais Kikwete.

Awali, akimkaribisha Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga alisema utalii hivi sasa ndiyo sekta inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha zaidi za kigeni. Alisema watalii 719,031 walitembelea Tanzania mwaka 2007 na kuliingizia taifa dola za Marekani bilioni moja na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mwaka huu.

Alisema makadirio yanaonyesha kwamba ifikapo mwaka 2010, Tanzania itatembelewa na watalii milioni moja ambao wataingiza fedha zaidi za kigeni na lengo likiwa ni kupata watalii wengi kutoka Marekani. Mkutano huo wa siku tano unahudhuriwa na wadau katika sekta ya utalii kutoka kila pembe ya dunia na hii ni mara ya pili kwa mkutano huo kufanyika nchini. Mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1998.
 
Kama hawafanyi mambo mazuri wanategemea nani atayaandika? Serikali yake imeshika wapemba na kuwaweka ndani huku bado kukiwa na kumbukumbu za mauaji ya mwaka 95-95, 00-01, na 05-06.

Kama huheshimu haki za msingi za raia wako, unategemea nani atakuandika vizuri?
 
JK ataka Afrika iandikwe vizuri
Claud Gwandu, Arusha
Daily News; Tuesday,May 20, 2008 @00:03

Rais Jakaya Kikwete amevitaka vyombo vya habari vya nchi za Magharibi kuacha kuandika habari mbaya tu za nchi za Afrika na badala yake waandike mazuri yatakayovutia watalii.

Akifungua mkutano wa 33 wa chama kinachoshughulika na huduma kwa watalii Afrika (ATA) mjini hapa jana, Rais Kikwete alisema bara la Afrika lina mambo mengi mazuri ya kuandika.

“Kila mara kukitokea Darfur kuna tatizo wanaandika Afrika, kama pale Mogadishu kuna mapambano wanasema Afrika. Hii siyo sahihi kuna mengi mazuri ya kuandika juu ya bara letu,” alisema Kikwete.

Jk hayo mazuri kama yepi kama sio njaa na vita na ufisadi?

Alisema Bara la Afrika leo ni tofauti sana na ilivyokuwa miongo mitatu, miwili au miaka kadhaa iliyopita kwa kuwa sasa kuna demokrasia zaidi kuliko huko nyuma. Bara hili ambalo lina vivutio vingi vya utali halifaidiki na biashara kubwa ya utalii ya kimataifa kutokana na kuwa na miundombinu hafifu ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea, alisema.

Kumbe unajua...litafaidika vipi ikiwa vijisenti hivyo mnavipeleka offshore na kujaza matumbo yetu?


“Bara letu limejaliwa kuwa na vivutio vingi vya asili, lakini kiasi linachopata katika biashara ya utalii ni kidogo hivyo ni wakati wa kuiongezea uwezo Afrika ili iweze kupambana na umasikini kwa kutumia rasilimali hizi,” alisisitiza Rais Kikwete.

Kidogo?....shame on you.... we mpaka leo unaogopa kupokea hiyo ripoti ya tume ya madini halafu kwa macho makavu bado unaongelea rasilimali..

Awali, akimkaribisha Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga alisema utalii hivi sasa ndiyo sekta inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha zaidi za kigeni. Alisema watalii 719,031 walitembelea Tanzania mwaka 2007 na kuliingizia taifa dola za Marekani bilioni moja na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mwaka huu.

Sasa hayo mapesa yamesaidia nini wananchi au infrastucture?.......NIL..ilibidi uongelee ndio hata waandishi wa habari wakaandika waTZ wamenufaika vipi na hizo income...kumbe pesa mnapata na bado mnalia mnataka nyingi, jamani hizo haziwatoshi?
 
Hata kama Watanzania/Waafrika wenye mapenzi ya kweli na Tanzania/Afrika ndio wangekuwa wanaandika au kutangaza katika vyombo vya magharibi bado habari zingekuwa mbaya tu. Angalia Nigeria pamoja na utajiri mkubwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya wananchi wake wanaishi katika dhiki kubwa. Angalia Afrika Kusini bado asilimia kubwa ya wananchi wake wanaishi katika dhiki kubwa, pamoja na hayo sirikali ya nchi hiyo haikuona haya wala kusikia vibaya kutumia mabilioni ya fedha kugharamia kombe la dunia hapo 2010. Hali kadhalika Tanzania nayo mafisadi wa mabilioni ya shilingi hadi hii leo hakuna hata aliyeguswa. Ni kipi kizuri cha kuandika? Kwamba idadi ya watalii wameongezeka!!!!? Je kuongezeka huko kumenyanyua vipi kiwango cha maisha ya Watanzania? Jibu tunalijua.
 
Sio siri yaani watu nje ya africa wanachukulia africa vibaya sana watu wengine hawajui wengine kama africa watu wanaishi kwenye nyumba wanajua watu wanaishi kwenye miti na ni magonjwa na matatizo matupu.Ndio Kuna shida ila sio kipimo kinachopimiwa huku nje duh.Na si walaumu kwa kuwa media zinashinda zianonyesha ivyo.
 
Hata mimi nikitaka kuongelea Tanzania siwezi kusema mazuri yake, sababu ni machache ukilinganisha na machafu. Naweza sema natokea Tanzania kisiwa cha Amani, swala linakuja jee ni amani gani wakati kuna walimu wananashindwa kutibiwa sababu kiongozi wao anatibiwa kwa million za shilingi peke yake. Ni amani gani wakati hakuna barabara mahususi inanayo unganisha watanzania walio kona mbili tofauti za Tanzania, nasema ni amani gani wakati Pemba hakuna huduma za kijamii sababu wanachagua CUF kwenye chaguzi kuu.

Naendelea kujiuliza jee hii amani anayongelea JK ni ipi wakati wakazi wa Kibwa, Bariadi, Kahama hawana huduma za afya, elimu bora wakati wanakalia madini yenye thamani kubwa sana. Jee ni amani gani wakati baadhi ya vigogo wa CCM wana mamilion ya dolla kwenye account za nje huku Watanzania wanafariki pale Muhimbili sababu hakuna mitungi ya oxygen. Jee ni amani gani JK anayongelea? Huu sio muda wa kuficha kidonda kwani haina maana kabisa.

JK anataka western countries zizungumzie nini, Ngorongoro creter? Wakati mamilioni ya watanzania hawafaidiki kutokana na cretor hiyo. Au anataka wazungumzie mlima Kilimanjaro wakati wakazi wa Kilimanjaro hawapati maji safi. Jk anataka watu wazungumzie nini bora ndani ya Tanzania?

Hakuna cha kuzungumzia, the system is broken and no one is working hard to fix it.
 
anataka waandike vizuri yaani wamsifie? zile sifa alizopewa na waandishi uchwara kuwa eti haijapata kutokea kwa kuwa alitembelea magereza kwenda kuwasanifu wafungwa? au HAIJAPATA KUTOKEA KIKWETE MWISHO KABISA kwa kuwa tu alikuwa anatalii kila wizara? anataka waandike lipi? shule za za sekondari uchwara zilizojengwa kwa kelele nyingi kila kata? shule ambazo wanafunzi waliofanya vizuri msingi wanadanganywa kujiunga na shule uchwara zisizo na waalimu huku vipaji vyao vikiishia huko huko huko vijijini kwakukosa walimu hasa wa sayansi?anataka kusifiwa kwa hili? wakati watoto wao wanasoma ulaya na maerkani wameanzisha makambi haya wanayoyaita shule ili watoto wetu wasipate elimu bora wabaki vijijini, ili siku moja watoto wao waendelee kutawala wa kwetu?ANATAKA KUSIFIWA KWA HILI?

waandike yapi? kuhusu karume kuendelea kuitawala zanzibar huku akijua kua hakubaliki unguja na hali akikataa kuwaingiza wapemba kwennye serikali ya umoja kuijenga zanzabar? anataka kusifiwa kwani amafanya nini cha maana kwa wazanzibar hawa?
anataka kusifiwa kwa lipi? kama mwenyekiti wa AU, wazimbabwe wanachinjana wenyewe na hadi sasa haeleweki anaeegemea wapi? waandike kipi kizuri cha africa? kuhusu joseph kony kuendelee kuteka mamia ya watoto na kutokomea nao msituni? huku kikwete na akina museveni wakitafuta sifa kwa kuunda shirikisho la afrika masha riki au kugharamia mabilioni kwa mikutano ya kujitukuza kama CHOGM NA SULLIVAN FOUNDATION?
waandike yapi? wakati viongozi wetu wamewagawa wananchi kwa misingi ya itikadi, udini, ukabila na kusahau utaifa wao?
kwa kweli hawana cha kuandika, MIKONO YAO ILIYOSHIKA KALAMU HIZO NI LAZIMA IWE MIZITO, HAWAWEZI KUACHA HABARI NZURI KAMA ZA AKINA OBAMA, ETI WAANDIKE MASIFU NA LITANIA ZA KUASIFU MAFISADI WA AAFRIKA, KAMWAE KIKWETE FIKIRIA TENA
 
Afrika itaandikwa vizuri kama matendo yetu na yataendana na misingi ya haki an utawala bora. Kwa mfano angalia matukio yafuatayo:
1. Kuua na kuchoma moto wageni Afrika Kusini
2. Uchaguzi usio huru na haki Zimbabwe
3. Wizi wa mali ya umma Tanzania

Tukirudi nyuma, Ni yapi ya maana ambayo yametokea katika nchi ya Tanzania katika kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari ambayo Serikali yetu inaweza kujisifia?

My Take: Positive press will come when Africans start doing positive things.
 
binafsi nikiangalia hizo channel za wakoloni naona wanachotangaza kuhusu afrika kiko wazi na ni ukweli, kama ni darful wanaelezea hali halisi, kama ni somalia hali kadhalika, so jamaa anataka waeleze mazuri yepi?
au waonyeshe chenge alivyopokelewa na vipofu bariadi?
 
Tanzania, mojawapo ya nchi tatu masikini zaidi duniani! Leo JK anaomba nayo iandikwe kwa mazuri, Je ni mazuri yapi hayo? Ni nyanja gani unaweza kuizungumzia kwa mazuri, iwapo viongozi wake u-invest, pamoja na kuhifadhi fedha nje ya bara lao? kutibiwa nje ya bara lao! shopping nje ya bara lao! Elimu ya juu nje ya bara lao! Wataalamu wa kuandika mikataba mizuri isiyo na 10% (wala unyonyaji) wanapatikana nje ya bara lao! ... sasa lipi limebaki la kuandika kuhusu bara lao!

JK lazima afahamu
palipo na rushwa, hakuna utalii
palipo na manung'uniko ama ghasia, hakuna utalii (ZNZ ndipo inapoelekea!)
pasipo na uwazi na uwajibikaji, hakuna utalii (Wizara ya Utalii na Maliasili bado wako njozini, huku waki-enjoy mvinyo wao pamoja na wageni wachache!!)
 
JK aanze na Zanzibar ukandamizaji , Kukata rufaa dhidi ya mgombea binafsi, wizi na uongo majukwaani .Akimaliza haya wanaweza kuwa na mambo ya kuandika na si zaidi ya hapo.
 
Yanayoandikwa mabaya nikweli. nayatabakia hivyo hivyo, huwezi kuuficha moshi

JK fanya mazuri uihakikishie dunia kwamba unaweza kuiongoza nchi masikini nakuwa mfano kwa mataifa mengine ya Afrika, lakini kama unaendekeza maskendo basi wamagharibi wataandika mabaya yako nakusahau uzuri wa mbuga zetu, nchi yetu nzuri, buzwagi yetu, nk.
 
Back
Top Bottom