BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
JK ataka Afrika iandikwe vizuri
Claud Gwandu, Arusha
Daily News; Tuesday,May 20, 2008 @00:03
Rais Jakaya Kikwete amevitaka vyombo vya habari vya nchi za Magharibi kuacha kuandika habari mbaya tu za nchi za Afrika na badala yake waandike mazuri yatakayovutia watalii.
Akifungua mkutano wa 33 wa chama kinachoshughulika na huduma kwa watalii Afrika (ATA) mjini hapa jana, Rais Kikwete alisema bara la Afrika lina mambo mengi mazuri ya kuandika.
Kila mara kukitokea Darfur kuna tatizo wanaandika Afrika, kama pale Mogadishu kuna mapambano wanasema Afrika. Hii siyo sahihi kuna mengi mazuri ya kuandika juu ya bara letu, alisema Kikwete.
Alisema Bara la Afrika leo ni tofauti sana na ilivyokuwa miongo mitatu, miwili au miaka kadhaa iliyopita kwa kuwa sasa kuna demokrasia zaidi kuliko huko nyuma. Bara hili ambalo lina vivutio vingi vya utali halifaidiki na biashara kubwa ya utalii ya kimataifa kutokana na kuwa na miundombinu hafifu ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea, alisema.
Akitoa takwimu, Rais Kikwete alisema inakadiriwa kuwa Afrika itapokea watalii milioni 47 ifikapo mwaka 2010 na watalii milioni 77.3 mwaka 2020, ukuaji wa kiwango cha asilimia 5.5 kwa mwaka.
Hata hivyo, alisema kwa dunia nzima inakadiriwa kuwa kutakuwa na watalii bilioni moja ifikapo mwaka 2010 na bilioni 1.6 mwaka 2020, jambo linaloonyesha Afrika ipo nyuma ingawa ina rasilimali nyingi.
Bara letu limejaliwa kuwa na vivutio vingi vya asili, lakini kiasi linachopata katika biashara ya utalii ni kidogo hivyo ni wakati wa kuiongezea uwezo Afrika ili iweze kupambana na umasikini kwa kutumia rasilimali hizo, alisisitiza Rais Kikwete.
Awali, akimkaribisha Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga alisema utalii hivi sasa ndiyo sekta inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha zaidi za kigeni. Alisema watalii 719,031 walitembelea Tanzania mwaka 2007 na kuliingizia taifa dola za Marekani bilioni moja na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mwaka huu.
Alisema makadirio yanaonyesha kwamba ifikapo mwaka 2010, Tanzania itatembelewa na watalii milioni moja ambao wataingiza fedha zaidi za kigeni na lengo likiwa ni kupata watalii wengi kutoka Marekani. Mkutano huo wa siku tano unahudhuriwa na wadau katika sekta ya utalii kutoka kila pembe ya dunia na hii ni mara ya pili kwa mkutano huo kufanyika nchini. Mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1998.